Kupata Mimba Ukiwa Na Uzito Mwingi Kuna Athari Zipi?

Kupata Mimba Ukiwa Na Uzito Mwingi Kuna Athari Zipi?

Kupata mimba ukiwa na uzito mwingi kuna athari hasi kwa ujauzito wako na huenda kuka ibua matatizo kwa safari yako ya mimba.

Kupata mimba ukiwa na uzito mwingi kuna athari hasi kwa ujauzito wako na huenda kuka ibua matatizo kwa safari yako ya mimba. Matatizo kama vile:

  • Shinikizo la damu katika ujauzito. Hili lisipo tatuliwa mapema, huenda lika sababisha matatizo makubwa kwa mama ama hata mama kuugua hali ya kifafa.
  • Mama mwenye uzani mwingi ako katika hatari kubwa zaidi ya kupasuliwa wakati wa kujifungua.
  • Mama anapo kuwa na uzani wa juu, huenda akaugua kisukari.  Na mtoto anaye zaliwa pia huenda akawa na hali hii. Mtoto mkubwa anamweka mama katika hatari ya kupasuliwa wakati wa kujifungua.

Mtoto anaye zaliwa kwa mwanamke mnene ako katika hatari ya:

mimba ukiwa na uzito mwingi

  • Kuwa na matatizo ya mfumo wa neva
  • Matatizo ya mtima
  • Kuwa mnene anapo kua
  • Kiwango kidogo cha sukari mwilini

Madaktari wana mshauri mama kuanza kuitunza afya yake mara tu anapo gundua kuwa angependa kutunga mama. Kuangazia lishe yake na kufanya mazoezi. Anapo kuwa na afya inayo faa, hata tizika sana katika safari yake ya ujauzito na pia anapo jifungua. Ni kawaida kwa mama kuhisi uchovu katika mimba na hata miguu kufura kufuatia uzito zaidi unao shinikiza viungo vya mwili kama miguu. Unapokuwa na uzito mwingi, uchovu huu utakuwa zaidi.

Kutembea kutakutatiza, kwani una uzito wako na wa mwanao na huenda ukalemewa kufanya vitu vingi mapema katika safari yako ya ujauzito. Hata kama utahisi hamu ya kula vyakula vingi na tofauti katika mimba, ni vyema kujaribu kula vyakula vyenye afya. Na vitakavyo isaidia afya yako na ya mtoto na kuhakikisha kuwa anapata virutubisho tosha na vinavyo faa.

Fanya kazi na mtaalum wa mazoezi ili akushauri mazoezi sawa ya kufanya unapokuwa na mimba. Kuna uwezekano wa kupunguza uzani ungali ukiwa katika safari yako ya mimba. Lakini kuwa makini kwani kuna aina tofauti za mazoezi ambayo sio salama kwa mtoto katika kipindi hiki.

Mama anapokuwa na uzani mdogo, kuna athari kwa mtoto pia.

kujifungua kwa urahisi

Mtoto aliye zaliwa kwa mama mwenye uzani mdogo, ako katika hatari ya:

  • Kuzaliwa kabla ya wakati. Huenda akazaliwa katika ama kabla ya wiki 37 kufika
  • Kujifungua mtoto aliye na uzito wa chini. Kiwango chini ya kilo 2.5

Mtoto anaye zaliwa akiwa na uzito mdogo huenda akawa na matatizo ya kiafya kama vile kutatizika kupumua, ama hata kubaki kwa kitengo spesheli kwa kipindi hadi wiki 2. Mtoto huyu huenda akatatizika kuongeza uzito baadaye maishani mwake.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Wakati 5 Unapo Paswa Kufanya Kipimo Cha Mimba

Written by

Risper Nyakio