Kwa mwanamke anaye tatizika kupata mimba ama ambaye angependa kuongeza nafasi zake za kupata mimba, kuna baadhi ya vitu ambavyo anaweza kufanya.
Njia hasa ya kuongeza nafasi zake za kutunga mimba ni kufahamu siku ya kupevuka kwa yai. Mara nyingi, hii huwa siku ya 14 baada ya kuanza hedhi yake. Baada ya yai kuachiliwa kutoka kwa ovari, lina uwezo wa kudumu mwilini kwa siku moja. Huku manii yakiwa na uwezo wa kudumu mwilini hadi wiki moja. Siku mbili kabla na siku tatu baada ya siku ya kupevuka kwa yai, huwa siku ambazo mwanamke ana rutuba zaidi. Na ana nafasi zaidi za kutunga mimba.
Kalenda ya hedhi
close up of calendar and clock on green background, planning for business meeting or travel planning concept (close up of calendar and clock on green background, planning for business meeting or travel planning concept, ASCII, 109 components, 109 byte
Miili ya wanawake huwa tofauti, sawa na mizunguko ya hedhi kwa kila mmoja. Huku wanawake wengine wakiwa na mizunguko ya hedhi iliyo ya kawaida, kwa wengine hubadilika. Kuwa na kalenda ya mzunguko wa hedhi, kuna msaidia mwanamke kufahamu siku anazo kuwa na rutuba zaidi. Ili kufanya tendo la ndoa na kuongeza nafasi yake ya kutunga mimba. Kalenda hii pia inaweza kumsaidia kuepuka kutunga mimba kwa kumsaidia kufahamu siku anazo stahili kujiepusha na tendo la ndoa. Kalenda hii inamsaidia mwanamke kufahamu siku atakapo pata hedhi.
Chati ya rutuba
Chati hii ya rutuba ina mwezesha mwanamke kufahamu mzunguko wake wa hedhi. Kwa kudhibitisha mabadiliko mwilini kama vile, ongezeko la temprecha, mabadiliko kwenye kamasi ya uke na siku zenye rutuba.
Uzazi wa mpango

Kwa mwanamke anaye tumia mojawapo ya mbinu za uzazi wa mpango na angependa kupata mimba. Ni vyema wakati wote kuwasiliana na daktari wake ama kuenda kwenye kituo cha afya. Kwa wanao tumia tembe, koma kuzitumia, kwa walio na kifaa cha IUD, lazima kitolewe mwilini.
Kutumia uzazi wa mpango haku athiri uwezo wako wa kutunga mimba siku za usoni. Ila kuna baadhi ya wanawake watakao chukua muda zaidi kutunga mimba baada ya kukoma kutumia mojawapo ya mbinu za kupanga uzazi. Mwanamke anaweza tumia njia hizi kuongeza nafasi za kupata mimba, lakini akumbuke kuwasiliana na daktari wake kwanza.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!