Je, Kunyonyesha Mtoto Kuna Athiri Mwundo Na Saizi Ya Matiti?

Je, Kunyonyesha Mtoto Kuna Athiri Mwundo Na Saizi Ya Matiti?

Will breastfeeding affect the shape and size of my breast?

Umaarifa wa hivi sasa una onyesha kuwa kumnyonyesha mtoto ni mojawapo ya njia bora kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho ambavyo anahitaji. Hasa wakati muhimu wa miezi 6 ya kwanza ya maisha yake. Wanawake wengi wata epuka kunyonyesha kwa sababu wana fikira kwamba kunyonyesha kutakuwa na athari hasi kwa mwili wao – kuwa matiti yao itashuka ama kupoteza shepu wanapo nyonyesha. Ila, kunyonyesha mtoto kuna athiri mwundo na saizi ya matiti?

 Mama wanao nyonyesha furahikieni! Sayansi yasema apana.

Ni imani ya kale kuwa kunyonyesha mtoto kuna athiri mwundo na saizi ya matiti – mabadiliko ambayo wamama wanao nyonyesha hushuhudia ni kufuatia ujauzito na wala sio kunyonyesha.

Wakati  wa ujauzito, mwili wako, ikiwemo matiti, yataanza kubadilika ili kutayarisha kumpokea mtoto mdogo. Na viwango vilivyo ongezeka vya estrogen na progesterone, huenda ukagundua kuwa unaweza nunua sindiria za saizi kubwa. Baadhi ya mabadiliko haya huenda yakafanyika mapema sana kama punde tu unapo jifungua! Matiti yako yataanza kuwa makubwa kutayarisha mwili kunyonyesha. Chuchu zako na areola huenda pia zikaanza kuwa nyeusi.

Athari za kunyonyesha kwa matiti.

Utafiti wa mwaka wa 2008 unaonyesha kwamba kunyonyesha hakukuwa sababu binafsi ya ptosis ya matima, inayo julikana kwa sana kama kusag kwa matiti.

Sababu zinazo athiri iwapo matiti ya mama yata sag baada ya kujifungua yalidhibitika kama wingi wa umri, unene zaidi, kupata mimba mara nyingi, saizi kubwa ya sindiria unazo valia kabla ya ujauzito na kuvuta sigara.

Matiti yako yametengenezwa na tishu za ufuta na tishu unganishi zinazo julikana kama Cooper’s ligaments. Japo matiti yako yanavyo zidi kuongezeka saizi wakati wa ujauzito na baada ya kumaliza safari yako. Tishu unganishi itanyooka ili kukidhi mabadiliko haya.

Unapo wacha kunyonyesha, matiti yako yanapaswa kuanza kurudi yalivyo kuwa hapo kabla ya ujauzito wako. Huenda kukawa na alama za kunyooka zilizo baki kama ushuhuda wa ujauzito. Ila, kwa kijumla, hakuna haja ya kuendea hiari zozote za kimatibabu.

Nini ninacho weza kufanya kuepuka kusag kwa matiti?

Zingatia afya, kula vyema na uwe makini na uzito wa mwili

Kufuatia matokeo ya utafiti huu, ni muhimu kwa wamama kuzingatia unene wa mwili ulio wa afya kabla ya kuwa mama. Hali yako ya afya kabla ya ujauzito huenda ukaathiri jinsi utavyo pona baadaye.

Kuna baadhi ya wataalum wanao himiza kula pomegranate ili kufanya matiti yako yawe imara ama firm.

Kunywa maji mengi

breastfeeding affect shape size breasts

Kunywa maji mengi

Bila shaka! Maji ni uhai wa maisha na huenda yakawa na athari chanya katika kufanya matiti yako yawe imara zaidi. Wakati ambapo hauna maji tosha mwilini, huenda hali hii ikafanya ngozi iliyo juu ya matiti yakae kana kwamba imekuwa ndogo na kufanya matiti yazeeke mapema. Jambo hili likiendelea kwa muda, litafanya matiti yako yakose kuwa imara.

Koma kuvuta sigara

stop-smoking

Uvutaji sigara unaongeza nafasi za matiti yako kutokuwa imara!

Ni muhimu sana ukome kuvuta sigara. Uvutaji huu wa sigara hauongezi nafasi za matiti yako kuwacha kuwa imara tu mbali kunamhatarisha mtoto wako kupata SIDs kwa urahisi. Iwapo wazazi wote wawili wanavuta sigara, nafasi za mtoto kupata SIDs zinaongezeka kwa mara 3 unusu zaidi ya ilivyo iwapo wazazi wote wawili hawavuti sigara.

Valia sindiria zinazo kutosha vyema

breastfeeding affect shape size breasts

Hakikisha unavalia sindiria inayo kutoshea vyema!

Unaweza hakikisha kuwa unayasitiri matiti yako kwa kuvalia sindiria inayo kutosha vyema. Kuvalia sindiria inayokutoshea vyema kunaweza kusaidia kuhakikisha matiti yako yako imara na kuhakikisha kuwa yamesitiriwa na pia mgongo wako umeegezwa vyema.

Unahitaji msaada? Usitie shaka!

Una shaka kuwa kunyonyesha mtoto huenda kuka athiri saizi na muundo wa matiti yako? Tafadhali wasiliana na mtaalum wa kumlisha/kumnyonyesha mtoto, ambaye atakupatia ushauri wa kipekee na hali ya mwanao ilivyo.

Republished with permission from theAsianparent 

Soma PiaWhy Breastfeeding Moms May See Blood In Breastmilk

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Roshni Mahtani kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio