Baada ya kusherehekea sherehe ya kufikisha umri 35, Halima alijazwa na wasiwasi mwingi. Saa yake ya kibiolojia ilikuwa inazidi kupita, hakuwa na uhakika iwapo angeweza kupata watoto watatu kama ilivyokuwa kusudi lake. Je, naweza kupata mtoto wa pili punde tu baada ya kujifungua wa kwanza? Hakufahamu cha kufanya. Sawa na Halima, kuna wanawake wengi wanaokuwa na shaka kuhusu kupata mimba baada ya kujifungua. Kuna hatari? Je, ni salama? Makala haya yana zungumzia kuhusu kushika mimba punde tu baada ya kujifungua.
Kupata mtoto baada ya kujifungua

Wanawake wengi wana amini kuwa kunyonyesha mtoto baada ya kujifungua kuna linda dhidi ya kupata mimba. Ni vyema kukumbuka kuwa, kunyonyesha kama njia ya kupanga uzazi kuna faulu pale ambapo mama ananyonyesha pekee na kwa muda zaidi. Kumlisha mtoto baada ya kila masaa manne, na masaa sita wakati wa usiku. Ikiwa mama ananyonyesha kwa mara chache kwa siku, nafasi za kupata mimba ziko juu.
Rutuba ya mwanamke baada ya kujifungua
Mama anayenyonyesha huchukua muda kabla ya hedhi zake kurudi. Katika kisa kama hiki, ako salama kutoshika mimba tena. Ila, hedhi yake inaporudi baada ya miezi michache, anaweza kupata mimba wakati wowote. Ikiwa mama hanyonyeshi, kupevuka kwa yai hurejea baada ya wiki sita. Hata hivyo, miili ya wanawake hutofautiana.
Kupata mtoto mwingine baada ya kujifungua

Kulingana na Idara ya Afya Na Huduma za Binadamu nchini Umarekani, mama anastahili kungoja kwa kipindi cha angalau miezi 12 kabla ya kushika mimba baada ya kujifungua. Kulingana na utafiti, mwanamke anapopata mimba kwa kipindi kifupi kuliko miezi 12, ako katika hatari ya kujifungua mtoto ambaye hajakomaa. Ama kujifungua mtoto aliye na uzani wa chini zaidi. Hasa muda chini ya miezi sita. Kungoja kipindi kirefu sana zaidi ya miaka sita kabla ya kupata mtoto mwingine kuna athari hasi kwa mama na mtoto.
Wanawake wengi huchukua muda kabla ya kupevuka kwa yai kurejea baada ya kujifungua, kwa kawaida wiki sita. Kipindi cha hedhi hutofautiana kati ya wanawake. Rutuba ya mama baada ya kujifungua huathiriwa na kunyonyesha, lishe, iwapo alikuwa anavuta sigara ama mbinu za kupanga uzazi anazotumia.
Mama anayepanga kupata mtoto baada ya kujifungua anashauriwa kuzungumza na daktari wake. Atamweleza iwapo ni salama kufanya hivyo na jinsi ya kuhakikisha kuwa ana ujauzito salama.
Soma Pia: Vyanzo Vikuu Vya Kuvuja Damu Katika Ujauzito