Kufahamu mzunguko wa hedhi kunamsaidai mwanamke kujua siku hatari za kufanya tendo la ndoa. Kwa kawaida, wastani wa mzunguko wa hedhi huwa siku 28. Mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi, hadi mwanzo wa kipindi cha pili cha hedhi kinapo anza. Kuelewa mzunguko wa hedhi, kunamsaidia mwanamke kupata mimba baada ya kipindi cha hedhi.
Sifa za mzunguko wa hedhi wa kawaida

- Siku za mzunguko wa hedhi
Kwa kawaida, mzunguko wa hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Wanawake wengi huwa na wastani wa siku 28.
- Mzunguko wa hedhi wa kawaida
Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa na uwiano wa idadi ya siku kati ya mzunguko mmmoja wa hedhi hadi mwingine. Kwa mzunguko wa hedhi wa kawaida, huwa na siku sawa kati ya kipindi kimoja hadi kingine kila siku. Kwa mfano, ikiwa mwanamke alipata kipindi cha hedhi tarehe 5 mwezi huu, atapata kipindi kifuatacho tarehe sawa ama katika wiki iliyo na siku hiyo.
Hii ni idadi ya siku ambazo mwanamke anavuja damu akiwa katika hedhi. Kwa kawaida huwa kati ya siku 3 hadi 7.
- Kiwango cha damu kinachotoka
Hedhi huwa tofauti. Huenda mwezi huu ukapata kipindi kizito na mwezi ujauo kipindi kikawa chepesi zaidi.
Kupata mimba baada ya hedhi kipindi cha hedhi

Kupata mimba baada ya hedhi kunafanyika wanandoa wanapojihusisha katika kitendo cha mapenzi mama anapokuwa katika siku hatari. Siku ya kupevushwa kwa yai ama ovulation huwa siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi. Mwanamke ana nafasi zaidi za kupata mimba anapofanya ngono katika siku hii. Kufanya mapenzi siku tano kabla ya siku ya kupevushwa kwa yai kunamuweka katika hatari ya kupata mimba. Kwani manii yana uwezo wa kubaki hadi kwa kipindi cha hadi siku tano.
Kupata mimba baada ya hedhi kunafanyika mama anapofanya mapenzi siku tano kabla ya siku ya kupevuka kwa yai ama siku yai linapopevushwa mwilini. Siku mbili baada ya kupevushwa kwa yai hadi mwanzo wa kipindi kijacho cha hedhi, ni siku salama za kufanya ngono bila kinga na kutopata mimba. Kwa wanawake wasio tayari kuwa wazazi, ni vyema kufahamu siku hizi. Hata hivyo, tendo la wanandoa linapaswa kuwa kati ya watu waliofunga pingu za maisha na wanaofahamu hali yao ya kiafya.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuepuka Kupata Mimba Kwa Mama Anaye Nyonyesha!