Mama anapo toka hospitalini baada ya kujifungua, atakuwa anahisi uchovu mwingi. Hana nguvu na nishati ya kufanya kazi zake kama alivyo kuwa hapo mbeleni. Mchakato wa kujifungua huhitaji nishati nyingi, yote ambayo anaitumia katika chumba cha kujifungua. Ni vyema kwa mama kupata usaidizi kufanya kazi za nyumbani katika kipindi hiki. Pamoja na kumsaidia kumtunza mtoto mchanga.
Jinsi ya kumtunza mtoto mchanga

Mtoto aliye zaliwa ana hitaji kutunzwa kwa makini. Tazama baadhi ya mambo yaliyo muhimu zaidi kufanya.
- Kunawa mikono vizuri kabla ya kumshika mtoto
Mfumo wa kinga katika watoto haujakua vizuri wanapo zaliwa. Ni rahisi kwao kuugua maambukizi wanapo shikwa na mikono michafu. Hakikisha wageni wako wananawa mikono kabla ya kumshika.
Mtoto bado ako katika kipindi nyeti, hapaswi kutingishwa kwa sababu yoyote ile. Kumtingisha kuna mweka katika hatari ya kuvuja damu kwenye ubongo na huenda kukasababisha kifo. Mshike kwa upole.
- Egemeza kichwa na shingo ya mtoto
Mshike mtoto na uhakikishe kuwa mkono wako una mwegemeza shingo na kichwa. Unapo msimamisha, mshikilie kwenye shingo.
- Dhibiti nambari ya wageni unao pata kwa siku
Siku baada ya mama kurudi nyumbani na mtoto huwa wakati wake kuwa na wakati wa kutangamana na mtoto. Kuwa na wageni wengi kunapunguza wakati wao wa kuwa pamoja.

Mtoto mchanga hulishwa kwa mahitaji. Anapo onekana kuwa ana njaa, hakikisha kuwa unamlisha. Huenda aka ashiria kwa kulia, kutoa sauti kana kwamba ana nyonya ama kwa kuingiza mikono kwenye mdomo.
Watoto wachanga wana stahili kulishwa baada ya kila masaa mawili ama matatu. Mnyonyeshe kwa angalau dakika 15 kwa kila pande kabla ya kubadilisha na kumnyonyesha chuchu nyingine. Kwa watoto wanao chukua formula, huenda wakachukua angalau mili lita 90 kila mara wanapo lishwa.
Mtoto anapo lala zaidi, na kupitisha wakati anao paswa kunyonya, mama anaweza kumwamsha ili amlishe. Unapo gundua kuwa kuna jambo lisilo la kawaida ama kuwa na shaka zozote zile kuhusu kumlisha mtoto. Wasiliana na daktari wake bila kukawia.
Jinsi ya kufahamu ikiwa mtoto wako ana nyonya vya kutosha
Kwa mama anaye mpa mtoto wake formula, ni rahisi kufahamu ikiwa ana kula vya kutosha na kiwango anacho pata. Ila kwa mama anaye nyonyesha, ni vigumu kidogo. Lakini mama anaweza jua kwa kuangalia mara ambazo anam-badilisha nepi zilizo jaa, anavyo lala usiku na jinsi anavyo ongeza uzani wa mwili.
Mama anastahili kuhakikisha kuwa kabla kubadilisha chuchu anapo mnyonyesha mtoto, hahisi kana kwamba imejaa bado.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Faida 5 Za Unyonyeshaji Wa Kipekee Kwa Mtoto Mchanga!