Je, Ni Salama Kunywa Maji Moto Ukiwa Na Mimba?

Je, Ni Salama Kunywa Maji Moto Ukiwa Na Mimba?

Kuwa na maji tosha mwilini unapokuwa na mimba ni muhimu ili kuhakikisha kuwa una amniotic fluid tosha. Lakini je, kunywa maji moto ukiwa na mimba ni salama?

Mtoto aliye ndani ya tumbo yako ana asilimia 75 ya maji. Asilimia hiyo huanza kupunguka mtoto anapo zidi kukua, na kwa sababu hiyo, inategemea kiwango cha mama cha maji anayo kunywa ili awe na amniotic fluid tosha. Kwa sababu hii kunywa maji ni muhimu sana kwa sababu amniotic fluid ndogo huenda ikasababisha changamoto za kuzaliwa na hata kuharibika kwa mimba. Ni maarifa ya kimsingi kuwa wanawake wajawazito wanapaswa kuepuka kukosa maji tosha mwilini vyote wawezavyo. Lakini, je, kunywa maji moto katika mimba ni salama?

Kunywa maji moto katika mimba: Ni Salama? 

drinking hot water during pregnancy

Kunywa maji tosha kuna saidia mwili wako kwa njia tofauti. Kama vile kuimarisha afya ya misuli na mifupa yako na kuusaidia mwili kupigana dhidi ya maambukizi na kutumia virutubisho zaidi. Ina aminika kuwa kunywa maji moto (sio moto sana) kuna faida nyingi za kiafya, lakini hakuna ushuhuda wa kisayansi kudhibitisha imani hii. Walakini, watafiti wana anza kufanya utafiti kuona iwapo manufaa ya kiafya ni sawa na tunayo amini. Tuna angazia baadhi ya faida za kunywa maji moto.

  • Kusafisha mfumo wako wa utumbo

Kunywa maji moto kunatoa chembe chembe za sumu kutoka kwa mfumo wako wa utumbo na kuiweka hai. Sumu hizi ziki zidi, huenda ukawa na upungufu wa maji mwilini na kukufanya utatizike kuenda haja kubwa. Wakati ambapo maji baridi hayana athari kwa ufuta kwenye utumbo wako, maji moto yana yeyusha ufuta wako na kutengeneza nafasi ya mwendo.

  • Kuboresha mzunguko wa damu mwilini

how drinking warm water can help you during pregnancy

Mzunguko wako wa damu mwilini unaweza ongezeka kwa sana unapo kunywa maji moto ikilinganishwa na maji baridi. Maji moto yana fungua misuli yako ya damu, kuifanya iwe mikubwa na kukubalisha mwendo rahisi wa damu mwilini mwako.

  • Kuepuka kufunga choo

Kufunga choo ni jambo la kawaida katika wanawake wengi walio na mimba. Lakini unaweza epuka tatizo hili kwa kunywa maji moto asubuhi wakati tumbo yako haina kitu. Kuna saidia kuboresha mwendo wa tumbo na kuhakikisha kuwa hautatiziki na kufunga choo.

  • Kuongeza nishati yako mwilini

drinking hot water during pregnancy

Mabadiliko ya homoni na ukweli kuwa una kiumbe kinacho kua mwilini mwako huenda ukahisi unachoka wakati mwingi. Kwa bahati nzuri, maji moto yana kusaidia kupunguza uchovu. Maji moto yana fanya hivi kwa kuboresha mzunguko wa damu mwilini mwako na pia mwendo wa mifupa na misuli yako. Pia unaweza ongeza kiwango kidogo cha ndimu kwenye maji yako moto.

  • Kuboresha afya ya mafua yako

Kugonjeka homa unapokuwa na mimba sio nzuri kwako ama kwa mtoto wako. Kwa hivyo kunywa maji moto kunaboresha afya ya mafua yako, na kupunguza nafasi za kupata maambukizi ya koo, kukohoa, homa na mafua. Sababu kwa nini si vyema kugonjeka ukiwa na mimba ni kuwa utahitajika kunywa dawa na sio vyema kwa mtoto wako.

Kunywa maji moto katika mimba: Vidokezo zaidi kwa wanawake wenye mimba kuhusu kunywa maji

  • Maji hayapaswi kuwa moto sana kwani yata choma mdomo wako. Maji ya vuguvugu ni bora zaidi
  • Kunywa angalau glasi nane za maji kila siku kuhakikisha hauna upungufu wa maji mwilini
  • Epuka maji ya mfereji kwa sababu huenda yakawa na viwango vingi vya madini ambayo yanaweza hatarisha mtoto wako
  • Wakati wote beba chupa ya maji kila mahali unapo enda
  • Pia unaweza hitaji maji kutoka kwa vyanzo vingine kama supu, sharubati ya matunda na mboga

Wakati wa ujauzito, kukosa maji tosha mwilini kunaweza sababisha matatizo mengi kama vile kichefuchefu, kuhisi kizungu zungu na oedema. Kuepuka hizi, hakikisha una maji tosha mwilini na usingoje hadi unapo hisi kiu kunywa maji. Pia, usikunywe maji moto sana kabla ya kungoja yapoe yawe vuguvugu.

Chanzo: Medical News Today, Healthline

Soma Pia: Shaka Za Ujauzito: Kupata Mimba Ukiwa Na Zaidi Ya Miaka 35

Written by

Africa parent