Vyakula Vya Lactogeni Vya Kumsaidia Mama Kuongeza Maziwa

Vyakula Vya Lactogeni Vya Kumsaidia Mama Kuongeza Maziwa

Vyakula vyenye afya vya kukusaidia kukumbana na tatizo la upungufu wa maziwa ya mama.

Je, wewe ni mama anaye nyonyesha na una tatizo la upungufu wa maziwa ya mama? Vyakula hivi vya lactogeni vya kuongeza maziwa ya mama vitakusaidia kuboresha utoaji maziwa na kunyonyesha kwa urahisi.

Unahitaji Vyakula Vya Lactogeni Iwapo Una Tatizo La Upungufu Wa Maziwa

Upungufu wa maziwa wakati unapo nyonyesha huenda ukaathiri hisia za kuwa mama hasa kwa mama wa mara ya kwanza. Wamama hukosa furaha wanapo gundua kuwa chuchu zao hazitoi maziwa tosha ya kunyonyesha watoto wao. Wanawake wengi tayari hushangaa iwapo wao ni wazazi wazuri, na mama asipo toa maziwa tosha, hisia za kutokuwa tosha huenda zika athiri kiwango cha utoaji wa maziwa.

Iwapo hautoi maziwa tosha ya mtoto wako, huenda kukawa na sababu nyingi zinazo sababisha kupunguka kwa maziwa yako ya mama. Kwanza, huenda ikawa hauli vyakula tosha vya lactogeni kuongeza utoaji wa maziwa. Sababu za kimazingara na homoni kutokuwa sawa huenda kuka athiri utoaji wa maziwa. Unapaswa kujua kwa kweli chanzo ili ujue jinsi ya kutatua tatizo hilo.

Baadhi ya sababu kuu zinazo sababisha kupunguka kwa maziwa ya mama kwa mama anaye nyonyesha:

Mabadiliko ya homoni
Prolactin ni homoni inayo husika na utoaji wa maziwa. Kunapo kuwa na kutokuwa sawa kwa utoaji wa homoni hii, utoaji wa maziwa una athiri.

• Lishe

Ni kweli kuwa lishe yako huathiri utoaji wa maziwa. Unapaswa kula matunda na mboga kwa wingi ili kutoa maziwa ya mama tosha.

Kutokunywa maji tosha

Maji ni muhimu sana kwa utoaji wa maziwa. Usipo kunywa maji kiwango kinacho shauriwa cha glasi nane kwa siku, huenda utoaji wako wa maziwa uka athiriwa.

Kuto nyonyesha vya kutosha
Cha kuhuzunisha ni kuwa, baadhi ya wamama hukosa maziwa tosha wasipo nyonyesha watoto kwa muda mrefu.

Vyakula vya lactogeni vya kuongeza maziwa ya mama

Athari kuu ya utoaji mdogo wa maziwa ni kuwa mtoto wako hata pata virutubisho tosha. Hutaki mtoto wako akose chakula, kwa hivyo kuboresha utoaji wa maziwa ya mama ni muhimu. Mtoto wako anahitaji maziwa ya mama kwa sababu yana virutubisho vyote muhimu vinavyo hitajika vya ukuaji na maendeleo ya mtoto.

Pia, kwa miezi ya kwanza sita ya maisha ya mwanao, una shauriwa kumnyonyesha pekee kwani maziwa ya mama ndiyo chakula pekee ambacho kinaweza kuchakatwa na tumbo zao laini. Wakati ambapo maziwa yako ya mama, chakula cha kipekee cha mtoto, yako kwa idadi ndogo, unapaswa kutafuta suluhu.

Huenda mama akawa na shaka anapo kosa kuwa na maziwa tosha ya mama ya mtoto wake. Mbali na hisia na athari za kisaikolojia, utoaji mdogo wa maziwa ya mama huwa na athari za kifizikia. Chuchu huenda zikakauka ama kupasuka usipo toa maziwa tosha. Chuchu zilizo kauka huenda zikawa chungu na ndiyo sababu kwa nini unapaswa kuwa na suluhu.

