Mwanamke Ako Katika Hatari Gani Anapo Jifungua Na Miaka Zaidi Ya 35

Mwanamke Ako Katika Hatari Gani Anapo Jifungua Na Miaka Zaidi Ya 35

Mwanamke mwenye afya bora hata tazika kupata mimba. Ni vyema kuwa mwangalifu wa afya yako ya kiakili, kihisia na kifizikia.

Kwa sasa huenda ukawa umesikia kuhusu saa ya bailojia kwa wanawake. Hili ni jambo ambalo limezungumziwa kwa sana. Mwanamke anapo fikisha umri wa miaka 35, mayai mwilini hutatiza kupevuka. Ubora na afya ya mayai huanza kudidimia na idadi ya mayai yenye afya na uwezo wa kupevuka huwa ndogo ikilinganishwa na mayai ya hapo awali. Na uwezo wake wa kupata mtoto baada ya miaka 35 hupunguka.

Katika miaka hii, mzunguko wa hedhi hubadilika na mayai haya pevuki kwa wakati unaofaa. Kufuatia teknolojia inayo zidi kuibuka kila siku, kuna uwezo wa kuongeza ubora wa mayai, ila ni vigumu kuongeza idadi ya mayai. Lakini shukrani kwa teknolojia, mayai yanaweza kuvunwa na kuhifadhiwa hadi pale ambapo mwanamke atafanya uamuzi wa kupata mimba.

Kwa nini kupata mtoto baada ya miaka 35 kuna tatiza

kupata mtoto baada ya miaka 35

  • Huenda mama akawa na ugonjwa wa endometriosis
  • Kupungua kwa uteute unao toka kwa mlango wa kizazi ama cervix
  • Ongezeko la hatari ya kuugua magonjwa sugu
  • Kuvimba kwa ovari ama fuko la uzazi

Kadri umri wa mwanamke unavyo zidi kuongezeka ndivyo nafasi za tumbo kuharibika zinavyo zidi. Asilimia ya mimba kuharibika kwa wanawake wenye umri huu huwa hadi 21-35.

Jinsi ya kuongeza nafasi za mama kupata mimba baada ya umri wa miaka 35

Hata kama ni jambo linalo watatiza wanawake, sio kumaanisha kuwa mwanamke hawezi jifungua baada ya kufikisha umri wa miaka 35. Kufuatia teknolojia katika nyanja ya afya. Mama anaweza boresha nafasi zake za kutunga mimba. Tazama baadhi ya njia za kutimiza hili.

  • Kuwa na subira

kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi

Bila shaka wanawake wenye umri zaidi huchukua muda zaidi kutunga mimba. Ikilinganishwa na wanawake walio katika miaka yao ya 20' ambao hawatatiziki sana kutunga mimba, walio katika miaka zaidi ya 35 watachukua muda zaidi. Kwa hivyo ni vyema kuwa na subira. Huenda ikachukua kati ya mwaka mmoja hadi miwili kufanikiwa.

  • Kuwa mwangalifu wa afya yako

Mwanamke mwenye afya bora hata tazika kupata mimba. Ni vyema kuwa mwangalifu wa afya yako ya kiakili, kihisia na kifizikia. Punguza ama utupilie mbali utumiaji wa vileo, sigara na dawa za kulevya.

Mbali na hayo, hakikisha kuwa unawasiliana na daktari aliye katika nyanja ya uzalishaji. Ili upate vipimo vinavyo faa mara kwa mara.

Soma PiaChanzo Cha Kusongwa Na Mawazo Baada Ya Kujifungua Na Suluhu Lake!

Written by

Risper Nyakio