Jinsi Ya Kumpa Bwanako Hamu Ya Kufanya Mapenzi Ili Kuipa Ndoa Yako Ladha

Jinsi Ya Kumpa Bwanako Hamu Ya Kufanya Mapenzi Ili Kuipa Ndoa Yako Ladha

Ngono ina faida nyingi katika ndoa, kwa hivyo unapaswa kuchukua jukumu hili mikononi na kujua jinsi ya kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi. Sio kazi ya bwana kufanya hivi wakati wote. Jambo rahisi kama kumwanzishia huenda likafanya chumba chako cha kulala kibadilike.

kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi

 Sababu kwa nini unapaswa kutia bidii na kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi

Kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kuchukua jukumu la kuongoza kitandani.

I. Huenda ika rudisha ladha ya maisha yenu ya mapenzi

Wanandoa katika ndoa zisizo fanya mapenzi wanaweza rekebisha hali hii iwapo wenzi wote wawili wanatia bidii kurejesha mapenzi yao. Maisha yako ya ngono yana hitaji bidii kutoka kwa wenzi wote wawili ili kufanya ndoa yao iwe ilivyo kuwa hapo awali.

II. Ni njia nzuri ya kuongeza ujasiri wako

Juhudi unazo tia kuanza kufanya mapenzi zitakusaidia kujiamini zaidi. Fikiria kuhusu vitu vizuri vyote ambavyo juhudi hizi zitafanya kwa utu wako unapo mkaribia bwanako kumpa hamu ya kuwa na wakati mzuri.

III. Inaweza kuhamasisha kujaribu vitu vipya katika chumba cha kulala

Ni vigumu kufanya juhudi za kumfikia bwanako na kumhamasisha ili kufanya mapenzi bila kuwa na fikira kuhusu mitindo tofauti ambayo mnaweza jaribu. Endelea na ujaribu mitindo yote ambayo umeishi kutamani.

Iv. Inamhakikishia mwenzi wako kuwa unamthamini

Sio wanawake tu wanaotaka kuhisi kuwa wanapendwa. Bwanako angependa kuonyeshwa kuwa anapendwa na kujaribu juhudi zote kufanya mambo iwe sawa katika chumba cha kulala ni njia kuu.

v. Kuanzisha kufanya mapenzi na bwanako kutasaidia ndoa yako kuwa na utangamano zaidi

Juhudi za kuanzisha mapenzi katika ndoa huenda zika puuzwa. Ngono ina boresha uhusiano wenu na kuwafanya mwe na utangamano zaidi.

kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi

Jinsi ya kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi

Fikiria kuhusu ngono, kwa sana

Lazima uiweke akili yako katika hamu hiyo ili kukusaidia kufanya hivi kwa mafanikio. Kufikiria kuhusu ngono kutakusaidia kupata hamu. Unaweza tumia wakati huu kupanga fursa mwafaka ya kufanya kilicho akilini mwako.

Lazima utake kufanya hivi

Hamu itakusaidia sana. Bwanako anapo ona kuwa una mtamani sana, bila shaka ataitikia mwito wako.

 Kuanzisha ngono kuna maana ya kuanzisha ngono!

Haunzishi ngono tu kwa kumgeukia uso na kumtazama. Hatajua kuwa ungependa kufanya mapenzi na yeye kwa sababu ulienda kulala punde tu baada ya chajio alipo taka kutazama mpira. Kwa hivyo, ulinunua mavazi ya kumtamanisha ya usiku huu, ila, hakuona ulivyo pendeza, huenda akageuka na kuanza kung'orota iwapo hautafanya chochote.

Lengo ni kuwa wazi kuhusu matakwa yako.

Jaribu kuto ona haya

Hili huenda likawa gumu kidogo, hasa iwapo hapo awali uliamini kuwa mwanamme anapaswa kuwa ndiye anaye kufikia wa kwanza ili kufanya ngono. Unapo anza kuona haya, kumbuka kuwa mwanamme huyu ni bwanako, na sio mara ya kwanza ama ya mwisho kufanya mapenzi naye. Tulia, usiwe na shaka!

Bwanako hata kataa mwito wako wa kufanya mapenzi, fursa kubwa ni kuwa atakuwa na hamu kubwa pia.

Anza kumwonyesha kuwa una hamu yake kabla ya siku kuu

Kwa sasa kwani una hamu, unaweza mfanya bwanako aanze kutamani kufanya mapenzi nawe pia. Njia nzuri zaidi ya kufanya hivi ni kumwambia jinsi unavyo mtaka siku yote. Mtumie jumbe za kimapenzi kumjulisha kuwa una mipango ya kufanya mapenzi naye. Mkumbushe vitu anavyopenda ufanye na umjulishe jinsi huwezi ngoja kufanya vitu hivyo naye.

Jinsi Ya Kumpa Bwanako Hamu Ya Kufanya Mapenzi Ili Kuipa Ndoa Yako Ladha

Kuwa na ujasiri

Uwoga wako umeisha, mshike bwanako na umpe busu ambalo umekuwa ukifikiria siku yote. Mwambie jinsi unavyo mtamani. Kujua jinsi ya kuanzisha ngono na bwanako kutakuwa na mafanikio ukitumia maarifa yako vyema.

Kuwa na ujasiri unapo hisi hamu ya kufanya mapenzi. Unahisi kumshika bwanako na kumtoa nguo mara tu mnapofika chumba cha kulala? Fanya hivyo! Usipoteze muda kufikiria sana. Huenda ukakosa hamu.

Usiwe na uwoga kumgusa

Kumwambia kuwa unapendeza na uko tayari ni jambo moja, kumwonyesha ni mada tofauti. Unajua wanavyo sema kuwa matendo huongea kwa nguvu zaidi kuliko maneno?

Mfikie kwanza. Mpe busu shingoni asipo tarajia. Mpe masi ya mgongo (ni kweli, wanaume wanapenda hivyo pia!) na kisha ufuatilie na masi ya kimapenzi itayo isha na nyote mkiwa na kipindi cha kusisimua.

Hitimisho

Mapenzi ni kitu cha kupendeza, ila huenda yakawa kama kazi iwapo bwanako ndiye atakaye kuwa akikufikia wakati wote. Vidokezo hivi vya jinsi ya kumpa bwanako hamu ya kufanya mapenzi vitakusaidia kuwa na ujasiri zaidi na kuongoza.

Kumbukumbu: VeryWellMind.Com

Soma pia: Sex drive foods: 7 Libido-enhancing foods to improve your performance

Written by

Risper Nyakio