Mwanamke Kumnyonyesha Bwana Baada Ya Mtoto: Kitendo Maarufu Uganda

Mwanamke Kumnyonyesha Bwana Baada Ya Mtoto: Kitendo Maarufu Uganda

Katika nchi ya Uganda, wanaume wana amini kuwa maziwa ya mama huwa na nguvu za kimiujiza. Wana kunywa maziwa ya mama na wake wao hawawezi wakataza.

Kitendo cha mwanamke kumnyonyesha bwana baada ya mtoto huenda kikawa ndoto ya watu wengi, ila sio jambo nadra katika nchi ya Uganda. Bwanake Abbo anapenda maziwa ya mama. "Yeye husema anapenda ladha yake, na inamsaidia katika afya yake. Ana hisi vyema baada ya kumaliza," alisema mwanamke wa miaka 20 kutoka Uganda aliye na mtoto wa miezi sita. Abbo alisema kuwa bwanake alianza kuitisha maziwa ya mama, usiku alio fika nyumbani kutoka hospitalini baada ya kujifungua. "Alisema kuwa kungenisaidia na utoaji wa maziwa. Nikahisi ni sawa."

kumnyonyesha bwana baada ya mtoto kumnyonyesha bwana baada ya mtoto

Bwanake Abbo ni mmoja kati ya mamia ya wanaume kutoka Uganda wanao sisitiza kunyonya chuchu za bibi zao. Kitendo hiki pia ni maarufu katika pande za Tanzania na Kenya. Kwa sasa kina husishwa na udhalilishaji wa kijinsia na tabia ya kulazimisha na kuna shaka kuhusu tendo hili na athari zake kwenye lishe ya mtoto.

Dunia ilijua machache sana kuhusu kitendo hiki hadi hivi majuzi. Waziri wa afya wa Uganda, Sarah Opendi, alivunja kimya chake bungeni mwaka wa 2018. Alionya dhidi ya "ukuaji wa tamaduni ya wanaume kuamrisha kunyonya; ambayo ilikuwa tatizo ibuka kwa baadhi ya wamama walio kuwa wana nyonyesha na watoto wao".

Aliendelea kueleza sababu kwa nini wanaume wengi wali sema wanahitaji maziwa hayo, kwa kusema "wanaume ni mojawapo ya tatizo wakati wa kunyonyesha. Mama ana nyonyesha, bado unataka kitu kwenye upande, na kudai kuna yanaweza ponya Ukimwi, saratani na matatizo ya kiume. Ni imani isiyo kweli."

Maoni Ya Watafiti Kuhusu Kitendo Cha Mama Kumnyonyesha Bwana Baada Ya Mtoto

kumnyonyesha bwana baada ya mtoto

Sababu za tendo hili na ishara zinazo tokea, zilizua masomo ya kwanza kupata ujumbe zaidi kuhusu jambo hili. Chuo Kikuu cha Kyambogo huko Kampala na Chuo Kikuu cha Britain huko Kent ndio walio fanya utafiti huu. Utafiti huu pia unasherehekea utegemezi wa Global Challenges Research Fund.

"Ilikuwa misheni ambayo haikuwa fiche," alisema daktari Rowena Merrit. Ni mwana sayansi wa British na uspesheli wake ni afya ya umma, na mtafiti mkuu wa mradi. "Hatukujua iwapo tungepata mtu ambaye angependa kuongea nasi kuhusu jambo hili ama aliye tendekewa. Hatukujua iwapo ilikuwa kweli ama la," alisema.

Somo hili lili angazia zaidi wilaya ya Buikwe, katika sehemu ya kati, ambapo tabia hii ili ripotiwa kuwa maarufu.

Kama somo hilo, watafiti walifanya mahojiano na wana boda boda wanne kwenye wilaya hiyo ya mashinani. Waliwaambia watafiti kuwa "hawakuwai ongea kulihusu" ila walisema inawapatia nishati.

"Ina ni endeleza, nakuja nyumbani kula chamcha na ina saidia kutoa fikira nyingi katikati ya siku ninapo fanya kazi," mmoja alisema.

Pia waliitumia kama mbinu ya kuanza ngono, hata na wachumba wao ambao walikuwa wamejifungua. Mada ingine walisema watafiti: "Unapo nyonyesha, nahisi kana kwamba nachungwa kama mtoto, na ni jambo linalo furahisha. Nahisi kana kwamba mimi ni mtoto wa mfalme."

Utafiti wa hivi majuzi ume ashiria kuwa wanaume mara nyingi hunyonya kabla ya mtoto kulishwa; mara moja kwa siku, baadhi ya wakati mara zaidi, na kwa angalau lisaa limoja kila mara. "Kuna imani kuwa baadhi ya jamii kuwa maziwa ya mama ina nguvu za kukupatia nishati na kukuponya, hata virusi kama vile ukimwi na saratani," alisema daktari Peter Rukundo, mhadhiri mkuu wa Chuo Kikuu cha Kyambogo aliye saidia katika utafiti.

Kumnyonyesha bwana baada ya mtoto: Wanawake hawakuwa na mengi ya kusema katika suala hili

kumnyonyesha bwana baada ya mtoto

Wanawake hawaonekani kuwa na chaguo katika jambo la kuwa nyonyesha mabwana zao baada ya watoto. "Inaonekana kuwa tabia ya kulazimishwa kati ya watu wengi tulio ongea nao," aliongeza Merritt. Walipo ulizwa kitu ambacho kingetendeka iwapo wangesema apana, mwanamke mmoja alijibu: "Naogopa kuwa bwanangu anaweza enda mahali pengine iwapo ningekosa kufanya hivi."

Tabia hii imehusishwa na hatari za kijinsia katika sehemu ya Karamoja upande wa Kaskazini Mashariki Uganda. "Mtaalum mkuu wa lishe alisema kuwa ni jambo la kawaida na kuna aina ya vurugu; kuwa wanaume walipolewa, baadhi yao walienda na vita na vurugu nyingi," alisema Rukundo.

Wataalum wa kiafya, ukihusisha wakunga na wataalum wa lishe, waliwaambia watafiti kuhusu visa ambapo watoto wao walikunywa maziwa ya chupa kwa sababu wanaume wao walitaka kunyonya. Pia kuna visa ambapo wanawake walikuja kwa zihanati walikuja na chuchu zilizo umwa wanaume wao wakinyonya. Jambo hili pia lina athari za watoto kupata maambukizi kutoka kwa mate ya mwanamme.

"Kuna changamoto kuu ya kwenye elimu ya umma kuhusu hatari katika mambo kama haya. Ila changamoto ni kuwa hatuna ushuhuda wa ukuu wa tabia hii. Tuna hitaji kuangazia zaidi," alisema Rukundo.

Pia aliialika serikali na washiraka wa maendeleo kufanya kazi pamoja ili kupunguza hatari hii. "Hatuna ujumbe hasa ama juhudi za kipekee, hata na waziri wa afya akisema kuwa kuna tatizo. Kwa hivyo, kwa njia, ni kama hatutaki kukubali. Iwapo wanabaki wametulia, tatizo hili litatupiliwa mbali," alisema.

Merrit aliongeza kuwa: "Uwoga wangu, ni japo jambo hili linavyo zidi kuendelea, litakuwa kama utamaduni na itikadi za kizazi kijacho. Naona liki lingana na FGM."

The Guardian

Soma pia: Is It Possible to Get Pregnant While You're Breastfeeding?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio