Jinsi Ya Kuongeza Stamina Yako Kwa Njia 6 Za Kiasili

Jinsi Ya Kuongeza Stamina Yako Kwa Njia 6 Za Kiasili

Are you always low on energy? Here are 6 ways to improve your stamina naturally

Stamina ya juu ni sababu kwanini baadhi ya watu wana uwezo wa kufanya shughuli ngumu kwa kipindi cha wakati bila ya kuchoka ama kupungukiwa na pumzi. Stamina ya kifizikia na kiakili zina umuhimu sawa kwa sababu wakati ambapo moja inakusaidia kuweza kufanya kazi za kifizikia, ingine inakusaidia kustahimili kazi za kiakili. Huku kuna maana kuwa unapo angazia kujenga stamina yako, ni muhimu kujaribu na kuimarisha kifizikia na kiakili. Katika makala haya, tuna kuonyesha njia 6 za kuongeza stamina yako kiasili.

Jinsi ya kuongeza stamina yako kiasili

Kuna njia asili za kuongeza stamina, na hapa chini kuna baadhi ya njia bora za kufanya hivi.

exercising to improve energy through the day

  • Mazoezi

Iwapo una kiwango cha chini cha nishati, huenda ukafikiria kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kusaidia popote katika hatua hii. Ila, umenoa. Kufanya mazoezi kutasaidia kujenga stamina yako na kukusaidia kuhisi una nguvu zaidi unapofanya shughuli za kifizikia na kiakili. Masomo yameonyesha kuwa kufuata ratiba ya mazoezi kunapunguza viwango vya uchovu unao husishwa na kazi.

  • Kafeini

Hiki ni kiungo kichechemuzi ambazo kinaweza ongeza mpigo wako wa roho huku kikiupa mwili wako nishati ya muda. Kafeini inapatikana kwenye chai, kahawa na vinywaji vyepesi. Somo lililo chapishwa kwenye Makala ya Michezo ya Sayansi lilifanyika ambapo kundi la wanaume 9 ambao ni waogeleaji mashuhuri walikunywa kikombe cha kafeini cha miligramu 3 lisaa limoja kabla ya kuanza mazoezi. Watafiti waligundua kwamba waogeleaji hawa walifanya vyema na hakukuwa na tofauti kwenye mpigo wao wa moyo. Walakini, epuka kunywa kafeini wakati wote kwa sababu mwili wako utazoea. Huku kutapunguza athari ya kafeini na huenda ukawa na uzoefu.

coffee bean

  • Meditation ama  yoga

Yoga na meditation hazisaidii kutulia na kupunguza mawazo tu. Pia kunaweza saidia kujenga fizikia yako na stamina ya kiakili. Utafiti uliofanyika kwa kutumia wanafunzi wa matibabu 27 na ulionyesha kuwa yoga na meditation inapunguza kiwango cha fikira nyingi na kuimarisha uhai wa mwili.

  • Muziki

Mbali na ukweli kuwa muziki unaweza geuza hisia za mtu, pia unaimarisha uwezo wa roho yao kufanya kazi ipasavyo. Mtego ni kusikiza muziki huku ukifanya mazoezi na stamina yako ita imarika. Iwapo utafiti zaidi utahitajika, utafiti mdogo ulipata kwamba mpigo wa moyo wa walio sikiza muziki wakifanya mazoezi ulikua mdogo kuliko wa wale ambao hawakusikiza.

Music helps

  • Ashwagandha

Inatumika kwa ujumla wa mwili na kuwa na nguvu, , Ashwagandha ni mmea wa asili ambao pia unaweza kutumika kuimarisha uwezo wa kufikiria na kupunguza kukwazwa kimawazo na kuimarisha viwango vya nishati. Masomo yaliyo fanyika kwa watu 50 wazima ambao pia ni wana michezo kuchukua mili gramu 300 za kiungo hiki kwa wiki 12. Ilipatikana kuwa uwezo wa kuvumilia wa roho zao kwa ujumla na miili yao ili imarika.

Inatumika kwa ujumla wa mwili na kuwa na nguvu,

  • Chakula bora

Chakula unachokula kinachangia pakubwa unavyo hisi. jaribu kula lishe bora iliyo na virutubisho vyote na ziwe na protini na wanga kwenye lishe yako. Vyakula vyenye protini ni kama vile mayai, nyama, na samaki, njugu na mbegu na legumes ama familia ya maharagwe, maziwa ya bururu. Wanga ni vyakula kama vile mihogo, maharagwe na mchele wa hudhurungi. Vyakula hivi vina kaa kwa mwili kwa muda mrefu na kukupa nashati siku yote. Kwa watoto, tuna vyakula vilivyo na nishati nyingi vyao na unaweza kutumia ratiba hii ya ki Nigeria ya chakula cha watu wazima.

Lazima uwe nayo akilini kuwa viwango vya nishati hu ongezeka kisha kupunguka. Kwa hivyo ni sawa na kawaida kutokuwa katika kiwango chako cha juu zaidi wakati wote. Pumzika vyema kisha uusikize mwili wako ili usi ufanye ukachoka.

Soma PiaHow To Handle A Hyperactive Child At Home

Chanzo: Healthline

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio. 

Written by

Risper Nyakio