Chaguo la kunyonyesha mtoto mdogo ama kumpa maziwa kupitia kwa chupa huwa la mzazi. Kumnyonyesha mtoto ni njia pekee ya kumlisha kwani angali hana meno ya kukitafuna chakula. Mzazi ana uhuru wa kufanya uamuzi wa jinsi ya kumlisha mtoto wake, kupitia kwa chupa ama kumnyonyesha. Bila kuhisi kana kwamba anafanya hatia. Hakuna chaguo mbaya na nzuri, kwani mtoto bado ataweza kupata virutubisho anavyohitaji mwilini. Mama anapaswa kufanya uamuzi ulio bora na wenye afya kwake na kwa mtoto. Akihisi kuwa anatatizika, jambo bora ni kuwasiliana na daktari wake na sio watu wasio na utaalum katika mambo ya afya ya mtoto.
Kunyonyesha

Katika miezi ya kwanza sita baada ya kujifungua, mama anashauriwa na wataalum kunyonyesha mtoto bila kumlisha kitu kingine. Baada ya miezi sita, anaweza kumwanzishia chakula kigumu. Kulingana na Shirika la Afya Duniani, mtoto anastahili kunyonyeshwa hadi anapofikisha miaka miwili. Kufanya hivi kuna manufaa mengi kwa mtoto.
Manufaa ya kunyonyesha mtoto
- Kunyonyesha ni bure na hakuna gharama kwa mama. Hahitajiki kununua chochote tofauti na anavyoamua kumlisha mtoto kupitia kwa chupa
- Hahitaji kufanya chochote kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto. Wakati wowote na mahali popote ni salama kwa mama kumnyonyesha mwanawe
- Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu katika ukuaji na afya ya mtoto
- Ni muhimu katika kuboresha mfumo wa kinga kwa mtoto. Na kumlinda dhidi ya kupata maambukizi kama vile ya masikio, virusi na bakteria
- Kuboresha ushupavu wake. Utafiti unadokeza kuwa watoto wanao nyonyeshwa mara nyingi huwa shupavu zaidi ikilinganishwa na wanao lishwa kupitia kwa chupa
- Kuboresha mfumo wa kuchakata chakula katika watoto. Watoto wanaonyonyeshwa wana nafasi changa za kutatizika na kuendesha ama kuumwa na tumbo
- Kupunguza hatari za magonjwa. Mtoto anayenyonyeshwa ana nafasi changa za kupata matatizo kama ya kisukari ama mizio
Manufaa kwa mama

- Kunyonyesha mtoto mdogo kunamsaidia mama katika mambo haya!
- Kupunguza uzito wa mwili. Mwili unapochakata maziwa, unachoma kalori zaidi na kusaidia mama kupunguza uzito wa mwili
- Kupunguza hatari ya magonjwa. Mama anapomnyonyesha mtoto wake, anapunguza hatari ya kupata magonjwa kama kisukari na saratani ya moyo na ovari
- Kupunguza hatari ya kufilisika kimawazo baada ya kujifungua
- Kupona kwa kasi. Kunyonyesha mtoto kunamsaidia na uterasi ya mama kurejelea saizi yake ya hapo awali kwa kasi zaidi
- Mama anaponyonyesha, mwili unatoa homoni zinazomsaidia kuboresha utangamano wake na mwanawe.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya Kujifungua