Mapenzi yanapo noga, ni vigumu kufikiria kuhusu kitakacho tendeka wakati wewe na mchumba wako mtakapo achana. Mapenzi kweli ni kitu kizuri na sote tuna stahili kupata nafasi ya kupenda na kupendwa. Ila pale ambapo mambo huenda mrama na kuwafanya wapenzi kutengana. Hiki huwa kipindi cha kuhuzunisha na chenye maumivu mengi kwa wachumba walo kuwa katika mapenzi pamoja. Na kutengana kunapo fanyika, hakuna jambo unalo weza kufanya katika hatua hii. Ni vyema kufahamu jinsi ya kukumbana na kuwachwa na kumsahau mpenzi wako wa awali.
Vidokezo vya jinsi ya kumsahau mpenzi wako wa awali

Ni muhimu kwako kujua jinsi ya kukabiliana na kuachwa katika uhusiano, jinsi ya kukabiliana na hili na kuendelea na maisha yako bila kuchukua muda mrefu sana ukiomboleza.
- Usisisitize kupatana mara ya mwisho
Kosa moja maarufu sana kwa wachumba walio tengana ni kusisisitiza kupatana ili mzungumze kuhusu kilicho sababisha kutengana kwenu. Hili huwa jambo mbaya na kamwe halishauriwi.
Kufanya hivi kutakufanya uendelee kushikilia hisia za hapo awali, za nyakati nzuri na uchungu ulio pitia. Na kurefusha wakati wako wa kupona baada ya kutengana.
2. Kulia sio hatia
Usiwasikize watu wanao sema kuwa, haupaswi kulia kwa sababu wewe ni mtu mzima. Watu wazima pia wana hisia na huumia wanapo tendwa. Kulia ni mojawapo ya njia ya kukubali kilicho tendeka na hatua ya kwanza ya safari yako ya uponaji.
3. Rudia maisha yako asili

Badala ya kujaribu kurudiana na mchumba wako wa hapo awali, wakati ambapo ashafunga kurasa yako, tia juhudi kurejesha maisha yako mahali yalipo kuwa.
Fanya vitendo vinavyo kufurahisha kama vile kusoma kitabu, kujumuika na marafiki zako wanapo safiri, kujiunga na darasa la mazoezi na kadhalika.
4. Kata mawasiliano yao
Unapo wasiliana na mchumba wako wa hapo awali, nafasi kubwa ni kuwa hisia za hapo awali zita anza kurudi. Kwa hivyo, hakikisha kuwa hauzungumzi nao tena. Kupitia kwa njia yoyote ile ambayo mlikuwa mna wasiliana hapo awali.
5. Jitahini
Huenda ukawa unamchukia sana mchumba wako wa hapo awali katika kipindi hiki. Lakini kwa kusema ukweli, baadhi ya wakati, huenda ikawa sisi ndiyo tuliokosea. Je, kuna kitu ulicho kosea ambacho ungefanya vitofauti? Kuna mambo uliyo soma kutoka kwa uhusiano huo? Katika uhusiano wako mpya, ni yapi ungependa kufanya kwa njia tofauti?
Ni vyema kujiuliza maswali haya, kwani baada ya muda utaingia kwa uhusiano mpya na itakuwa vyema kufanya uamuzi bora.
Soma Pia: Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako