Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

Mara nyingi, jukumu la afya wanandoa wanapo jaribu kupata mimba huachiwa wanawake. Ila, hili ni jukumu la watu wawili.

Unapokuwa tayari kuanza safari yako ya kuwa mzazi, hakuna njia ya kutabiri wakati utakapo ona kipimo cha mimba chanya. Lakini kama una afya nzuri, unafanya ngono mara kwa mara na mpenzi wako na hautumii mbinu za kudhibiti uzalishaji, unapaswa kutarajia kupata mimba katika mwaka wako wa kwanza wa kujaribu. Alieleza Amelia Mclennan ambaye ni mtaalum wa matibabu katika kituo cha afya cha UC Davis. Kulingana na utafiti uliofanyika katika nyanja hii, karibu nusu ya wanandoa hupata mimba katika kipindi cha miezi 6 na asilimia 70-80 hutunga mima katika kipindi cha mwaka mmoja. Aliongeza.

Lakini wana ndoa wanaweza ongeza ama kuboresha nafasi zao za kutunga mimba na kuwa wazazi. Siri ni kugundua mambo hasi na chanya, ya kufanya na kuto fanya kuhusu uzazi. Tazama miongozo hii ya kukusaidia kufuzu katika lengo lako.

Jinsi ya kuongeza nafasi zako za kutunga mimba

kuongeza nafasi zako za kutunga mimba

Wanawake: Fahamu na uwe makini kwa ishara

Mimba hutungwa pale ambayo yai hupatana na manii. Kwa hivyo zinahitaji kuwa mahali pamoja katika wakati sawia. Ili kusaidia kufanyika kwa hili, unaweza angazia wakati ambapo kupevuka kwa yai hutendeka ama ovulation. Huu ni wakati ambapo ovari zako huachilia yai. Hakikisha kuwa unafanya mapenzi siku hiyo ama siku chache kabla na katika siku hiyo.

Njia rahisi ya kujua siku ambapo ovulation itatendeka mwilini mwako ni kwa kuhesabu siku 14. Kwa kawaida, ovulation huwa siku ya kumi na nne ya kipindi chako cha hedhi. Kwa mfano, kama utaanza hedhi yako siku ya tatu ya mwezi fulani, siku ya 14 itakuwa tarehe 17 ya mwezi huo. Na hiyo ndiyo siku ambapo una ovulate na pia una nafasi za juu za kutunga mimba unapo fanya ngono siku hiyo.

Kuna vipimo hasa vinavyo nunuliwa kwenye maabara, vya kukusaidia kujua wakati unao ovulate.

Wanaume: Kuwa mwangalifu kwa afya yako

stay healthy at a desk job

Mara nyingi, jukumu la afya wanandoa wanapo jaribu kupata mimba huachiwa wanawake. Ila, hili ni jukumu la watu wawili, mwanamme pia anapaswa kuhakikisha kuwa afya yake iko sawa wanapo jaribu kutunga mimba. Kulingana na mtaalum wa afya ya uzazi wa kiume huko Stanford.

Ni vyema kukumbuka kuwa kuna uhusiano mkuu kati ya afya yako ya kijumla na ya uzalishaji. Kwa hivyo, hakikisha kuwa una kula vyema, kufanya mazoezi mara kwa mara, una angazia uzani wa afya wa mwili na kuzingatia mitindo yenye afya ya kulala na pia hauna fikira nyingi. 

Kwa wanawake, ili kuongeza nafasi zako za kutunga mimba, unapaswa kuhakikisha kuwa uzani wako ni wa afya pia. Anza kuzingatia kuishi maisha yenye afya, kupitia kwa lishe yako, kufanya mazoezi na kupunguza unywaji wa kafeini nyingi.

Wanandoa wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafanya ngono mara kwa mara ili kuboresha nafasi zao za kupata mtoto.

Soma Pia: Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio