Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi Ya Kuongeza Maziwa Ya Mama: Vidokezo Kwa Mama Mpya

2 min read
Jinsi Ya Kuongeza Maziwa Ya Mama: Vidokezo Kwa Mama MpyaJinsi Ya Kuongeza Maziwa Ya Mama: Vidokezo Kwa Mama Mpya

Ni vyema kwa mama kuwasiliana na daktari wake ili ampe ushauri bora kuhusu anachostahili kula na kunywa kuongeza idadi ya maziwa.

Wazazi wapya hasa wa mara ya kwanza huwa na shaka tele wakati mwingi kama sio wakati wote. Kushangaa iwapo mtoto wao ako sawa, ikiwa wanamtunza anavyostahili na kama anashiba. Wanataka mambo yote yawe sawa na kuhakikisha kuwa mtoto wao anakua ipasavyo. Wazazi huwa na shaka mtoto anapokuwa na joto ama baridi kama kushuku kuwa kuna jambo lililo na kasoro. Mama huenda akawa na shaka na kushangaa iwapo mtoto anapata maziwa tosha. Je, ni njia zipi anaweza kutumia kuongeza idadi ya maziwa ya mama?

Vidokezo kwa mama anayenyonyesha

kuumwa na chuchu

Mama anaweza kutumia mbinu hizi kuhakikisha kuwa anatoa kiwango tosha cha maziwa ya mama cha kumtosheleza mwanawe.

  1. Anza kunyonyesha mapema

Mama anapaswa kuhakikisha kuwa anamnyonyesha mtoto wake katika lisaa la kwanza baada ya kujifungua. Hata hivyo, huenda matatizo yakaibuka mama anapojifungua na kufanya iwe vigumu kwake kumnyonyesha mtoto na hapaswi kuhisi hatia. Lakini, akiweza ni vyema kuanza kumnyonyesha mapema.

Mama anaponyonyesha, kumgusisha mwanawe kwa ngozi yake kuna boresha uhusiano wao. Kuanzia mapema kunamwezesha kunyonyesha mtoto hadi miezi sita bila kumlisha chakula kingine.

2. Kunyonyesha mtoto mara nyingi

Katika siku za kwanza, mtoto anapaswa kunyonyeshwa hadi mara nane ama kumi kwa siku. Kufanya hivi kunauhimiza mwili wako kutoa maziwa zaidi kutosheleza mahitaji ya mtoto. Kumnyonyesha mtoto mara zaidi kunaboresha kiwango cha maziwa kinachochakatwa na kuongeza idadi yake. Hakikisha unamnyonyesha mtoto kila mara anapotaka kunyonya.

3. Kunywa maji na viowevu tosha

kuongeza idadi ya maziwa ya mama

Ni muhimu kwa mama kuchukua viowevu na maji tosha anaponyonyesha. Viowevu vinatumika katika kuchakata maziwa na kuhakikisha mwili wa mama una maji tosha.

Ni vyema kwa mama kuhakikisha kuwa anazidi kunywa glasi nane za maji kwa siku. Anaweza kunywa maji akinyonyesha pia.

4. Punguza fikira nyingi

Fikira nyingi huathiri homoni mwilini na kupunguza idadi ya maziwa ambayo mama anaweza kutoa. Mama anapaswa kutunzwa katika kipindi hiki na kuhakikisha kuwa hafanyi kazi ngumu ili asiwe na mawazo mengi na atosheleze mahitaji ya mwanawe.

5. Kuwasiliana na daktari wake

Mama anaponyonyesha atapata maoni mengi na tofauti kuhusu vyakula vitakavyo msaidia kuongeza kuongeza idadi ya maziwa ya mama. Ujumbe huu huenda ukawa sio sahahi na haujapitishwa na Shirika la Afya Duniani. Ni vyema kwa mama kuwasiliana na daktari wake ili ampe ushauri bora kuhusu anachostahili kula na kunywa kuongeza idadi ya maziwa iwapo ana shaka kuwa hatoshelezi mahitaji ya mwanawe.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Jinsi Ya Kumdhamini Mchumba Baada Ya Kujifungua Mbali Na Kufanya Ngono

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Breastfeeding & Formula
  • /
  • Jinsi Ya Kuongeza Maziwa Ya Mama: Vidokezo Kwa Mama Mpya
Share:
  • Matatizo ya Kunyonyesha Yanayowakumba Mama Wapya na Suluhu

    Matatizo ya Kunyonyesha Yanayowakumba Mama Wapya na Suluhu

  • Fahamu Manufaa Ya Kunyonyesha Kwa Wote Mama Na Mtoto

    Fahamu Manufaa Ya Kunyonyesha Kwa Wote Mama Na Mtoto

  • Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Na Umuhimu Wa Kumshika Mtoto Ifaavyo

    Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Na Umuhimu Wa Kumshika Mtoto Ifaavyo

  • Matatizo ya Kunyonyesha Yanayowakumba Mama Wapya na Suluhu

    Matatizo ya Kunyonyesha Yanayowakumba Mama Wapya na Suluhu

  • Fahamu Manufaa Ya Kunyonyesha Kwa Wote Mama Na Mtoto

    Fahamu Manufaa Ya Kunyonyesha Kwa Wote Mama Na Mtoto

  • Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Na Umuhimu Wa Kumshika Mtoto Ifaavyo

    Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Na Umuhimu Wa Kumshika Mtoto Ifaavyo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it