Kuna Uwezekano Wa Mama Kupata Mimba Katika Umri Wa Ugumba?

Kuna Uwezekano Wa Mama Kupata Mimba Katika Umri Wa Ugumba?

Baada ya umri wa miaka 35, hatari za matatizo fulani huongezeka ikilinganishwa na wanawake wenye umri mdogo.

Unapo ingia katika umri wa ugumba, huenda ukawa na maswali mengi. Kama vile kushangaa iwapo mama anaweza tunga mimba katika ugumba. Ni swali nzuri, kwa sababu jibu lita athiri mbinu za upangaji uzazi utakazo amua kutumia. Ni muhimu kwa mama kuelewa msimu huu wa maisha yake na kama kuna uwezekano wa kupata mimba katika umri wa ugumba.

Ishara maarufu za kipindi hiki ni kuhisi joto jingi mwilini na vipindi vya hedhi visivyo dhabiti. Sio maana kuwa hauwezi tunga mimba. Ina maana kuwa una uwezo wa kutunga mimba, ila kwa nafasi chache zaidi na pia hauna rutuba kama hapo awali. Unapo enda mwaka mzima bila kushuhudia vipindi vyako vya hedhi, ndipo unaweza kuwa na uhakika kuwa umeingia katika umri wa ugumba. Na katika kipindi hiki, sio rahisi kwa mama kutunga mimba bila usaidizi wa teknolojia mpya za uzalishaji.

Kupata mimba katika ugumba

kupata mimba katika ugumba

Kabla ya ugumba

Huu ni wakati ambapo mabadiliko yanaanza kufanyika mwilini mwako. Ovari za mwanamke zinatoa homoni chache za estrogen na progesterone, huku viwango vya FSH na LH vikipanda. Kufuatia mabadiliko ya viwango vyako vya homoni, utaanza kushuhudia ishara tofauti mwilini kama vile kutoa jasho jingi mwilini ama kuhisi joto kwa wingi. Pia, vipindi vyako vya hedhi vitaanza kupotea ama kuto kuwa na wakati dhabiti. Kwa sababu bado unapata vipindi vyako vya hedhi, ni vyema kuhakikisha kuwa unatumia mbinu mojawapo ya kudhibiti uzalishaji.

Ugumba

Ikiwa imekuwa mwaka mzima kabla ulipo shuhudia vipindi vyako vya hedhi, bila shaka umefikisha ugumba. Huenda ikawa ni umri kati ya miaka 40 na 55. Katika umri huu, mwanamke ana kosa kuovulate tena na viwango vya homoni za estrogen na progesterone zinashuka.

Umri baada ya ugumba

Katika umri huu, viwango vyako vya homoni sio sawa kwa mchakato wa kutunga mimba ama kubeba mimba. Na sio lazima kwa mama kutumia mbinu za kudhibiti uzalishaji.

Matibabu ya Invitro Fertilization (IVF) baada ya umri wa ugumba

Mayai ya mwanamke baada ya umri wa ugumba hayana uhai. Lakini una hiari ya kutumia mayai uliyo kuwa umehifadhi ama kununua mayai. Utahitaji matibabu ya kihomoni ili kuutayarisha mwili wako kutunga mimba na kubeba mimba hadi ikomae.

Hatari za kiafya za ujauzito ukiwa na umri mkubwa

kupata mimba katika ugumba

Hatari za kiafya za mimba huongeza japo mwanamke anavyo zidi kuzeeka. Baada ya umri wa miaka 35, hatari za matatizo fulani huongezeka ikilinganishwa na wanawake wenye umri mdogo. Kama vile:

  • Kujifungua watoto zaidi ya mmoja, na mama huenda akajifungua kabla ya wakati. Nafasi kubwa ni kuwa watoto hawa watazaliwa kabla ya wakati na huenda wakawa na matatizo ya kiafya
  • Mimba kuharibika ama kifo cha mtoto kabla ya kuzaliwa
  • Kisukari cha gestational na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto
  • Kujifungua kupitia upasuaji wa C-section
  • Kujifungua mtoto kabla ya wakati na mwenye uzani mdogo
  • Shinikizo la juu la damu

Ni kawaida kwa wanawake wenye umri zaidi kuwa na matatizo ya kiafya ambayo huenda yaka athiri kutunga mimba kwao, safari ya mimba na hata kujifungua.

Hitimisho

Kuna uwezekano wa mama kuwa na uwezo wa kubeba mimba hadi ikomae lakini kwa kupitia matibabu ya homoni, na IVF. Kumbuka kuwa sio rahisi na kuna hatari zake. Ni vyema kuwasiliana na daktari anaye husika na uzalishaji akushauri kuhusu mambo muhimu unayo hitajika kufanya na kufahamu.

Chanzo: healthline

Soma PiaJinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba

Written by

Risper Nyakio