Jinsi Ya Kupika Wali Wa Jollof Wenye Ladha Na Nyanya Zilizo Gandishwa

Jinsi Ya Kupika Wali Wa Jollof Wenye Ladha Na Nyanya Zilizo Gandishwa

Iwapo nyanya zako za shambani zimeisha, bado unaweza pika wali wako wa jollof kwa kutumia nyanya zilizo gandishwa. Nyanya mbichi kama vyakula vingine Nigeria visivyo kawia muda mrefu ni zawadi ya muda, kwa hivyo ni nadra na za bei ghali katika vipindi tofauti mwakani. Kwa hivyo, kujua jinsi ya kupika wali wako wa jollof na nyanya zilizo gandishwa ni uhodari ambao utasaidia wakati wote.

Jinsi ya kupika wali wa jollof Na nyanya zilizo gandishwa

cooking jollof rice

Picha: Unsplash

Ili kutoa ladha ya kuganda kutoka kwa nyanya zilizo gandishwa, lazima ukaange nyanya zako vyema ama uzisiage kwa kutumia kifaa cha kusiaga na uweke pilipili na kitunguu. Vitunguu hivi vinafanya kazi kupunguza baadhi ya ladha ya kuganda. Ni unge tupike!

       Viungo

 • Vikombe 5 vya mchele
 • 2 na 1/2 kilo za kuku
 • 1 kopo la nyanya zilizo gandishwa  (300 grams) Huenda zikawa nyingi kabla ya kusiaga

tin tomatoes in Nigeria

 • 3 vitunguu vikubwa
 • 3 vikombe vya pilipili mbichi (kuongeza ladha)
 • Mafuta ya kukaanga
 • Viungo vya kuongeza ladha kwenye kuku inayo chemka
 • 1 pilipili ya rangi ya kinjano
 • 1 pilipili ya rangi nyekundu
 • 1 pilipili ya kijani
 • 1 kipande cha kitunguu saumu
 • 2 vijiko vya tangawizi iliyo waviwa
 • ½ kijiko cha thyme iliyo kaushwa
 • 2 vijiko vya viungo vilivyo changanywa
 • ½ kijiko cha mbaazi
 • 3 karoti kubwa zilizo safishwa

 

Jollof Rice with Stew

Chanzo cha picha: Noahalorwu / CC BY-SA

Maagizo

 • Siagi chombo chako cha nyanya na pilipili na kitunguu.
 • Kaanga kitunguu chako kilicho katwa, hoho nyekundu, chembe za ladha, hoho za kijani na hoho za kinjano kwenye mafuta hadi zipate harufu ya kupendeza.
 • Kisha uongeze nyanya zilizo siagwa na uchanganye hadi uone kuna mtengano kati ya mafuta na nyanya.
 • Ongeze kuku wako kisha uchanganye, kisha uonje kidogo kupima kiwango cha chumvi na iwapo unahitaji kuongeza.
 • Ongeza mchele ulio oshwa na iwapo bado unaonekana juu ya viungo vingine, ongeza kiwango cha maji. Kisha ongeza thyme, kiungo cha jollof kisha uongeze tawi la bay na uwache chungu chako kitokote. Kinapo anza kutokota, punguza moto na uwache mchele upike hadi uive.
 • Baada ya maji kwenye chungu kukauka, unaweza ongeza karoti na mbaazi na hoho za kijani, na ukoroge na ufunike zikauke. Kwa njia hii karoti na mbaazi zitapikika vya kutosha kiwango cha kulika.

Chakula hiki cha kuvutia huenda kika pakuliwa kwa moin-moin, ndizi zilizo kaangwa na kinywaji baridi.

Soma Pia: No Eggs, Milk, Or Butter? Here Are Things You Can Still Bake

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio