Kunguruma kwa tumbo kwa mtoto mchanga, kusokotwa na tumbo kwa watoto ama chango ni maneno yanayotumika kueleza hali ya Colic iliyo maarufu kwa watoto wachanga. Colic ni maumivu makali yanayowapata watoto na kuwafanya walie kwa sana kwa muda kama masaa matatu bila kunyamaza.
Mara nyingi hali hii huanza watoto wanapofikisha wiki mbili baada ya kuzaliwa na kuzidi hadi wanapokuwa kati ya miezi mitatu hadi minne. Sio watoto wote wanaopata chango, na wengine huzidiwa na hali hii hadi wanapofikisha miezi sita ya umri.
Vyanzo vya kunguruma kwa tumbo kwa mtoto mchanga

Mtoto anapokunywa maziwa ya kopo ama formula, maziwa haya yana lactose inayowaletea mzio na kusababisha kunguruma kwa tumbo.
Vyakula vya mama huchangia pakubwa katika mtoto kusokotwa na tumbo. Ulaji wa vitu kama ndizi, viazi, vibanzi, kahawa na soda huwa na gesi nyingi.
Kukosa ratiba ya kumlisha mtoto na kumnyonyesha kila anapolia sio sawa. Mtoto mchanga anastahili kunyonyeshwa baada ya kila masaa mawili. Kutozingatia wakati huu wa kunyonyesha humfanya mtoto kuvimbiwa na kumpa gesi.
Kuna namna ya kumshika mtoto unapomnyonyesha. Kumshika vibaya kunamfanya mtoto kupata hewa tumboni.
Kulia kwa sana ama kunyonya kwa kasi kunaweza kumfanya mtoto kumeza hewa inayomwumiza tumbo.
Dalili za chango kwa mtoto mchanga

- Mtoto kulia kwa muda mrefu isivyo kawaida
- Uso kugeuka rangi na kuwa mwekundu
- Mtoto kushtuka mara kwa mara
- Mtoto kunyamba mara kwa mara
Jinsi ya kupunguza kusokotwa na tumbo kwa mtoto mchanga
- Mama anapaswa kumtoa mtoto gesi baada ya kumnyonyesha. Anaweza kumpakata kisha kumkanda mgongo, kumlaza kati kati ya miguu kisha kumkanda ama kumshinikiza mgongo kwa upole
- Mama anapaswa kuwacha kula vyakula vilivyo na gesi nyingi katika kipindi cha miezi minne baaada ya kujifungua
- Mama anastahili kumshika mtoto ipasavyo anapomnyonyesha, ili kupunguza uwezekano wa mtoto kumeza hewa na kuhakikisha kuwa ako katika mazingara bora anaponyonyesha
- Kumtoa mtoto hewa tumboni kwa kumkanda kutumia mafuta ya olive au nazi. Mkande kwenye mgongo na tumbo, kisha umlaze chali na umfanyie kana kwamba anaendesha baiskeli
- Kuzingatia ratiba maalum ya kumnyonyesha mtoto mbali na kumnyonyesha kila anapolia ama kuamka
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Je, Ungependa Usaidizi Wa Kupanga Ratiba Ya Lishe Ya Wiki Moja?