Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

Kupevuka Kwa Yai Huanza Lini Kwa Mwanamke?

Ikiwa una fanya juhudi kutunga mimba, ni muhimu kwako kuji elimisha kuhusu kupevuka kwa yai. Maarifa haya ni muhimu kwa watu wanao epuka kupata mimba.

Kuelewa mzunguko wa hedhi kunaweza kusaidia iwapo ungependa kutunga mimba na wakati unapo taka kuepuka mimba isiyo pangwa. Ikiwa ungependa kugundua kupevuka kwa yai ni nini na wakati ambapo unaanza kwa mwanamke, uko kwa njia sawa ya kudhibiti afya yako ya uzazi.

Kupevuka kwa yai ni nini?

kupevuka kwa yai ni nini

Kila mwezi, mifuko ya mayai (ovari) ya mwanamke huachilia yai lililo komaa linalo safiri kwenye mirija ya uzazi kujitayarisha kurutubishwa. Safari ya yai hilo kutoka kwa ovari kupitia kwa mirija ya uzazi kujitayarisha kurutubishwa ina fahamika kama kupevuka kwa yai (ovulation)

Kabla ya yai kutoka kwa mifuko ya mayai, kuta za uterasi zita nenepa kutayarisha kurutubisha yai na kutunga kufanyika. Ikiwa yai halita rutubishwa, kuta za uterasi zita vunjika na kutoka kupitia kwa uke pamoja na damu- mchakato unao fahamika kama hedhi.

Kupevuka kwa yai huanza lini?

Kuna uwezekano wa kufahamu utakapo ovulati unapo fahamu jinsi ya kuhesabu mzunguko wako wa hedhi. Mzunguko wa mwanamke huanza siku ya kwanza anapo pata hedhi yake na kuisha siku ya kwanza ya kipindi kijacho cha hedhi. Huku kuna maana kuwa mzunguko wako huanza siku hedhi yako inapo anza na kuisha siku unapo pata kipindi chako kinacho fuata.

Kwa kawaida, wanawake wengi huwa na mizunguko ya hedhi ya muda wa siku kati ya 27-32. Walakini, kuna wanawake ambao wana mizunguko mirefu ama mifupi zaidi.

Njia tofauti za kuhesabu siku zenye rutuba kujua kupevuka kwa yai kunapo anza

Kupevuka kwa yai kunajulikana kama kipindi chenye rutuba. Katika kipindi hiki, kuna nafasi za juu za kupata mimba mwanamke anapo jihusisha katika ngono isiyo salama.

  • Kwa wanawake wengi, kupevuka kwa yai hufanyika kati ya siku 11 na 21 ya mzunguko wao wa hedhi. Ili kupata nambari iliyo sawa, hesabu siku 11 kutoka siku ya kwanza ya kipindi chako cha hedhi na utapata kuwa kipindi chako chenye rutuba huwa kati ya kipindi hicho na siku ya 21
  • Pia unaweza tabiri kupevuka kwa yai na siku zenye rutuba kwa kuhesabu siku 12-16 kabla ya kuanza kwa kipindi kijacho cha hedhi

Kuelewa fezi/hatua za kipindi cha hedhi na kupevuka kwa yai kunapo anza

kupevuka kwa yai ni nini

Kujibu swali la kupevuka kwa yai huanza lini, utahitajika kuelewa hatua za kipindi cha hedhi.

Hizi ni:

Fezi ya Follicular

Fezi ya ovulation

Fezi ya luteal

  • Fezi ya follicular

Fezi ya follicular huanza siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi na inaweza dumu hadi siku ya 11-21. Katika fezi hii, tezi ya pituitary hutoa FSH(follicle stimulating hormone). Homoni hii huchechemua mifuko ya mayai kutoa follicles, hadi 20 na kila moja huhifadhi yai. Mwishowe, follicles zote hufa isipokuwa moja itakayo komaa na kuwa yai lililo iva.

Katika fezi hii, kuta za uterasi ama endometrium hunenepa kujitayarisha kurutubishwa na ujauzito.

  • Fezi ya kupevuka kwa yai ovulation

Kupevuka kwa yai hufanyika yai lililo iva linalo baki lina achiliwa kutoka kwa mifuko ya mayai. Mara nyingi, kupevuka kwa yai huanza wiki 2(siku 14) kabla kipindi kijacho- ikiwa hedhi yako ni ya kawaida. Katika fezi ya ovulation, tezi ya pituitary hutoa viwango vya juu vya homoni ya luteinizing (LH).

Yai lililo iva linatolewa kutoka kwa mirija ya mayai na yai huishi kwa muda wa masaa 24. Ikiwa hakuna manii ya kurutubisha yai, lina kufa baada ya siku moja. Kupevuka kwa yai ni wakati muhimu kwa ujauzito na kutunga na kufahamu kupevuka kwa yai kuna anza lini ni muhimu sana kwa wanawake wanao taka kudhibiti afya yao ya uzazi.

  • Fezi ya luteal

Fezi ya luteal huanza mwisho wa kupevuka kwa yai na kuisha siku unapo pata kipindi chako kinacho fuata cha hedhi. Baada ya kupevuka kwa yai kumefanyika, corpus luteum, hushikilia yai lililo iva, kuachana na kutoa homoni ya progesterone.

Homoni hii husaidia kunenepesha kuta za uterasi na kutayarisha ili manii yarutubishe yai na kujipandikiza kwenye kuta hizi za uterasi.

Ikiwa kurutubishwa kunafanyika, yai hujipandikiza kwenye kuta za uterasi, kisha mwili hutoa HCG kama kuthibitisha kuwa kutunga kumetendeka. HCG ndiyo homoni unayo pima unapo fanya kipimo cha mimba.

Katika kesi ambayo hakuna kurutubishwa na mimba, corpus luteum hufa, na kusababisha utoaji wa progesterone kutolewa. Huku kuta sababisha kuta za uterasi kutoka kama hedhi.

Ikiwa una fanya juhudi kutunga mimba, ni muhimu kwako kuji elimisha kuhusu kupevuka kwa yai. Maarifa haya ni muhimu kwa watu wanao epuka kupata mimba.

Vyanzo: Betterhealth.vic.gov

Womenshealth.gov

American Pregnancy

Soma Pia:Je, Kwa Nini Kipindi Changu Cha Hedhi Kimechelewa? Mambo Yanayo Sababisha

Written by

Risper Nyakio