Kunyonyesha kwa muda mrefu kuna manufaa mengi kwa mama na mtoto wake. Mama anastahili kunyonyesha kwa muda upi ili mwanawe anufaike na manufaa haya? Je, kunyonyesha kwa muda mrefu zaidi kuna hatari kwa mtoto?
Shirika la Afya Duniani linawashauri wanawake kunyonyesha kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza bila kumlisha mtoto kitu chingine. Kisha baada ya hapo, kumwanzishia mtoto chakula kigumu na bado kuendelea kumnyonyesha. Mtoto anastahili kunyonyeshwa kwa mwaka wote wa kwanza. Hata hivyo, kufuatia sababu tofauti, sio wanawake wote wanaoweza kuwanyonyesha watoto wao kwa mwaka wa kwanza wote. Kumnyonyesha mtoto kwa muda mfupi na mrefu kuna manufaa gani?
Manufaa ya kunyonyesha ni yapi?

Wiki za kwanza
Wataalum wanashauri kuwa watoto wawe karibu na mama zao na kunyonyeshwa kati ya lisaa la kwanza baada ya kujifungua. Kugasana ngozi na mtoto kunasaidia kuboresha uhusiano na mtoto na kuhimiza utoaji wa maziwa. Maziwa ya kwanza yanayojulikana kama colostrum huwa na virutubisho muhimu na kusaidia kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi.
Mwezi wa kwanza
Kingamwili kwenye maziwa ya mtoto zinasaidia kumlinda dhidi ya maambukizi ya masikio, kifua, kuendesha na kumpa afya bora.
Mama anatoa homoni za kuhisi vizuri anapo na baada ya kunyonyesha na kumsaidia kuwa karibu zaidi na mwanawe.
Miezi minne
Maziwa ya mama katika wakati huu yanasaidia kukuza mfumo wa kuchakata chakula. Kumlinda mtoto dhidi ya mizio ya chakula na kukua vyema.
Mama anakata kilo kwa kasi anapomnyonyesha mtoto bila kumlisha kitu kingine.
Miezi sita
Maziwa ya mama yana virutubisho kama vitamini A, na zinginezo muhimu katika ukuaji wa mtoto. Yanamlinda dhidi ya magonjwa na maambukizi. Hata baada ya kuanzishiwa chakula, ni muhimu kuzidi kumlisha chakula kigumu.
Miezi tisa

Katika kipindi hiki, mtoto hunyonyeshwa anapotaka, tofauti na kabla ya miezi minne ambapo alinyonyeshwa katika wakati fulani. Katika miezi tisa, mtoto hunyonyeshwa kabla ya kulishwa chakula. Mama hushuhudia punguko la idadi ya maziwa anayotoa.
Mwaka mmoja
Kumnyonyesha mtoto hadi mwaka mmoja kunamsaidia kuwa na kinga ya mwili ya juu. Pia, misuli yake ya mdomo itakuwa na nguvu tosha.
Kuna baadhi ya wanawake wanaoamua kuwanyonyesha watoto zaidi ya mwaka mmoja wengine wakiwakomesha watoto wao kunyonya.
Kuna hatari za kunyonyesha kwa muda mrefu?
Kulingana na pande ya dunia unakoishi, wanawake huwanyonyesha watoto kati ya miezi sita hadi miaka minne. Hakuna hatari zilizo ripotiwa za kunyonyesha watoto kwa kipindi kirefu. Hakuna wakati haswaa wa kuwaachisha watoto maziwa ya mama. Ni uamuzi wa mama kulingana na afya ya mwanawe.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Sita Na Kinacho Tendeka Katika Hatua Hii