Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

Jinsi Ya Kupata Mimba Baada Ya Kipindi Chako Cha Hedhi

Je, ni rahisi kwa mwana dada kupata mimba baada ya hedhi? Hasa kwa wanawake walio na vipindi visivyo kawaida vya hedhi. Tunapo sema vipindi visivyo vya kawaida, ni kwa wasichana ambao wana siku chini ya 21 ama zaidi ya 36 kabla ya kupata kipindi kinacho fuata cha mimba. Kwa hivyo iwapo una vipindi visivyo vya kawaida vya hedhi na ungependa kupata mimba, hapa kuna vidokezo vya vitu muhimu unavyo paswa kuangazia.

Kitu muhimu kuhusu mimba ni kujua wakati wa kufanya mapenzi hasa kwa wanawake walio na hedhi zisizo za kawaida. Kutunga kuna andamana na ovulation. Yai linapo achiliwa kutoka kwa ovari, chakato unao julikana kama ovulation. Ni wakati huo ambapo mwili hujitayarisha kutunga mimba. Ila wakati huo ukipita bila kutunga yai, uterasi ina nyooka na kuyeyuka kisha kutoka kupitia kwa vagina. Na mwanzo wa kipindi cha hedhi. Pia, vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida kuingiliana mchakato tulio angazia na kupunguza nafasi zako za kupata mimba.

Kupata Mimba Baada Ya Hedhi: Vidokezo Muhimu

kupata mimba baada ya hedhi

 

 • Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida: Iwapo hedhi yako huwa ya kipindi chini ya siku 21 ama zaidi ya siku 36, fahamu kuwa una hedhi isiyo ya kawaida. Njia mojawapo ya kujua ni kuwa huwezi tabiri kipindi chako kijako cha hedhi.
 • Ovulation: Una nafasi zaidi za kupata mimba siku zinazo karibia siku yako ya ovulation. Ovulation ni pale ambapo yai lina achiliwa kutoka kwa ovari liki ngoja kutungwa.

 

Kwa nini ni vigumu kwa wanawake walio na vipindi visivyo vya kawaida kupata mimba?

Kila mwanamke hu ovulate siku 14 kabla kipindi chake cha hedhi. Kwa mwanamke aliye na vipindi visivyo vya kawaida, ata ovulate siku ya 14 iwapo ana kipindi cha siku 28. Iwapo kipindi chake ni cha siku 32, ata ovulate siku ya 18. Kwa bahati mbaya,wanawake walio na vipindi visivyo vya kawaida, sio rahisi kusema kwa uhakika siku yao ya kuovulate. Hii inaifanya iwe vigumu kwa wanawake hawa kupata mimba kwa sababu hujui utakavyo hesabu kinyume nyume siku ya 14.

Kulingana na George Carson, ambaye ni OB/GYN, mwanamke anaye ovulate na ana kipindi cha siku 28 ana ovulate siku 13 kwa mwaka. Kwa hivyo ana nafasi 13 za kupata mimba na anaweza tambua siku hizi ni zipi. Lakini iwapo ana ovulate mara 6 kwa mwaka, ana nafasi nusu ya za mwanadada anaye ovulate mara za kawaida.

Pia, wanawake walio na vipindi visivyo vya kawaida huenda wakakosa kuovulate kabisa. Huenda wakawa na hedhi ila kuachiliwa kwa yai hakufuati. Hali hii kwa kimombo inajulikana kama anovulatory.

Jinsi ya kupata mimba na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida

kupata mimba baada ya hedhi

Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida huathiri uwezo wako wa kutunga mimba, ila kwa kutumia vidokezo hivi, unaweza ongeza nafasi zako za kutunga mimba.

 

 • Hakikisha una angalia siku zako za ovulation 

Kalenda ya hedhi itakusaidia kujua siku unapo ovulate, na wakati ambapo una nafasi za juu za kutunga mimba.

 

 • Fanya mapenzi zaidi

Manii yanaweza baki mwilini mwako kwa hadi siku sita. Kwa hivyo, kufanya mapenzi zaidi huenda kukaongeza nafasi zako za kupata mimba hasa iwapo una vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida. Kadri unavyo fanya mapenzi zaidi, ndivyo unavyo ongeza nafasi zako za kutunga mimba.

Pia, jua wakati unaopaswa kufanya mapenzi, tumia kiti muhimu kupima mkojo wako. Hii inawezekana kwa sababu kabla ya ovulation, wanawake hutoa homoni ya luteinizing hormone (LH). Inayo lifanya yai kuanguka kutoka kwa ovari.

 

 • Kula vyakula vya afya

  Iwapo vipindi vyako vya hedhi sio vya kawaida, kula vyakula vilivyo na afya. Kaa mbali ama ujitenge na vyakula vyenye uzito mwingi na wanga. Pia, kaa mbali na vyakula vilivyo chakatwa na vitamu tamu na badala yake, kula matunda zaidi, mboga na nafaka.

 

 • Kuwa na uzito wa mwili wa wastani

  Hii ni kwa wanawake wenye uzito mwingi na walio na uzito mdogo. Ni muhimu kuwa na uzito wa wastani kwa sababu matatizo ya uzito huenda yakafanya homoni zako kutokuwa sawa. Unapokuwa na tatizo la homoni, huenda ukapata vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na kutatiza hali yako ya kujaribu kupata mimba. Wanawake walio na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na wana fanya uamuzi wa kupata mimba wanapaswa kuwa na uzito wa wastani kuwasaidia na homoni zao. Ni vyema kwa kila mwanamke kuhakikisha kuwa anaongea na daktari wake kabla ya kutunga mimba.

 

 • Punguza fikira nyingi

kupata mimba baada ya hedhi

Kupunguza fikira nyingi kuna athari kubwa iwapo unajaribu kupata mimba baada ya hedhi. Fikira nyingi huenda zikatatiza juhudi zako za kutunga na kuathiri nafasi zako za kuwa mjamzito. Jaribu kufuata mbinu za kupunguza fikira zako wakati wa mchana, kwani kujaribu kuwa na mimba huenda kukaleta fikira zake.

Soma piaEffective Home Remedies For Irregular Periods

Written by

Risper Nyakio