Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Umuhimu Wa Kupata Msaada Katika Ulezi Baada Ya Kujifungua

3 min read
Umuhimu Wa Kupata Msaada Katika Ulezi Baada Ya KujifunguaUmuhimu Wa Kupata Msaada Katika Ulezi Baada Ya Kujifungua

Kuomba usaidizi katika ulezi sio ishara ya kukosa nguvu, mbali kunamsaidia mama kupata wakati tosha wa kupumzika na kumhudumia mtoto wake.

Kuzungumza kuhusu mahitaji yetu sio jambo rahisi haijalishi hatua ya maisha tuliyo katika. Na haiwi rahisi kwa mama aliyejifungua. Hasa ikiwa yeye ni moja kati ya watu wasioweza kamwe kujieleza na kuona kana kwamba wanawasumbua watu. Katika kipindi hiki, mama ana mambo mengi, angali anapona baada ya kujifungua na anazidi kujifunza jinsi ya kuwa mzazi. Ni kawaida kwa mzazi wa mara ya kwanza kuhisi kuwa anawachosha watu anapo omba msaada. Hata hivyo, kujaribu kufanya kila kitu bila usaidizi kutamfanya mama achoke na huenda kukapunguza idadi ya maziwa ya mama. Ni vyema kwa mama mpya kuomba usaidizi katika ulezi.

Kulea mtoto hasa katika wiki za kwanza chache baada ya kujifungua kunahitaji msaada mwingi. Mama hapaswi kuhisi kana kwamba anapaswa kujifanyia kila kitu. La hasha, ni vyema kupata watu wa kumfanyia kazi za nyumba na wakati wake kuwa wake na wa mwanawe. Kwa wanawake wanaotatizika kuomba msaada, tazama njia za kukurahisishia jambo hili.

Jinsi ya kuomba usaidizi katika ulezi

kuomba usaidizi katika ulezi

  1. Fafanua unachotaka

Mama anapopata mtoto, huanza maisha upya kwani hajui jinsi ya kuwa mzazi, na haijalishi idadi ya vitabu ambavyo amesoma kabla ya kujifungua. Ukweli ni kuwa, anajifunza kuwa mzazi katika tendo la kulea. Ana mambo mengi ya kufikiria kuhusu. Mama anapaswa kuwa na orodha ya kazi ambazo anahitaji msaada kufanya. Kwa njia hii, itakuwa rahisi kutafuta mtu wa kumsaidia na kila jukumu ama mtu atakaye mfanyia majukumu haya.

2. Kuwa na orodha ya mambo ya kufanya kila siku

Siku huwa na mpango zaidi mama anapoamka akijua majukumu yake ya siku. Kumbuka kuwa, katika kipindi hiki, mama hapaswi kufanya majukumu yanayo husisha kuinama sana ama kuinua vitu nzito. Kufanya hivi kutamletea matatizo kwenye mgongo. Kufahamu majukumu yanayofanyika kila siku na atakaye yafanya.

3. Tafuta mfanyakazi

Kuwa na mtu anayemfanyia mama kazi za kinyumbani kama kusafisha nyumba, vyombo na nguo za mtoto kunampunguzia mawazo mengi ya kutafuta mtu wa kumsaidia kila siku. Baada ya kusaidiwa kufanya kazi hizi, mama atakuwa na wakati tosha wa kuwa na mwanawe.

kuomba usaidizi katika ulezi

4. Kuwa na marafiki wanaolea 

Kuwa na kundi la marafiki wanaolea humpa mama egemezo tosha katika safari yake mpya ya ulezi. Anapotatizika na kitu chochote, anajua kuwa ana marafiki ambao anaweza kuwauliza jinsi ya kutatua suala fulani. Pia anahisi kuwa chochote anachokipitia ni cha kawaida na wanawake wengine wamekipitia. Kupata usaidizi wa kihisia ni muhimu kwa mama katika kipindi hiki.

5. Kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako

Sio jambo rahisi, lakini kuzungumza na mchumba wako na kumweleza kuwa unahitaji msaada hata kwa kazi kama kubadilisha nepi za mtoto ni vyema. Mama atapata wakati wa kupumzika na kumpa mchumba wake chanya cha kutengeneza uhusiano wa karibu na mtoto wao. Kuomba usaidizi katika ulezi sio ishara ya kukosa nguvu, ni muhimu kupata usaidizi.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Umuhimu Wa Kupata Msaada Katika Ulezi Baada Ya Kujifungua
Share:
  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it