Ikiwa una uzani mdogo wa mwili, huenda ukawa na maswali mengi kuhusu jinsi ambavyo unaweza kuongeza uzito wa mwili kwa njia yenye afya. Unataka njia ambayo haitakuwa na athari hasi kwa mwili wako.
Baadhi ya njia za mkato zinazotumika kutimiza lengo hili kama kula na kunywa vitu vilivyochakatwa kama soda na burgers. Huwa na athari hasi kwa mwili kwa kuongeza hatari za kuugua magonjwa kama vile kisukari, ugonjwa wa moyo na saratani. Kuna baadhi ya saratani zinazosababishwa na ulaji wa chakula kisicho chenye afya. Ufuta mwingi kwenye sehemu ya tumbo kunahusika na kuongeza hatari ya kupata saratani.
Kwa wanaolenga kuongeza uzito wa mwili, ni muhimu kuhakikisha kuwa wanatumia njia zenye afya.
Kuongeza Uzito wa Mwili Kwa Njia Yenye Afya

- Ongeza kiwango cha kalori unachochukua
Jambo muhimu zaidi katika kuongeza uzani wa mwili ni kuongeza kiwango cha kalori unachokichukua. Hakikisha kuwa unakula kalori za kuutosheleza mwili wako. Unaweza kutumia kikokotoo cha kalori kupima kiwango cha kalori unachokula kwa siku. Anza kwa kalori kati ya 300 na 600 kwa siku kisha uongeza hadi kalori 1,000 kwa siku.
2. Kula chakula chenye protini kwa sana
Ulaji wa protini bora hasa zinazotokana na wanyama ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo bora ya mwili. Protini huchangia pakubwa katika kuongeza misuli ya mwili. Ulaji wa protini hupunguza njaa na kufanya uhisi kushiba kwa muda mrefu zaidi. Baadhi ya vyanzo bora vya protini ni kama vile samaki, mayai, nyama, njugu na bidhaa za maziwa.

3. Kula vyakula vinavyoongeza nishati
Matunda, mboga, nafaka na kunde ni muhimu katika lishe. Vyakula vinavyokuwa na viwango vya juu vya nishati ni kama vile njugu, bidhaa za maziwa kama maziwa ya bururu, nyama na nafaka. Nyama kama ya kuku, ng'ombe na nguruwe.
Hakikisha unakula mchele wa hudhurungi ikilinganishwa na mchele mweupe. Badala ya kula mkate asubuhi, kula viazi vitamu, nduma, viazi vikuu na oats.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Manufaa 7 ya Tufaha za Kijani Kwa Afya na Urembo