Je, Ni Sawa Kunywa Pombe Ukiwa Na Mimba?

Je, Ni Sawa Kunywa Pombe Ukiwa Na Mimba?

Kunywa pombe ukiwa mjamzito kuna athari hasi kwa afya ya mtoto wako na kumuweka katika hatari ya matatizo ya kimaumbile baada ya kuzaliwa.

Ushauri mkuu utakao pata kutoka kwa marafiki na jamaa zako wanapo gundua kuwa una mimba, kitu cha kwanza huenda kikawa, "koma kutumia vileo". Na huenda ukawa na maswali mengi akilini. Mbona huu ndiyo ushauri wa kwanza unao pokea? Kunywa pombe ukiwa na mimba kuna athari zipi? Kwako na kwa mtoto?

Mama anapo pata mimba, ana shauriwa kula chakula cha afya kwani, chakula hakisaidii utendaji kazi mwilini mwake tu, mbali mtoto anaye kua tumboni mwake ana tarajia chakula hiki pia. Huku kuna maana kuwa, chochote ambacho mama anatumia, kinamfikia mtoto kupitia kwa kitovu kisha kuingia kwa placenta na kumfikia mtoto.

Pombe itam zuia mtoto kukua ipasavyo, huenda ika athiri ubongo wake na viungo vingine vinavyo anza kukua katika wakati huu. Matatizo sugu ambayo huenda yaka ibuka kufuatia utumiaji vileo ungali na mimba ni kama vile:

Athari hasi za pombe kwa fetusi

Je, Ni Sawa Kunywa Pombe Ukiwa Na Mimba?

Kupoteza mimba: Kunywa pombe ukiwa na mimba kunaweza sababisha kuharibika kwa tumbo ama mimba ingali miezi michache.

Kifo cha mtoto angali tumboni: Katika trimesta yako ya pili ya mimba, unaweza mpoteza mtoto wako angali tumboni.

Uchungu wa uzazi usio komaa: Kwa wanawake wanao zidi kutumia vileo na mvinyo wakiwa katika safari yao ya mimba, huenda waka tatizika na uchungu wa mapema wa uzazi. Kujifungua mtoto kabla ya wakati, huenda akaugua matatizo mengi ya kiafya kama vile matatizo ya kupumua na mafua ambayo hayaja komaa.

Changamoto za kimwili kwa mtoto: Baadhi ya watoto wanao zaliwa kwa mama aliye kuwa akitumia vileo akiwa na mimba, huenda wakawa na matatizo ya moyo ama figo.

FASDs (Fetal alcohol spectrum disorders): Watoto wanao ugua maradhi haya huenda waka athiriwa kimaumbile, wanavyo fikiria na uwezo wao wa kusoma. Kuwa na matatizo ya kiakili na ukuaji ambayo huenda yaka dumu.

Watoto walio na FASDs huenda:

kunywa pombe ukiwa na mimba

  • Wakawa wafupi, wadogo na wenye uzani wa chini wa kimwili
  • Kuwa na ngozi laini kati ya pua na ulimi wa juu badala ya umbo la kawaida
  • Kuwa na uwezo duni wa kukumbuka na matatizo ya kusoma
  • Kutatizika kuwa makini darasani
  • Matatizo ya kuzungumza ama kuandamana na watu wengine
  • Kufanya uamuzi duni

Mama, una shauriwa kujitenga na mvinyo katika kipindi hiki muhimu sana maishani mwako. Kisha baada ya kumaliza kumnyonyesha mtoto wako, utakuwa huru kuanza kutumia vileo tena.

Soma Pia: Vyakula Vya Mimba: Umuhimu Wa Kalisi Katika Ujauzito

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio