Mwanamke anaweza kuwa na sababu tofauti za kutaka kupata mapacha. Huenda akawa angependa kujifungua mara moja kisha kumalizana na kisha kumalizana na kupata watoto. Huku wengine wakipendezwa na kuwa na mapacha. Kuna sababu tofauti zinazo athiri uwezo wa mama kupata mimba ya mapacha.
Sababu Zinazo Athiri Uwezo Wa Mama Kupata Mimba Ya Mapacha

Ikiwa familia yenu kuna mapacha wengi, una nafasi zaidi za kupata watoto mapacha. Ikiwa familia ya mwenzi wako ina mapacha, haiathiri nafasi zako za kupata watoto zaidi ya mmoja kwa njia yoyote.
Kila mara mama anapo beba mimba, nafasi zake za kutunga mimba ya mapacha huongezeka.
Kulingana na utafiti, wanawake walio na umri zaidi wana nafasi zaidi za kutunga mimba ya mapacha. Hasa wanawake wanaoshika mimba baada ya kufikisha umri wa miaka 35. Kulingana na utafiti, hili linawezekana kwasababu baada ya umri huu, ovari hutoa zaidi ya yai moja. Na kuongeza uwezekano wa kupata mimba ya watoto zaidi ya mmoja.
Kulingana na utafiti, wanawake walio na BMI ya juu wana nafasi zaidi za kutunga mimba ya mapacha. Wanawake walio na BMI ya 30 na zaidi wana nafasi za juu za kujifungua mapacha.
Mbali na sifa hizo, mwanamke anaweza fanya uamuzi wa kutumia uvumbuzi mpya wa kisayansi kumsaidia kupata mimba ya mapacha. Michakato kama ya IVF (invitro fertilization) kunaweza msaidia mwanamke kutimiza lengo hili. Pia, kuna dawa zinazo ongeza utoaji wa mayai.
Hitimisho

Kuna imani nyingi zinazo zingira uwezo wa mama kupata mtoto zaidi ya mmoja. Shukrani kwa teknolojia, mama anaweza kupata mimba hata kama anatoka kwa familia ambapo hakuna mapacha wengine. Kwa kutumia uvumbuzi wa kisasa wa kiteknolojia na pia dawa.
Kupata watoto mapacha ni jambo la kusisimua, lakini ni jambo la busara kwa wazazi kulenga kupata mtoto mwenye afya. Ni vyema kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawasiliana na wataalum wa afya wanapo anza juhudi za kutunga mimba. Kwa njia hii, watapata ushauri kuhusu jinsi ya kupata mtoto mwenyee afya, haijalishi iwapo ni mimba ya kwanza ama ya pili.
Soma Pia: Vyakula Muhimu Kwa Mtoto: Umuhimu Wa Uji Wa Muhogo Kwa Mtoto!