Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya Kujifungua

2 min read
Jinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya KujifunguaJinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya Kujifungua

Tendo la mapenzi kwa wanandoa hubadilika baada ya kujifungua, kuna mabadiliko mengi. Soma zaidi kuhusu kunyonyesha na ngono baada ya kujifungua.

Hakuna wakati hasa ambapo mama anapaswa kungoja kufanya tendo la ndoa baada ya kujifungua, hata kama wataalum wengi wa afya hushauri kipindi cha kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kurejelea tendo lile. Katika kipindi hiki, mwili hupata chanya cha kupona baada ya mchakato mrefu wa kujifungua ama upasuaji wa C-section. Kunyonyesha na ngono sio wazo kuu kwake.

Hata hivyo, baada ya kujifungua, mawazo mengi ya mama ni kuhusu mtoto na huenda akawa jambo la mwisho analofikiria kuhusu ni tendo la ndoa. Mwili wake bado unazoea mabadiliko mapya na angali anazidi kupata maarifa kuhusu maisha yake mapya ya kuwa mama. Mama anapojifungua, anafungua kurasa mpya maishani na yeye pia anazaliwa upya.

Kunyonyesha na ngono: Je, kunyonyesha huathiri hamu ya ngono?

kunyonyesha na ngono

Kulingana na utafiti, wanawake wanaonyonyesha huchukua muda kurejelea tendo la ndoa ikilinganishwa na wanawake wasionyonyesha. Baada ya kujifungua, vichocheo vya prolactin na oxytocin huongeza mwilini na huwa na athari tofauti mwilini. Kupitia kwa kunyonyesha, mama huhisi kuwa matakwa yake ya kifizikia na kihisia yametoshelezwa. Na huenda akakosa kuona haja ya kutafuta mapenzi kutoka kwa mchumba wake.

Kwa wanawake wengine, huenda mambo yakawa tofauti. Huenda homoni hizi zikaongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Na jambo lolote ndogo kuwafanya wapate libido ya juu. Kunyonyesha kwa kawaida huathiri tendo la ndoa na wanawake wanapaswa kufahamu kuwa ni kawaida na sio jambo la kuwatia wasiwasi.

Kufanya ngono kutafanya maziwa yamwagike?

kumnyonyesha mume baada ya mtoto

Kuwa tayari maziwa kumwagika ikiwa unanyonyesha na kufanya tendo la ndoa. Siku chache baada ya kujifungua, chuchu za mama huwa na maziwa tele. Kuguswa katika tendo la ndoa kutafanya maziwa yamwagike. Mama anaweza kunyonyesha muda kabla ya kufanya tendo la ndoa ili kupunguza uwezekano wa maziwa kumwagika katika tendo lile. Pia anaweza mjulisha mchumba wake kuhusu kumwagika kwa maziwa katika tendo la ndoa. Mbali na hayo, anaweza kuvalia sindiria zilizo na pedi za nursing wakati wa tendo la mapenzi.

Je, ni uchungu kufanya mapenzi mama anaponyonyesha?

Mama anaponyonyesha, kichocheo cha estrogen mwilini hupungua na kinahusika na kumfanya mama awe tayari kwa tendo la ndoa. Na kumwepusha kutokana na kuraruka kwenye uke katika tendo la ndoa.

Mchumba aliye na mama anayenyonyesha anapaswa kuchukua muda kumbusu na kumpapasa mama kabla ya kitendo ili kuhakikisha kuwa ako tayari ipasavyo.

Soma Pia: Watafiti Wagundua Manufaa Zaidi Ya Kiafya Ya Kunyonyesha Zaidi Ya Miezi 6

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Jinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya Kujifungua
Share:
  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it