Je, Mwanao Ana Mchumba? Vidokezo Hivi Vitakusaidia Kumwongoza Katika Uhusiano Wake

Je, Mwanao Ana Mchumba? Vidokezo Hivi Vitakusaidia Kumwongoza Katika Uhusiano Wake

Kwa wazazi wengi, kulea watoto hasa katika miaka yao ya wastani huwa sehemu ya kushtua katika ulezi. Nidhamu huwa ngumu kuangazia. Unashangaa wakati wa kuweka masharti na wakati wa kuwapatia uhuru, wakati wa kuwawacha wafanye watakacho na wakati wa kuwa imara katika msimamo wako. Wazazi wengi wa watoto hawa huwa na uwoga kuhusu wakati ambao ni sawa kwa watoto wao kuanza kuwa na uhusiano. Wakati ambapo ni hatua kubwa katika kukomaa kwako, ni vyema kuwa makini sana. Huenda akawa na uwezo wa kuwa na mchumba lakini angali mchanga na unahitaji kuwa makini sana. Ana hitaji kuongozwa, kwa sababu hata na watu wakubwa, uhusiano si kitu rahisi. Kama mzazi, unapaswa umwongoze mtoto wako kuhusu kuwa na uhusiano na mchumba hatua baada ya nyingine. Makala haya yana ushauri, hatua baada ya nyingine jinsi ya kumwongoza mwanao kuhusu uhusiano.

Jinsi Ya Kumwongoza Mwanao Kuhusu Uhusiano Na Kuwa na Mchumba

  1. Zungumza                                                                                                                                                                      Kila kitu kuhusu kulea watu wachanga ni cha kuchanganya hasa mazungumzo. Lakini ni muhimu na kila kitu kina egemea kwa mazungumzo hayo. Eleza mwanao uhusiano mwema ni nini. Huenda ukafikiria kuwa mwanao tayari anafahamu kuwa na uhusiano ni nini, huenda wasijue. Maarifa yao mengi yana chungwa kutoka kwa mtandao na yana paswa kuwa ya kuburudisha sio yaliyo kweli. Mtoto wako anahitaji kuelewa maana ya kuwa kwenye uhusiano wenye mapenzi, heshima na kusaidiana. Mfumo wa mazungumzo kamwe haupaswi kufungwa kati yako na mtoto wako. Wanapaswa kuhisi kuwa wanaweza ongea nawe kuhusu chochote wakati wowote ule.

vijana wa kizazi kipya

  1. Kuwa mfano mzuri wa kuigwaNyingi kuhusu ulezi ni kuwa mfano mwema, na hata katika uhusiano. Mfano wa kwanza wa mapenzi na kuegemezana katika uhusiano unapaswa kuwa kutoka kwako na mwenzi wako. Ni vigumu kufunza mtoto wako kupenda na kuwa heshimu wengine bila ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa katika mapenzi na heshima kwa wengine.
  2. Mfunze umuhimu wa kuanza polepoleJaribu kufanya yote uwezayo kumkanya kuhusu kuanza kujuana na mtu polepole hadi afike miaka 18. Kuanza kuwa na uhusiano mapema na mara kwa mara ni mojawapo ya sababu kuu za kumuweka katika hatari ya kujihusisha katika vitendo vya kingono. Mhimize mwanao kungoja kadri awezavyo.
  3. Mfunze mwanao awe na uhusiano mzuriHakikisha kuwa mwanao anaepuka picha za watu walio uchi, vipindi vya televisheni vinavyo kuwa na ngono, video na filamu anapokuwa akichumbiwa. Pia, hakikisha kuwa una zungumza naye kuhusu jumbe salama za kupitisha kwa wengine kwa mtandao ama hata kwa simu. Wafunze kufahamu lugha isiyo faa na kukataa mwito kama, "Iwapo una nipenda, utanifanyia hivi," na mengineyo. Pia wafunze na uwaonye dhidi ya kutumia lugha hiyo kwa watu wengine.
    guide your teen on dating
  4. Mpe msaada wakoWacha mtoto wako ajue kuwa utampatia msaada wako katika utaratibu wa kuwa na mchumba. Mwambie kuwa unaweza mpeleka ama kumchukua ama hata kumsikiza anapo hitaji mtu wa kuongea naye. Ama hata kwenda naye wanapo enda kula chamcha ili kujua rafiki yao zaidi. Kwa njia yoyote ile unayo kusudia kumsaidia mtoto wako naye, ni vyema kwao kujua kuwa uko nao katika safari hiyo yote.
  5. Wakati wote wapatane na kusalimianaOmba kupatana na kujua mtu aliye na mtoto wako kila mara kabla ya kwenda nje. Alika rafiki yake aje aongee nawe kuhusu mipango yake, wataenda wapi, saa za amri ya kutoka nje, na masharti ya kuendesha gari. Huku kutawafanya wajue kuwa unawaangalia wakati wote.
  6. Kuwa na mazungumzo kuhusu ngonoWakati ambapo huenda ukawa na wazo la kuepuka mazungumzo haya, kuna faida kwa kila mmoja wenu kuwa na mazungumzo haya na watoto wako. Jiulize iwapo ungependa mwanao asikie habari hizi kutoka kwa mtu mwingine. Tuna shauri kugeuza mada hii iwe mjadala badala ya mafunzo tu. Kuwa na uhakika wa kusikiza maoni ya mtoto wako na umjuze maoni yako pia. Jadili faida na athari hasi za ngono bila fiche. Ongea kuhusu majukumu na mambo yanayo faa kuangaziwa na pia imani kuhusu dini yenu.
  7. Mshauri apatane na marafiki wapya akiwa kwa vikundiMhimize mwanao kuwa katika vikundi. Ama, ongea na mwanao kuhusu kupanga kupatana na anaye kuwa na uhusiano naye wakiwa kwa kikundi. Halitakuwa jambo la kufurahisha tu, mbali litasaidia na watahisi wako salama zaidi, iwapo atajipata kwa kisa ambacho hakimpendezi. Msaidie na um-egemeze iwapo anakumbana na matatizo yoyote ya kuwa na mchumba, uhusiano na hata jinsia yake. Mbali na ushauri wako, kuna kumbukumbu nyingi kwenye mtandao ambazo zinaweza kusaidia kujua jinsi ya kuanza. Kumfunza mtoto wako maana ya kuwa kwenye uhusiano wenye afya ni muhimu sana kuwacha ujumbe kuwa asipuuze mambo na jambo ambalo huenda lita yaokoa maisha yake siku moja.

 

Kumbukumbu:

Good Therapy

Today Show

Soma pia: Sababu 4 Kwa Nini Wazazi Wa Afrika Wanapenda Kutawala

 

Written by

Risper Nyakio