Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Viwango vya manii ni muhimu sana katika mambo ya uzalishaji. Kuna njia tofauti za kuongeza viwango vya manii hasa kwa kupitia chakula unachokila.

Ubora wa manii ni muhimu ili kutimiza lengo lako la kupata watoto. Mara nyingi, wanaume kukosa nguvu za kumpa binti mimba una husishwa na kiwango kidogo cha manii. Nambari ya wastani ya manii inayo kuwa kwenye sampuli ya manii ndiyo inayo julikana kama kiwango cha manii. Na kufuata mwongozo kutoka kwa World Health Organisation, kiwango cha manii cha kawaida huwa na hadi milioni 15 kwa kila milimita ama milioni 39 angalau kwa kila sampuli. Kwa hivyo, hii ina maana kuwa kiwango chochote cha manii chini ya milioni 10 kwa kila milimita ni chini ya kawaida. Kwa hivyo katika visa vya uzazi wa kiume kuhusishwa na kiwango cha chini cha manii, suluhu ni kuongeza kiwango cha nambari. Makala haya yana angazia jinsi ya kuongeza viwango vya manii kwa kutumia chakula.

Jinsi ya Kuongeza Viwango vya Manii Kwa Kutumia Chakula

Kuna njia zingine za kuongeza kiwango cha chini cha manii. Kama vile kutumia matibabu. Ila tunakuletea vyakula tofauti ambavyo vinaweza kusaidia na kiwango cha chini cha manii kwa njia asili.

  • Mchicha

Increase sperm count by food

Mchicha na mboga za familia hiyo huwa na folic acid, ambayo ni muhimu sana katika utoaji wa manii yaliyo na afya. Kwa hivyo kuna nafasi kuwa manii yako haitakuwa yenye afya unapokuwa na kiwango cha chini cha folate. Kula spinachi ili kuweka idadi ya folate mwilini juu na ili utoe manii yenye afya ili ufikie na ku fertilise yai kwa urahisi.

  • Chokleti nyeusi

Huenda watu wengi wakaweka hii kama vitamu tamu ambavyo unapaswa kujitenga navyo. Ila chokleti nyeusi ni nzuri kwa viwango vya manii. Kwa hivyo inunue. Unaweza tengwa na watu wanao penda vitu vyenye sukari ili upate faida nyingi. Na iwapo una amini wanacho sema, mbali na kuwa na amino acids zinazo ongeza viwango vya manii, inaweza kufanya ufike kwenye kilele cha ngono mbio.

  • Vyakula vilivyo na wingi wa Zinc

Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Kuwa na viwango tosha vya zinc ni muhimu katika lengo lako la kuongeza manii mwilini. Zinc inaweza patikana kwenye vyakula vya wanyama kama vile samaki na nyama. Kulingana na somo la kushuhudia, kukosa zinc tosha kuna husishwa na ongezeko katika kukosa uzalishaji kwa wanaume na testosterone iliyo chini. Kwa hivyo iwapo una viwango vya chini vya zinc, ulaji mwingi utafanya uwe na viwango zaidi vya testosterone na manii.

  • Kitunguu saumu

Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Kiungo hiki hujitokeza kuwa matibabu ya kitu kimoja ama kingine wakati mwingi. Hii ni kwa sababu ni mojawapo ya chakula kikuu ambacho unaweza pata karibu nawe. Na pia ni cha bei nafuu. Shukrani kwa vitamini (B6 na selenium) inayo kuwa kwa kitunguu saumu, ina saidia na tatizo la viwango vya chini vya manii. Pia, kitunguu saumu kina kubalisha damu kuzunguka kwa urahisi mwilini, na kukubalisha damu kufikia kibofu cha mwanamme.

  • Pomegranate 

Pomegrenate helps increase sperm count

Mbali na ladha ya kupendeza, pomegranate inasaidia kuboresha viwango vya chini vya manii. Baadhi ya watu wanaila kwa sababu ya uwezo wake wa kuongeza hamu ya ngono. Ina wingi wa antioxidants zinazo pigana na free radicals zilizo kwenye mfumo wako na damu. Iwapo huwezi pata tunda hili, tafuta sharubati yake.

  • Walnuts

Walnuts Increase sperm count by food

Omega-3 fatty acids huongeza mzunguko wa damu mwilini, na kwa hivyo kukubalisha damu zaidi kufika kwenye sehemu za uume. Mbali na hayo, zina wingi wa arginine na antioxidants zinazo boresha wingi wa semen na kupigana dhidi ya toxins kwenye mfumo wako wa damu.

  • Nyanya

kuongeza viwango vya manii

Nyanya ni mojawapo ya vyakula vinavyo patikana kwa urahisi katika soko nyingi. Zina antioxidant ya lycopene inayo saidia manii sana na hata kuyasaidia kuzunguka kwa urahisi. Iwapo hupendelei kula nyanya, unaweza kunywa sharubati yake.

  • Mandizi

Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Vitamini A, B1 na C ni vitamini zilizoko kwenye mandizi. Kwa hivyo ulaji mwingi wa mandizi utasaidia mwili wako kuwa na vitamini hizi na zita boresha afya yako ya manii na hata utoaji wake. Pia, mandizi huwa na enzyme maarufu kama bromelain inayo saidia katika mwendo wa manii. 

  • Mayai

kuongeza viwango vya manii

Mayai ni maarufu kwa uwezo wake wa kuboresha kiwango cha manii kwenye wanaume walio na matatizo ya uzalishaji. Vitamini E na protini zilizoko kwenye mayai zina linda manii yako dhidi ya free radicals zinazo punguza kiwango chako cha manii. Na pia, yana saidia mwili wako kutoa manii yenye afya.

  • Berry 

Kula Vyakula Hivi Kuongeza Idadi Ya Manii Yako

Familia yote ya berry ni muhimu katika kutibu kuto zalisha kunako husikana na afya ya manii na kiwango chake. Kama vile blueberries, blackberries, cranberries na strawberries. Familia yote ya berry ina quercetin na resveratrol ambazo ni anti-oxidant na anti-inflammatory. Kupitia kwa ulaji mkubwa wa hizi, zina boresha afya yako na viwango vya manii. Sharubati za blackberry na cranberry hupatikana sana katika maduka makuu.

Hitimisho

Vyakula tulivyo orodhesha vitakusaidia na matatizo yako ya manii na pia afya kwa ujumla. Walakini, huenda ikawa hauhitaji haya tu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo huenda ukahitajika kukaa mbali navyo iwapo ungependa kuongeza kuongeza viwango vya manii na nafasi zako za uzalishaji. Vitu hivi ni kama vile utumiaji mwingi wa madawa ya kulevya na pombe, na kuepuka soy, kupunguza fikira nyingi, kuvuta sigara na kuwacha madawa ambayo huenda yana sababisha kiwango cha chini cha manii.

Soma zaidi:Jinsi Ambavyo Tende Huongeza Idadi Ya Manii Na Faida Zake Kwa Wanaume

Written by

Risper Nyakio