Mama aliyejifungua hivi karibuni angependa kujua iwapo kuna njia ya kujilinda dhidi ya kupata mimba isiyoathiri utoaji wa maziwa. Kupanga uzazi baada ya kujifungua kutampa wakati tosha kulea mtoto aliyejifungua na kuupa mwili wakati tosha wa kupona. Kabla ya kufanya uamuzi iwapo angependa kupata mtoto mwingine ama la. Katika makala haya, tunaangazia iwapo ni salama kupanga uzazi kwa mama anayenyonyesha.
Kupanga uzazi kwa mama anayenyonyesha

Upangaji uzazi ni salama kwa mama anayenyonyesha na hakutakuwa na athari hasi kwa mtoto mdogo. Hata hivyo mbinu za kupanga uzazi zinazotumika ikiwa ni za homoni zinapaswa kuwa za progestin peke yake.
Mbinu kama implant ama kijiti cha mkono, IUD na sindano ama tembe za progestin.
Wiki za kwanza chache baada ya kujifungua, mwanamke hushauriwa kujitenga na kufanya mapenzi ili kuupa mwili muda tosha kupona. Kipindu cha wiki sita, baada ya muda huu, daktari na mama huwa na kipindi cha kujadili mbinu bora ya kupanga uzazi.
Manufaa ya kupanga uzazi kwa mama anayenyonyesha
Mama aliyejifungua hushauriwa kuchukua miezi 18 kabla ya kupata mimba tena. Kupata mimba ingine chini ya miezi 18 kuna madhara haya:
Kujifungua kabla ya wakati. Mama huwa katika hatari ya kujifungua kabla ya wiki 37 kufika. Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati huwa na matatizo ya kiafya kwani mfumo wao wa kinga haukuwa umekomaa.
Uzito wa chini. Kujifungua tena kabla ya miezi 18 kupita huwa na hatari ya kujifungua mtoto aliye na uzani wa chini.
Madhara ya uzazi wa mpango kwa mama anayenyonyesha

Kupanga uzazi muda mfupi baada ya kujifungua huwa na athari ya kupunguza maziwa ya mama. Iwapo mama anatumia uzazi wa mpango wenye homoni ya estrogen. Kwa sababu hii, mwanamke anashauriwa kutumia mbinu za kupanga uzazi zisizo za homoni ama zenye homoni za progestin peke yake.
Kutokuwa na maziwa tosha huwa na athari hasi kwa mtoto. Ukuaji wake wa kawaida utaathiriwa na kupunguza uzazi ama kutokua kwa kiasi kinachotarajiwa.
Wakati wote, ni vyema kwa mwanamke kujadiliana na daktari wake mbinu bora. Kupanga uzazi kwa mama anayenyonyesha kuna manufaa kwake na kwa mtoto.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Athari Hasi za Matumizi Marefu ya Tembe za Kupanga Uzazi