Jukumu La Vyakula Vya Kundi La Wanga Ni Nini Mwilini?

Jukumu La Vyakula Vya Kundi La Wanga Ni Nini Mwilini?

Jukumu kuu la vyakula katika kundi hili ni kuupa mwili nguvu. Mfano wa vyakula vya wanga ni kama vile, nafaka zisizo kombolewa.

Chakula ni muhimu sana ili kudumisha uhai na siha yako. Mwili wako unahitaji virutubisho muhimu ili kutimiza utendaji kazi wake. Vyote vinavyo patikana kwa aina tofauti ya vyakula. Virutubisho muhimu mwilini ni kama vile protini, kundi la vyakula vya wanga, vitamini na madini. Zote ambazo zina boresha siha yako.

Baada ya kukila chakula, kina meng'enywa tumboni na kupasuliwa kuwa sehemu asilia ambazo ni rahisi kuchakata na kutumika mwilini. Chakula kina vyanzo viwili vikuu, wanyama ama mimea.

Lishe bora

kundi la vyakula vya wanga

Sahani yako inapaswa kuwa na vyakula vya aina gani ili kuidhibitisha kuwa na virutubisho vyote? Chakula kinapaswa kuwa na mahitaji na virutubisho vyote vinavyo hitajika mwilini. Kukosa aina fulani ya virutubisho huenda kukasababisha magonjwa ya mwili ama utapiamlo. Hasa kwa watoto wadogo. Lishe bora ni muhimu sana katika ukuaji wa watoto.

Virutubisho vina saidia nyanja tofauti za mwili. Ubora wa afya ya binadamu una athiriwa na aina ya chakula anacho kila. Unapo kosa kula kwa muda mrefu, hali yako ya afya ina dhoofika, pia, kula aina moja ya chakula ita athiri afya yako kwa njia hasi. Unapokula kundi la vyakula vya wanga kwa wingi, huenda ukaongeza uzito mwingi wa mwili.

Kundi la vyakula vya wanga

kundi la vyakula vya wanga

Jukumu kuu la vyakula katika kundi hili ni kuupa mwili nguvu. Mfano wa vyakula vya wanga ni kama vile, nafaka zisizo kombolewa, kama ngano, mchele, mahindi, mtama, uwele. Mihogo, viazi vikuu, viazi vitamu, ndizi, viazi mviringo, magimbi na viazi vikuu ni aina ya wanga.

Mikate, sima, wali, vibanzi, na keki. Aina ya wanga iliyo kwenye sahani yako ni muhimu zaidi kuliko kiwango chake. Inapofika kwa wanga, unashauriwa kuhakikisha kuwa unakula kiwango kidogo. Sahani yako inapaswa kuwa na chanzo cha wanga, protini, madini na vitamini. Kwa mfano, kula sima kwa kitoweo cha nyama, mboga za kijani kama vile mchicha na tunda kama chungwa ama ndizi.

Sahani yako itakuwa na virutubisho vyote muhimu vinavyo hitajika mwilini.

Soma Pia: Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

Written by

Risper Nyakio