Koma Kufanya Mambo Haya Usiku Ili Uweze Kulala Kwa Urahisi

Koma Kufanya Mambo Haya Usiku Ili Uweze Kulala Kwa Urahisi

Kwa wazazi wengi, kupata usingizi mwanana kwa urahisi huenda likawa ni jambo la kale. Lakini kuna njia za kufanya hivi kuwe rahisi zaidi. Anza kwa kuweka tabia hizi mbali.

Jinsi ya kupata usingizi kwa urahisi usiku

  1. Kufanya mazoezi kabla ya kulala

Koma Kufanya Mambo Haya Usiku Ili Uweze Kulala Kwa Urahisi

Hata kama ni kawaida kudhania kuwa mazoezi yata pumzisha ama kuchokesha misuli yako, huwa na athari tofauti. Unapo fanya mazoezi ya kifizikia, mpigo wa moyo huongezeka na adrenaline kuzidi mwilini wako. Na kufanya iwe vigumu kuutuliza mwili wako.

Unacho weza kujaribu ni kujinyoosha kabla ya kulala na unapo amka. Wakati wa usiku, kujinyoosha kabla ya kugeuka hupumzisha misuli na kuboresha nishati yako asubuhi.

2. Kuangalia simu yako kabla ya kulala

Wengi wetu tuna uraibu wa kufanya hivi. Wakati wote tuko kwenye simu tuki angalia yanayo tendeka na kuongea na marafiki zetu tuki ngoja kulala. Lakini kuangalia akaunti zako za mtandao na kucheza michezo ya simu hakusaidii kutuliza akili yako. Mwangaza unao toka kwenye simu yako una punguza homoni ya melatonin. Ambayo jukumu lake ni kukusaidia kulala. Kulingana na wataalum, unapaswa kuzima bidhaa zote za kielektroniki dakika 30 kabla ya kulala.

3. Kuoga na maji moto

kupata usingizi kwa urahisi

Hata kama kuoga na maji moto kuna saidia kutuliza misuli yako na kupunguza mkazo, kufanya hivi hakukusaidii kulala. Wakati wa kulala, mwili wako unahitaji kuwa na temprecha sawa kuboresha kupumzika na kulala. Baada ya kuoga na maji moto, unaweza jaribu kujituliza na maji baridi na kukusaidia kulala vyema.

4. Kutokuwa na wakati maalum wa kulala

Wakati wa kulala sio wa watoto pekee. Hata mama na baba wanahitaji kuwa na ratiba ya kulala ili kuwa na utaratibu wenye afya wa kulala. Kulala zaidi usiku mmoja kulipizia kulala masaa machache usiku uliopita kuta kuathiri sana. Utalala vyema zaidi ukiwa na wakati maalum wa kulala na ratiba unayo ifuata kwa sababu una ufunza mwili wako kulala wakati maalum kila usiku.

Ni matumaini yetu kuwa makala haya yana rahisha mambo kwa wazazi wanao tatizika kulala! Je, ulitupilia mbali tabia zozote ili kutatua tatizo lako la kuto lala ama kutatizika kupata usingizi? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!

Soma PiaUlezi Wa Usiku Kwa Watoto: Mbadala Wa Kuwafunza Kulala Wakati Wa Usiku

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio