Kuwa mzazi huanza na kupata mimba na huwa jambo la kusisimua. Ujauzito katika umri wowote ule huambatana na changamoto zake. Ikiwa una mimba baada ya miaka 40, matatizo haya huja na hatari ya juu. Hata hivyo, nambari ya wanawake wanaopata mimba baada ya miaka 40 imeongezeka.
Kitu hasa ni kumaliza kupata watoto katika umri wa miaka 35. Hii ni kwa sababu mwanamke aliye na miaka zaidi ya 35 huwa na uzalishaji uliopunguka kufuatia nambari ya mayai iliyopunguka ya kurutubisha. Baadhi ya mayai yake huenda yakawa hayana rutuba, ama ovari zake zikakosa kuziachilia vyema ama kwa wakati. Pia kuna nafasi iliyo ongezeka ya kuharibika kwa mimba unapozidi kuzeeka. Na nafasi ya juu ya kupata matatizo ya afya ambayo yanaweza kuathiri uzalishaji wako. Madaktari huangazia mambo haya unapopata mimba baada ya miaka 40 ama katika umri uliozidi.
Vitu Ambavyo Daktari Wako Huangalia Katika Mimba Baada Ya Miaka 40

- Shinikizo la juu la damu
- Pre eclampsia
- Kisukari cha gestational
- Kasoro za kuzaliwa
- Kuharibika kwa mimba
- Uzani wa chini
- Mimba ya ectopic
Inakuwa rahisi, shukrani kwa teknolojia
Maendeleo ya kiteknolojia katika matibabu imefanya iwe rahisi kupata mimba na kujifungua katika miaka ya 40, hata kama bado inafikirwa kuwa hatari ya juu. Kupata mimba katika miaka ya 40 kunaweza ongeza maumivu utakayo hisi, kwani mifupa inaanza kupoteza mass kufuatia umri. Uchovu unaohusika na mimba pia unazidi na kujifungua kupitia kwa uke kuna nafasi ya chini katika miaka ya 40's. Kujifungua mara nyingi kutakuwa kufuatia upasuaji wa c-section, kuhakikisha kuwa mama na mtoto wako salama. Ikiwa mtoto atazaliwa kufuatia njia ya uke, huenda kukawa na matatizo zaidi kufuatia umri kwani uchungu wa uzazi ni mwingi zaidi. Kuna nafasi ya juu ya mtoto kuzaliwa kama ameaga. Hata hivyo, wanawake wengi wameweza kutunga mimba na kupata watoto wenye afya katika umri wa miaka 40.
Tembelea mtaalum wa uzalishaji

Kutunga mimba huenda kukachukua muda haijalishi umri. Ikiwa una umri zaidi ya miaka 40 na hujaweza kutunga mimba kwa ufanisi, ni vyema kuwasiliana na mtaalum wa afya.
Kupata mimba katika miaka ya 40 kunaweza chukua muda zaidi kwa baadhi ya wanawake ikilinganishwa na wengine. Daktari wako wa uzalishaji anastahili kufanya kazi nawe kujua hali yako. Kwa sababu uwezo wa kujifungua hupunguka kwa kasi katika miaka ya 40's. Ikiwa unatatizika kujifungua kwa kawaida, ni vyema kuamua iwapo uko tayari kufanya majaribio kadhaa na matibabu ya uzalishaji na iwapo una njia ya kulipa kwani huwa na gharama ya juu.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Njia Bora Zaidi Za Kudhibiti Uzalishaji Kwa Mama Anaye Nyonyesha