Bahati ni kuwa kuna vyakula vya lactogeni vinavyo kusaidia kuongeza maziwa ya mama. Unaweza tatua hali hii kwa kuongeza vyakula hivi vya ladha kwenye lishe yako.

Vyakula vya lactogeni vya kuboresha maziwa ya mama

Fenugreek na mbegu za fennel: Hizi zina uwingi wa omega-3 fatty acids, beta carotene na virutubisho vingine ambavyo husaidia kuongeza maziwa. Unaweza nunua mbegu hizi kwenye duka kubwa ama duka za madawa.

Mboga za majani: Kula mboga za majani husaidia sana katika kuboresha utoaji wa maziwa ya mama.

kuongeza maziwa ya mama

Kitunguu saumu: Kitunguu saumu kinasifika kwa faida nyingi hasa za kiafya. Ni muhimu katika kuboresha utoaji wa maziwa. Kuweka kipande kimoja ama viwili vimetosha kuongeza kiwango cha maziwa. Ni vyema kukumbuka kuwa unapaswa kula kitunguu saumu kwa idadi sawa, kwani kula kingi huenda kuka athiri harufu ya maziwa ya mama. lactogenic foods

Oatmeal: Iwapo viwango vyako vidogo vya maziwa ya mama vina sababishwa na idadi ndogo ya iron mwilini, ni vyema kuongeza oatmeal kwenye lishe yako. Itasaidia kuongeza utoaji wa maziwa yako kwa kasi.

Maji: Unahitaji kunywa maji kwa wingi kwa afya yako ya ujumla na pia kuweza kutoa maziwa zaidi ya mtoto wako.
kuongeza maziwa ya mama

Matunda: Matunda yana wingi wa virutubisho na yatakusaidia kukumbana na tatizo la upungufu wa maziwa ya mama. Kama vile papai, tikiti, maembe, machungwa na matunda mengineyo.

kuongeza maziwa ya mama

Salmon

Salmon ina wingi wa omega-3 fatty acids, kwa hivyo ni muhimu kuongeza kwa lishe yako hasa kwa mama anaye nyonyesha mtoto. Ina fanya maziwa yawe na virutubisho zaidi, ni muhimu kwako na mtoto wako.

Mchele wa hudhurungi: Nafaka hii mzima ni muhimu katika kuboresha utoaji wa maziwa na iko katika orodha ya vyakula vya lactogeni ambavyo vinasaidia kuboresha maziwa ya mama.

• Karoti: Wamama wanao nyonyesha wanahitaji kula karoti. Zina wingi wa vitamini A na beta-carotene inayo saidia katika utoaji wa maziwa.
Mbali na vyakula hivi vya lactogeni, kuna mabadiliko ya mitindo ya maisha ambayo inayo weza kukusaidia kunyonyesha kwa urahisi na kufanya mazoezi ni nambari moja kwa orodha yako.
foods

Kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kukusaidia na utoaji wa maziwa. Madaktari wana shauri wamama wanao nyonyesha kufanya mazoezi ili kusaidia na mzunguko wa damu mwilini na katika virutubisho kutumika mwilini. Huku kuna saidia kuboresha utoaji wa maziwa. Walakini, unahitajika kufanya mazoezi huku umevalia sindiria nzuri kwa mazoezi magumu. Hautaki chuchu zako zianze kuuma.

Kwa hitimisho, kumbuka kula lishe iliyo na wingi wa matunda na mboga freshi. Na pia lishe zenye virutubisho na maji kwa wingi. Mnyonyeshe mtoto kwa pande zote mbili na umhimize kunyonya kwa muda mrefu.

Kumbukumbu: NHS

Soma pia: Breastfeeding mums who eat spicy food have less picky babies

Written by

Risper Nyakio