Vidokezo 6 Muhimu Vya Jinsi Ya Kumnyonyesha Mtoto Bila Kumpa Chakula!

Vidokezo 6 Muhimu Vya Jinsi Ya Kumnyonyesha Mtoto Bila Kumpa Chakula!

Kuna manufaa mengi ya kuwa na mtoto chumbani nawe, hasa unapo kuwa hospitalini na nyumbani. Kama vile kuepuka kifo cha ghafla cha mtoto.

Vitendo vya kwanza vya kumtunza mtoto kama mama mpya ni kumnyonyesha mtoto. Kwa wanawake wengi, huku kunamaanisha kunyonyesha peke yake. Hata kama kunyonyesha ni kitendo asili, unaweza kuwa na shaka za kutosheleza mahitaji ya mwanao ya virutubisho. Na ukawa na maswali chungu nzima kuhusu inavyo fanya kazi na jinsi ya kumnyonyesha mtoto bila kumlisha chakula kinginecho.

Vidokezo vya kumnyonyesha mtoto bila kumlisha chakula

faida za kunyonyesha

Kutoka wakati ambapo mtoto anazaliwa, kuna idadi ya vitu ambavyo unaweza fanya kuboresha nafasi za kunyonyesha kufuzu.

  • Baki na mtoto baada ya kuzaliwa

Kubaki na mtoto wako baada ya kujifungua kutahimiza hisia za kuwa pamoja na hisia za homoni zinazo husishwa na kunyonyesha peke yake kufuzu. Katika visa vingi, kuna uwezekano wa kuwa na mtoto wako punde tu baada ya upasuaji wa C-section.

  • Mshike mtoto inavyo faa

Siku za kwanza chache baada ya kujifungua huwa na nafasi nzuri kwako na kwa mtoto wako kujua jinsi ya kumnyonyesha. Chuchu zako bado ni laini kwa siku za kwanza chache baada ya kujifungua. Na kadri maziwa wa mama yanavyo zidi kubadilika kutoka kuwa colostrum hadi kuwa maziwa yaliyo komaa. Na matiti yako yata ongezeka na kujaa. Jaribu na utumie siku za kwanza chache kufahamu unavyo stahili kumshika mtoto.

Kufanya hivi kutakusaidia kuepuka matatizo ambayo yanaweza yakaibuka baadaye.

  • Kuwa mvumilivu

Kunyonyesha ni kitendo ambacho wewe na mtoto wako mnajifunza na kwa baadhi ya wamama na watoto, huenda wakatatizika zaidi kushinda wengine. Sawa na kitu chochote kipya, kinachukua muda na uvumilivu. Kupumzika ni muhimu kwako na mtoto wako. Ukigundua kuwa una kasirika na kukata tamaa unapo nyonyesha, simama kisha uendelee baada ya muda. Ikiwa mtoto wako ana tatizika, na ikiwezekana, uliza mtu awachunge hadi uhisi uko tayari kujaribu tena.

Pia unaweza kamua maziwa ya lishe hiyo na ujaribu kumnyonyesha katika lishe ijayo.

  • Mnyonyeshe mtoto anapo hitaji

kumnyonyesha mtoto bila kumlisha chakula

Unapo anzia kunyonyesha, mtoto wako atanyonya kati ya mara saba hadi kumi na mbili kwa masaa ishirini na manne. Hadi utakapo kuwa na ratiba dhabiti ya kunyonyesha. Kumnyonyesha mtoto vizuri na mara kwa mara kutakusaidia kuwa na maziwa tosha ya mtoto wako.

  • Kunywa maji kwa wingi

Unamnyonyesha mtoto anapo hitaji na ni vyema kuhakikisha kuwa una maji tosha mwilini wakati wote.

  • Mweke mtoto chumbani kimoja nawe

Kuna manufaa mengi ya kuwa na mtoto chumbani nawe, hasa unapo kuwa hospitalini na nyumbani. Kama vile kuepuka kifo cha ghafla cha mtoto. Kufanya hivi pia kuna boresha kunyonyesha. Kuwa na mtoto chumbani kutakusaidia kufahamu mtoto anapokuwa na njaa, anapo choka na anapo hitaji kukumbatiwa. Utajua wakati bora wa kumnyonyesha.

Hakikisha kuwa ana mazingira salama anapo lala usiku na mchana.

Soma Pia: Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Written by

Risper Nyakio