Vyakula 5 Vya Kuboresha Ubora Na Idadi Ya Manii Mwilini Mwako

Vyakula 5 Vya Kuboresha Ubora Na Idadi Ya Manii Mwilini Mwako

Protini na vitamini E zinazo patikana kwenye mayai zina saidia kulinda seli za manii kutokana na kupunguka.

Ugumba katika wanaume mara nyingi husababishwa na kiwango cha chini cha manii. Kulingana na ripoti iliyo tolewa na Shirika ya Afya Duniani, idadi ya manii yenye afya ni milioni 15 kwa kila ml, na idadi yoyote chini ya hiyo sio sawa.

Huenda ikawa vigumu kurekebisha hali ya ugumba kwa wanaume. Lakini, habari nzuri ni kuwa, unaweza boresha hali hii kupitia kwa lishe yenye afya, kubadilisha mtindo wako wa maisha na vinginevyo. Tazama vyakula bora katika kuongeza ubora na idadi ya manii.

Kuongeza Ubora Na Idadi Ya Manii Kupitia Kwa Chakula

  1. Mandizi

Pregnancy snacks

Hili ni tunda lililo na wingi wa vitamini na linalo usaidia mwili wako kutoa manii yenye afya na pia kuongeza idadi ya manii mwilini. Wanaume wanashauriwa kuliongeza kwenye lishe zao. Hakikisha unakula tunda hili angalau mara tatu ama nne kwa wiki.

2. Kitunguu saumu

kuongeza idadi na ubora wa manii

Kitunguu saumu kina sifika kwa manufaa yake mengi ya kiafya. Kinasaidia kusafisha damu mwilini na kuepusha mishipa kufungana, na kuboresha mzunguko wa damu kwenye kibofu. Kina wingi wa vitamini B6 na selenium ambazo zinasaidia katika utoaji wa manii yenye afya.

3. Mayai

kuongeza ubora na idadi ya manii,

Protini na vitamini E zinazo patikana kwenye mayai zina saidia kulinda seli za manii kutokana na kupunguka. Pia, mayai yanasaidia katika kuongeza idadi ya manii inayo tolewa na kuboresha uwezo wa kudumu kwa muda.

4. Broccoli

Vyakula 5 Vya Kuboresha Ubora Na Idadi Ya Manii Mwilini Mwako

Hii ni mojawapo ya mboga zinazo sifika zaidi kwa ladha na manufaa mengi ya kiafya. Ina asidi ya folic na vitamini ya B9 zote ambazo ni muhimu katika utoaji wa manii zaidi.

5. Chokleti nyeusi

vitamu tamu katika mimba

Kwa muda mrefu, chokleti imejulikana kuwa kitamu tamu kwa wanawake wengi. Na haija husishwa sana na wanaume. Ila sasa hivi, mambo yame badilika. Na utafiti unao zidi kufanyika unaonyesha kuwa zina saidia wanaume katika utoaji wa manii yenye afya.

Ikiwa una shaka kuwa huenda manii yako hayana afya, tembelea kituo cha afya ili uweze kufanyiwa vipimo zaidi!

Soma Pia: Vidokezo Vya Kukusaidia Kujua Ikiwa Manii Yana Afya Kwa Kuangalia

Written by

Risper Nyakio