Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Vidokezo 4 Vya Kuboresha Usingizi Wa Mtoto Na Mama

3masomo ya dakika
Vidokezo 4 Vya Kuboresha Usingizi Wa Mtoto Na MamaVidokezo 4 Vya Kuboresha Usingizi Wa Mtoto Na Mama

Katika umri wa miezi mitatu, watoto huanza kutoa homoni ya melatonin inayo fanya mzunguko wao wa kulala kuwa wa kawaida.

Maria alifahamu kuwa ako taabani usiku wa pili baada ya kutoka hospitalini na kifungua mimba chake cha siku moja. Mtoto wake wa kiume alilia usiku mzima, Maria aliwaelezea marafikia zake walio kuja kumpakata mwanawe baada ya kutoka hospitalini. Nilikuwa nimechoka sana baada ya kushuhudia uchungu wa uzazi kwa siku tatu kabla ya mtoto kufika. Na alipo fika na kudhania kuwa ningepata angalau wakati wa kutuliza mwili na kulala vyema, alianza kulia usiku mzima na kufanya mambo yawe magumu zaidi. Sikujua cha kufanya wala mbinu za kumsaidia mtoto kulala vyema.

Baada ya miezi michache, hali haikuwa imebadilika. Alikuwa ana lala kidogo na nilipo fikiria kuwa mambo yame badilika, alirudi kwa uraibu wa kuamka baada ya kila lisaa usiku, Maria alielezea.

Ni vigumu kwa wazazi hasa wa mara ya kwanza kujua jinsi mtindo wa kulala wa watoto wao utakavyo kuwa. Kitu cha kipekee wanacho kifahamu ni kuwa watakaa jicho wazi usiku kwa miezi ya kwanza michache. Kulingana na wataalum wa watoto, miezi ya kwanza baada ya kuzaliwa kwa mtoto huwa migumu kwa mtoto na wazazi wake. Mtoto asipo lala, itakuwa vigumu kwa mzazi kulala ama kupata wakati wa kupumzika. Njaa ama shibe ina dhibiti jinsi mtoto atakavyo lala na kuamka. Matatizo haya ya kuamka usiku mzima huanza kupungua mtoto anapo fikisha miezi mitatu. Katika umri huu, watoto huanza kutoa homoni ya melatonin inayo fanya mzunguko wao wa kulala kuwa wa kawaida.

Jinsi ya kumsaidia mtoto kulala peke yake

kumsaidia mtoto kulala

Watoto huwa tofauti na masaa wanayo lala hutofautiana pia. Watoto walio zaliwa wanaweza lala kati ya masaa 10- hadi 18 kwa siku. Kati ya masaa haya, mtoto atalala kwa masaa 5 kabla ya kuamka. Anapo fikisha miezi minne (4) hadi mwaka mmoja, masaa anayo lala kwa siku yana punguka hadi masaa 9-12. Wakati mtoto anapo lala, mama anashauriwa kulala pia ama kupumzika. Katika umri wa miezi minne, epuka kumchukua mtoto kwa kasi anapo lia. Mpe angalau dakika chache kudhibitisha iwapo alikuwa analia ama ana ota. Akiendelea kulia, mtulize, akiendelea kulala, mwache hadi pale ambapo ataamka.

Kutomchukua punde tu anapo lia kutamsaidia kujituliza hadi alale tena.

Siri za usingizi wa mtoto

kumsaidia mtoto kulala

  • Mfunikie mtoto wako kwa blanketi wenye joto anapo lala ili alale vizuri. Kumbuka kuhakikisha kuwa hauja mvisha mavazi zaidi. Kufanya hivi kutamtatiza kulala ama kumfanya aamke kwa sababu ya joto jingi.
  • Usiweke mito ama blanketi zaidi kwenye kitanda cha mtoto wako, kufanya hivi kuna hatarisha maisha yake.
  • Epuka kulala na mtoto wako kitandani kimoja anapo kuwa mchanga.
  • Epuka kulala unapo mnyonyesha mtoto wako.

Vyanzo: WebMD, NHS

Soma Pia: Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Ages & Stages
  • /
  • Vidokezo 4 Vya Kuboresha Usingizi Wa Mtoto Na Mama
Gawa:
  • Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

    Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

  • Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

    Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

  • Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

    Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

  • Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

    Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

  • Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

    Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu

  • Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

    Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

  • Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

    Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

  • Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

    Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it