Kunywa Garri Unapokuwa Na Mimba Na hamu Zingine Zisizo Za Kawaida

Kunywa Garri Unapokuwa Na Mimba Na hamu Zingine Zisizo Za Kawaida

Matamanio yasiyo ya kawaida ya ujauzito yatakufanya uamke kati kati ya usiku ukitafuta vitu ambavyo kwa kawaida huwezi kula. Utajipata ukiwa na hamu ya kunywa garri unapokuwa na mimba na huku mara yako ya mwisho ulipo ikunywa ulikuwa unateseka ulipokuwa shule ya bweni.

Cha kufurahisha ni kwamba hutamani chakula tu unapokuwa na mimba.

Ni Aina Gani Ya Matamanio Yanasababisha Kunywa Gari Unapokuwa Na Mimba?

kunywa garri unapokuwa na mimba

Kwa kweli, ni tamanio ya chakula isiyo ya kawaida. Kuna aina mbili ya matamanio unapokuwa na mimba, haya ni:

a. Matamanio ya vyakula
b. Matamanio yasiyo ya chakula

Matamanio ya vyakula

Matamanio ya vyakula ni unapo pata hamu kubwa ya kula vyakula fulani. Wakati huu, huenda ukataka kula vyakula ambavyo kwa kawaida huvipendi.

Matamanio yasiyo ya chakula

Matamanio yasiyo ya chakula hufanyika unapopata hamu usiyo weza kuithibiti ya kula vitu visivyo chakula. Huenda ukapata ladha ya chaki, majivu, makaa, mchanga, matope ama hata vitu vyenye sumu kama vile rangi. Hamu hii ya kula vitu ambavyo sio chakula inajulikana kama pica.

Sayansi nyuma ya matamanio haya na kwa nini unafikiria kunywa garri unapokuwa na mimba

Sio wanawake wote hupata matamanio haya, hata hivyo, wanawake wengi wenye mimba hupata. Kulingana na karatasi hii iliyo chapishwa kwenye US National Library of Medicine, asilimia 50-90 ya wanawake huko Umarekani wanapata matamanio ya vyakula wanapokuwa na mimba. Hii ni nambari ya juu sana, inayo dhibitisha kuwa kuna visa vingi duniani kote.

Karatasi hii inazidi kuonyesha kuwa vyakula vingi vinavyo tamaniwa ni switi, vyakula baridi, vya maziwa na nyama.

 Ila, kwa nini mwili hutamani kwa sana baadhi ya vitu hivi katika mimba?

kunywa garri unapokuwa na mimba

1. Kunywa garri unapokuwa na mimba huenda kukatendeka kufuatia mabadiliko ya homoni

Ujauzito unaleta matendo mengi kwenye viwango vya homoni. Wakati huu, wanawake wengi wameripoti kuwa uwezo wao wa kuonja na kunusia unabadilika sana. Mabadiliko haya huenda yakamfanya mwanamke kula vyakula alivyo chukia hapo awali na kutupilia mbali vyakula walivyo penda hapo awali. Huenda kukamfanya apate hamu ya kula vitu kama mchanga ama sabuni kwa sababu ya harufu.

Unyeti wa hamu ya kula na kunusa unapokuwa mjamzito huenda ukamfanya mwanamke kubadilisha chakula chao wanapokuwa na mimba.

2. Hamu zako zisizo za kawaida za mimba kwa sababu mwili wako unajaribu kupata virutubisho fulani

Kulingana na karatasi hii, mwili wako unatamani baadhi ya vyakula kwa sababu unajaribu kupata virutubisho fulani kutokana chakula hicho. Kwa hivyo unaweza pata ladha ya mbio ya kuonja nyama, mboga, ama mayai kwa sababu mwili wako unahitaji iron yote unaweza pata.

Iwapo wanawake wenye mimba wanaweza sikiza tamanio zao za vyakula, watapata kuwa chakula wanacho hitaji ni cha potassium, iron, zinc, magnesium, Vitamins, and calcium.

