Mambo Ya Kufanya Ili Upate Mtoto Wa Kike Mrembo

Mambo Ya Kufanya Ili Upate Mtoto Wa Kike Mrembo

Kuna mbinu nyingi za kupata mtoto wa kiume, ila mitindo hii itakusaidia kujifungua mtoto mrembo wa kike.

Je, ungependa kupata mtoto wa kike? Una mmoja tayari wa kiume na ungependa kuwa na jinsia zote mbili kabla ya kufunga kurasa ya kupata watoto? Kuna hadithi nyingi kuhusu kuongeza nafasi zako za kupata mtoto wa kike ama hata wa kiume. Baadhi ya hadithi hizi huwa za kweli na zingine huwa za kususiwa. Kuna habari za kisayansi kuhusu kuongeza nafasi zako za kutunga mimba ya mtoto wa kike. Nafasi zako za kutunga mimba ya mtoto wa kiume ama wa kike huwa karibia sawa.

kupata mtoto wa kike

Vidokezo vya kutunga mimba ya mtoto wa kike

 • Fanya ngono kila siku kutoka siku ambayo unamaliza kipindi chako cha hedhi hadi siku 2 hadi 4 kabla ya siku yako ya ovulation.
 • Kuwa na chati ya ovulation ili ujue siku unayo ovulate.
 • Mtindo wa missionary ni bora zaidi mnapo fanya ngono.
 • Kula vyakula vya asidi kama vile mboga za kijani, nafaka, nyama na blueberries.

kupata mtoto wa kike

 • Usingoja hadi dakika ya mwisho ili uanze kufanya mapenzi, anza mapema ili kuongeza nafasi zako za kupata mtoto wa kike.
 • Wanandoa ambao wanataka kupata mtoto wa kike wanashauriwa
 • Kuepuka kufanya ngono wakati wanapo ovulate ama siku chache baada ya siku hiyo. Kwani ina egemeza mwendo wa pole pole wa chromosome X.
 • Kamasi inayo tolewa unapo ovulate huwa na asidi na ina saidia katika kutunga mimba ya kike. Ni vyema kujua kuwa lishe yako ina saidia pakuu katika mafanikio ya takwa hili lako. Ili kuongeza nafasi zako za kujifungua msichana, hakikisha kuwa unakula vyakula vifuatavyo.

Mboga za majani ya kijani. Kulingana na watafiti, mboga hizi zina asidi ambayo ina saidia katika kutunga mimba ya msichana.

Mambo Ya Kufanya Ili Upate Mtoto Wa Kike Mrembo

 • Kula nafaka nzima (whole grains) kama vile nafaka, mchele ama mkate.
 • Kula nyama ila kuwa makini usikule viwango vingi.
 • Switi na chokleti.
 • Epuka kula njugu na almonds.
 • Kula vyakula vilivyo na wingi wa magnesium kama vile samaki, matunda na nafaka.

Hata kama sayansi ina unga mkono vidokezo tulivyo orodhesha kuhusu kutunga mimba ya mtoto wa kike, ni vyema kukumbuka kuwa Mungu ndiye mpaji. Ukikosa kupata mtoto wa kike, usikate tamaa, endelea kujaribu.

 

Soma pia: Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo

Written by

Risper Nyakio