Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

Kuongeza uzito katika uhusiano bora ni jambo linalo shuhudiwa kwa asilimia kubwa? Kipi kinacho tendeka kati ya wanandoa na kusababisha hili? Soma zaidi!
Huenda ikawa umeona ama wewe ni mmoja kati ya watu walio shuhudia kuongeza uzito katika uhusiano bora. Kipi kinacho sababisha jambo hili? Punde tu unapokuwa katika uhusiano bora na wenye furaha, unaanza kuongeza uzito. Huenda pia ukawa umeshuhudia jambo hili kwa wazazi wako ama majirani wako.
Kulingana na utafiti, kuna mambo mengi yanayo sababisha tukio hili. Mojawapo ya sababu kwa nini hili hutendeka ni imani kuwa, wachumba hawana shinikizo la kuvutia kwa watu wengine. Kwani wako katika uhusiano bora na ulio na furaha. Kwa hivyo wanapunguza mawazo mengi na kuto ishughulikia fizikia yao tena. Tazama sababu zaidi.
Kuongeza uzito katika uhusiano bora: Kwa nini wanandoa huongeza uzito katika uhusiano wenye furaha?
Utafiti zaidi una dhibitisha kuwa, wachumba huwa na tabia sawa na huenda zika sababisha ongezeko la uzito. Kwa watu wanao ishi pamoja, wao huiga mitindo sawa ya maisha na huenda ikawa sio yenye afya sana.
- Wanawake kula kiwango sawa cha chakula na wanaume
Mfano mzuri wa kuiga mitindo ya maisha ya mchumba wako ni wanawake kula chakula sawa ama kingi zaidi kuliko waume. Kula chakula kingi kuna sababisha ongezeko la uzito kwa jinsia zote mbili.
2. Kula viwango vikubwa vya chakula kilicho pikwa nyumbani
Ukiwa peke yako, ni vigumu kupika chakula kingi na wakati wote, na kwa sababu hii, watu wasio na wachumba huenda wakakosa kula mara kwa mara.
Wanandoa wanao ishi pamoja wana majukumu ya kindoa kama vile lishe ya familia. Majukumu haya yata wafanya wapike chakula kingi na wakati wote. Ukihusisha pombe na vyakula vyenye sukari. Vyote ambavyo vinachangia katika ongezeko la uzito.
3. Kupata watoto
Kupata watoto kuna changia katika ongezeko la uzito. Mama anapo pata mimba, bila shaka hushuhudia ongezeko la uzito wa mwili. Pia, wazazi humaliza chakula cha watoto wao wanapo bakisha.
4. Malengo ya kiafya ya mchumba wako
Utafiti mwingine ulipata kuwa kuto endelea kwa malengo ya kiafya ya mchumba wako huenda yaka laumiwa kwa kukosa kufuzu kwa yako. Mchumba anaye shindwa kupunguza upana wa kiuno chake anaweza sababisha upungufu wa motisha wa kutimiza malengo yako. Ni sababu hii inayo wafanya wanandoa wengi kuongeza uzito pamoja ikilinganishwa na wakati unapo kuwa peke yako.
Kumbukumbu: Huffington Post, healthline
Soma Pia: Mwongozo Kwa Wanandoa Wanao Jaribu Kupata Mimba Haraka