Jinsi Ya Kumwanzishia Mtoto Vyakula Vigumu Kwa Njia Inayo Faa

Jinsi Ya Kumwanzishia Mtoto Vyakula Vigumu Kwa Njia Inayo Faa

Mama anapaswa kuhakikisha kuwa anamlisha mtoto maziwa ya mama peke yake katika miezi sita ya kwanza ya maisha yake. Soma zaidi jinsi ya kumwanzishia vyakula vigumu.

Shirika la Afya Duniani lina shauri kunyonyesha mtoto peke yake bila kumlisha kitu kingine kwa miezi ya kwanza sita ya maisha yake. Katika kipindi hiki, haupaswi kumpa kitu kingine chochote mbali na maziwa ya mama. Kuna saidia kumlinda mtoto kutokana na magonjwa na kum epusha mama kupata aina fulani ya saratani. Baada ya miezi ya kwanza sita, ni vyema kumlisha mtoto vyakula vigumu hadi anapo komaa vya kutosha na kuwacha kunyonya.

Kumlisha mtoto vyakula vigumu

Ili kuelewa vyema kuhusu kumwanzishia mtoto vyakula vigumu, wamama wengi hukoma kuwanyonyesha watoto pekee kwa kuwaanzishia vyakula vilivyo laini pamoja na maziwa ya mama. Kipindi hiki huanza pale ambapo maziwa ya mama sio njia pekee ya kumlisha mtoto. Kulingana na American Academy of Pediatrics, mama anaweza koma kumnyonyesha mtoto anapo fikisha mwaka mmoja lakini anaweza amua kuendeleza akiamua.

Utaratibu wa kumwanzishia mtoto vyakula vigumu

kumlisha mtoto vyakula vigumu

Kutoka miezi 6

Hii ni hatua unapo jaribu vyakula tofauti mbali na kumnyonyesha mtoto wako. Ni vyema kumpa anuwai ya vyakula vigumu ili uone ikiwa wata kubali ama kuvikataa. Sio kusema kuwa ukome kuwapatia vyakula wanapo kataa; ina maana kuwa uendelee hadi watakapo vikubali.

Katika hatua hii, mtoto wako ako tayari kula vyakula vilivyo bondwa na pia matunda na mboga, ila ni vyema kukumbuka kuwa unapaswa kumwanzishia pole pole. Kumbuka haupaswi kuongeza sukari ama chumvi kwenye chakula cha watoto katika umri huu.

Mtoto pia anaweza kunywa maji kutoka kwa kikombe wazi, hata kama kutakuwa na kumwagika kwingi na uta hitajika kusafisha baadaye.

Miezi 6-9

Katika hatua hii, mtoto wako amezoea vyakula vingi na bado unaweza ongezea vyakula zaidi. Mbali na maziwa ya mama, mtoto wako ako tayari kwa vyakula tofauti ukihusisha maziwa ya bururu na mkate hata wali.

Miezi 9-12

Mtoto anaweza kula vyakula vigumu kidogo. Pia unaweza ongeza viwango unavyo mlisha. Katika umri huu, mtoto anaweza kula hadi vijiko 6 vya chakula kila mara. Kumnyonyesha mtoto katika hatua hii bado ni muhimu na unapaswa kumnyonyesha anapo hitaji. Ili kum himiza mtoto kula vyakula, mpe chakula kilicho katwa anacho weza kuchukua na kula bila usaidizi.

Kuna aina mbili za kumwanzishia mtoto chakula

majina ya wavulana

Kutoka kwa mtoto:

Kuna baadhi ya watoto ambao wako tayari kuwacha kunyonya kabla ya mama kuwa tayari kuwa komesha kunyonya. Katika aina hii, mtoto anakosa hamu ya maziwa ya mama. Mara nyingi, huku hufanyika baada ya kuanzishiwa vyakula vigumu na wanapokuwa hai zaidi na kukataa kukaa wanapo nyonyeshwa. Ama wana pendelea kula vitu vingine.

Kutoka kwa mama:

Aina hii, mama ako tayari kukoma kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama. Lakini mtoto bado hayuko tayari. Katika kesi hii, mama anahitajika kuwa na uvumilivu mwingi. Kukosa kumnyonyesha mtoto kwa kasi sio njia bora ya kumwanzishia vyakula vigumu. Inapaswa kuwa utaratibu wa pole pole, kwani kipindi hiki cha mabadiliko ni muhimu kwa mama na mtoto.

Jinsi ya kufanya utaratibu huu uwe rahisi

  • Kumbuka kuwa ni utaratibu unao chukua muda
  • Fupisha wakati wa kumnyonyesha mtoto

Anza kwa kupunguza wakati uwe nusu wakati wa kawaida. Ikiwa kwa kawaida wewe humnyonyesha kwa dakika tano, punguza wakati huo uwe nusu yake na umlishe vyakula vingine.

  • Kukosa kumnyonyesha kama ilivyo kawaida

Ikiwa wewe humnyonyesha mara nne kwa siku, punguza ziwe mara tatu kisha umpe formula ama chakula badala ya maziwa ya mama.

  • Usitarajie akubali mchakato huu ikiwa unafuata aina ya mama kuongoza ama kuanzisha. Ikiwa wana taka kunyonya, unaweza peleka fikira zao pahali pengine kwa kuwapa vidoli wacheze navyo ama aina nyingine ya vyakula.

Kumwanzishia mtoto wako chakula kutakuwa rahisi ukifuata vidokezo tulivyo angazia.

Vyanzo: World Health Organisation

American Academy of Pediatrics

Soma Pia: Je, Ni Vyema Kwa Mama Kumwamsha Mtoto Ili Amlishe?

Written by

Risper Nyakio