3. Huenda matamanio yako ya chakula yasiyo ya kawaida huenda yakawa kwa sababu ya utamaduni

Wanawake wengi wajawazito kutoka kusini-kusini na kusini-mashariki wanajua kula nzu unapokuwa na mimba. Watu wengi kutoka sehemu tofauti huenda wakaelewa kwa nini wanawake wanakula clay nyeupe ama chaki kama nzu kana inavyo itwa wakati mwingine, ila ni kitendo cha utamaduni kinacho kubalika.

4. Baadhi ya wakati unakunywa garri unapokuwa na mimba kwa sababu mwili wako unabadilika

Wanawake wenye mimba wakati wote hawatamani vyakula vyenye virutubisho. Hii ndiyo sababu kwa nini unaweza jipata ukikula vyakula vyenye ufuta na vyenye sukari nyingi zaidi zisizo na afya.

drinking garri during pregnancy

Lengo ni kula kila kitu kwa uthibiti.

 Jinsi ya kukumbana na hamu ya kula unapokuwa na mimba kama vile kula garri unapokuwa na mimba

• Huenda wakati wote ukakula unacho kitamani

Huenda ikawa vigumu kwako kuangalia mbali na harufu ya kutamanisha ya mchanga, ila kwa sababau haina virutubisho vyovyote, unapaswa kufikiria tena.

• Kuongeza uzito wa mimba sio salama kwako
 Mwili wako hauhitaji ule chakula cha watu wawili unapokuwa na mimba. Unahitaji kalori karibu 300-500 kuegeza mtoto wako anaye kua. Iwapo lazima uitikie mwito wako wa hamu ya kula, kumbuka kuwa sio lazima umalize kontena hiyo ya ice krimu.

 Kudumisha uzito wenye afya ni muhimu kwa afya yako na ile ya mtoto wako aliye tumboni.

• Iwapo ina sumu, sio wazo nzuri kuila

 Huku kuna maana kuwa, hakuna sabuni, rangi, ama makaa. Itakuwa bora kuangalia mbali na vitu ambavyo huenda vikawa na sumu.

Baadhi ya vitu visivyo vya kawaida ambavyo wanawake wajawazito hutamani Nigeria

Baada ya kuongea na idadi ya wamama, baadhi yao wanaitikuwa kuvitamani vyakula hivi na bidhaa zisizo za vyakula. Tazama orodha hii:

 • Bitter cola
 • Kola nut
 • Kunywa garri unapokuwa na mimba 
 • Nzu ama native chalk
 • Mchanga
 • Red clay
 • Ice cream
 • Chocolati
 • Corn pap
 • Milkshakes
 • Pilipili hoho
 • Vyakula vyenye pilipili 
 • Keki
 • Peppery suya
 • Makala
 • Detergent
 • Matunda
 • Switi
 • Banga stew ama ofe aku
 • Pastries kama vile doughnuts, meat pies, chin-chin
 • Supu ya tawi kali Bitter 
 • Supu ya Okro 
 • Kunu
 • Tiger nut milk ama kunu aya
 • Ndizi
 • Udara ama African star apple
 • Mchanga
 • Maji ya mvua 
 • Jivu
 • Majivu ya sigara
 • Akara
 • Supu ya Tuwo na draw 
 • Vinywaji baridi laini

Usiwe na shaka unapoanza kuhisi hamu ya kula vitu ambavyo hukuwa umezoea hapo awali unapokuwa na mimba. Mwili wako unapitia mabadiliko mengi, na unapaswa kuishi nayo. Kuwa upande salama, unaweza fuata vidokezo hivi vya kuthibiti tamani zako za kula chakula unapokuwa na mimba.

Kumbukumbu: Medicine.net

US National Library of Medicine

Soma pia: Issues that cause uncontrollable anger during pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio