Sababu Kwa Nini Kuolewa Ukiwa Na Miaka 30 Huenda Ikawa Wazo Nzuri

Sababu Kwa Nini Kuolewa Ukiwa Na Miaka 30 Huenda Ikawa Wazo Nzuri

Uta dhamini maisha ya kuolewa zaidi unapo olewa ukiwa katika miaka yako ya 30, kwa hivyo sio wazo mbaya kufunga ndoa katika umri huu!

Sio rahisi kufikisha miaka ishirini na mitano na kukosa shinikizo kutoka kwa jamaa na marafiki zako kuhusu kupata mchumba ama hata mtoto. Wakati mwingi, huenda mwana dada akaingia katika uhusiano ama ndoa kufuatia shinikizo kutoka kwa wanafamilia wengine. Maswali kama 'utapata bwana lini', 'utaolewa lini' ama 'utatoka kwenu lini' ni maarufu sana. Lakini ngoja na utulie kidogo. Unafahamu kuwa maisha haiishi baada ya miaka ishirini na mitano? Na bado kuna mambo yanayo pendeza sana ambayo yanaweza kufanyika baada ya umri huo? Tuna angazia kwa nini kuolewa ukiwa na miaka 30 huenda ikawa wazo nzuri.

Ndoa ni jambo kubwa na wakati wote, watu wanashauriwa kuwa wapole na kuchukua muda kufikiria kabala ya kufanya uamuzi mkuu wa kuingia katika ndoa.

Kwa Nini Kuolewa Ukiwa Na Miaka 30 Sio Wazo Mbaya

hofu za wanawake katika uhusiano

 1.Utakuwa imara kihisia na kifedha

Nafasi kubwa ni kuwa utakuwa imara kifedha ikilinganishwa na ulivyo unapo kuwa katika miaka yako ya ishirini. Hatusemi kuwa ni vibaya kupata mtoto ukiwa katika miaka yako ya 20. Na sio kusema kuwa kila kitu kitakuwa shwari unapo fikisha miaka 30. La hasha, lakini pia utakuwa umekomaa katika matumizi yako ya kifedha na unavyo fanya uamuzi unao husika na fedha.

2. Utakuwa na uamuzi bora kuhusu mambo unayo yataka

Na sio kwa maisha tu, mbali pia kutoka kwa mchumba wao. Huenda ikakuchukua muda kuamua unacho kitaka na mambo ambayo hautakubali kutoka kwa mchumba wako. Lakini unapo fika miaka 30 bila shaka utakuwa umefanya uamuzi wa unayo yataka. Pia, ni vyema kukumbuka kuwa mambo sio rahisi katika ndoa kama inavyo onekana kwenye sinema.

3. Wakati zaidi wa kuishi maisha

Unapo fikisha miaka 30, utakuwa umezuru zaidi, kutembea sehemu mbali mbali na kuyapitia mengi. Utakuwa umepata wakati tosha wa kuwa katika uhusiano, kuvunjwa moyo na kuelewa mapenzi zaidi. Ni vyema kufunga ndoa ukiwa umeyapitia haya yote ikilinganishwa na kufunga ndoa mapema na kushangaa jinsi inavyo hisi.

4. Uta dhamini maisha ya kuolewa zaidi

kuwa hamasisha wanawake

Uta dhamini maisha ya kuolewa zaidi unapo olewa ukiwa katika miaka yako ya 30. Katika kipindi hiki, watu wengi huwa wamepitia maisha yao ya kufanya sherehe na mambo mengi ambayo wangependa kufanya. Na wako tayari kuwacha hayo yote na kuishi na mtu wanaye hisi wanampenda na wako huru kufanya mambo tofauti pamoja.

5. Utakuwa na harusi bora zaidi

Katika umri huu, utakuwa na marafiki hasa unao jua kuwa wanakudhamini na unao wadhamini. Na ambao ungependa wajumuike nawe katika siku yako kuu. Utakuwa na ujasiri mwingi zaidi maishani na pia fedha tosha za kufanya harusi ya ndoto zako.

Soma PiaMalengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio