Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Umefanya uamuzi kuwa ni wakati mwema kwako kupata mtoto. Huenda ukawa na shaka kuhusu muda utakao chukua kupata mimba baada ya kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji. Kwa wanawake wengine, huenda ikachukua muda mrefu ikilinganishwa na wengine. Kulingana na mbinu ambayo wamekuwa wakitumia. Mbinu za kudhibiti uzazi zilizo na homoni huathiri mwili sana na huchukua muda baada ya kuacha kuzitumia kusawasisha viwango vya homoni mwilini. Uzuri ni kuwa, mbinu hizi za homoni (estrogen ama progestin) hazi athiri uwezo wako wa uzalishaji.

Unapaswa kukoma kutumia mbinu za uzalishaji lini?

Endelea kutumia vidhibiti mimba hadi pale ambapo utahisi kuwa uko tayari kupata mimba. Huenda mwili wako utakuwa tayari kutunga mimba mwezi mmoja ama miwili baada ya kukoma kutumia mbinu hizi. Kwa mbinu za homoni, unaweza wacha miezi michache kabla lakini uzidi kutumia mbinu zingine zisizo na homoni kama vile kondomu.

Inachukua muda upi kupata mimba?

kupata mimba baada ya kudhibiti uzalishaji

Ikiwa unatumia mbinu kama kondumu ama diaphragm, una nafasi nyingi za kupata mimba punde tu unapo fanya ngono. Kwa mbinu zilizo na homoni, kama vile tembe, IUD ama patches, mwanamke anaweza tunga mimba miezi michache baada ya kukoma kuzitumia. Ni vyema kukumbuka kuwa sio kwa wanawake wote na kuna mambo mengi yanayo athiri uwezo wa kupata mtoto mbio. Kama vile mtindo wako wa maisha, na geni zako. Kuna wanawake ambao huchukua muda zaidi ili kusawasisha homoni mwilini.

Tazama:

Tembe za kudhibiti uzalishaji

kupata mimba baada ya kudhibiti uzalishaji

Unaweza kutunga mimba kati ya miezi 1-3 baada ya kuacha kutumia tembe hasa zenye homoni zilizo changanywa. Wanawake wengi hupata mimba mwaka wa kwanza baada ya kukoma kutumia mbinu hii. Kulingana na utafiti, wanawake walio tumia tembe hizi kwa zaidi ya miaka minne huwa na uzalishaji wa juu ikilinganishwa na walio tumia kwa chini ya miaka miwili.

Implant (mbinu ya kupandikiza)

Kulingana na mwili wako na mtindo wako wa maisha, kuna uwezekano wa kupata mimba punde tu implant yako inapo tolewa na daktari wako.

Sindano ya depo provera

Tofauti na mbinu zingine za kudhibiti mimba, baada ya mwanamke kukoma kupata sindano hizi, huchukua muda kabla ya mwili wake kurudi kawaida. Na kuanza kuovuleti kila mwezi. Huenda ikachukua hadi miezi 10 kabla ya mwili kurudi kawaida. Na vipindi vyako vitarudi kati ya miezi ya kwanza 12 hadi 18. Mbinu hii ya kudhibiti uzalishaji haishauriwi kwa wanawake ambao hawajapata watoto kwani huenda ika athiri uwezo wako wa kuzaa.

IUD (intrauterine device)

Unapo toa IUD, kuna uwezekano wa kutunga mimba punde tu unapo tolewa. Wanawake huanza kuovuleti baada ya wiki moja na kutunga mimba kati ya mwaka wa kwanza baada ya kutolewa.

Baada ya kukoma kutumia mbinu tofauti za uzalishaji, utachukua muda kabla ya kupata vipindi vyako vya hedhi. Hasa mbinu zilizo na homoni. Kuna uwezekano wa mama kutunga mimba kabla ya kushuhudia vipindi vyake vya hedhi.

Hitimisho

Ikiwa lengo lako ni kupata mimba baada ya kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji, ni vyema kuhakikisha kuwa una ongea na daktari wako kabla ya kuanza juhudi za kutunga mimba. Kuna sababu nyingi zinazo athiri uwezo wako wa kupata mimba baada ya kukoma kutumia mbinu za uzalishaji. Kama vile umri wako, uzito wa mwili, afya yako na historia ya afya yako. Mwaka ukipita kama bado unajaribu kupata mimba bila kufanikiwa hata baada ya kukoma kutumia mbinu zozote za uzalishaji, ni vyema kumtembelea daktari wako.

Soma piaNjia 8 Mwili Wako Una Dhihirisha Kuwa Una Uzalishaji Bora!

Written by

Risper Nyakio