Mbinu Ya Kupima Mimba Kutumia Baking Soda Ni Ya Kuaminika Ama La?

Mbinu Ya Kupima Mimba Kutumia Baking Soda Ni Ya Kuaminika Ama La?

Kuna njia nyingi za kitamaduni ambazo zinakusaidia kujua jinsia ya mtoto unaye tarajia ikiwa ni mvulana ama msichana kama vile kipimo cha kupima mimba kutumia baking soda

Punde tu unapo anza kushuku kuwa huenda ukawa na mimba, ni asili kuwa na hamu ya kuhakikisha kuwa kwa kweli una mimba na pia kufahamu jinsia ya mtoto unaye tarajia. Huku ukingoja fetusi yako ikue kiwango tosha ili uweze kufanyiwa ultrasound, ya kuthibitisha jinsia yake, unaweza fanya kipimo cha kupima mimba kutumia baking soda ukiwa nyumbani kutosheleza hamu yako. Soma zaidi upate maarifa zaidi.

Habari za mimba ni mojawapo ya wakati wa furaha nyingi zaidi kwa wanandoa wengi, hasa ikiwa wamekuwa wakijaribu kutunga mimba kwa wakati mrefu. Haijalishi kama wewe ni mzazi wa mara ya kwanza ama mwenye uraibu, furaha ya kuwa na mtoto inapiku changamoto zinazo kuja na kupata mtoto. Katika kipindi hiki, mamia ya maswali yana jaa kwenye akili ya wanandoa wanao tarajia, kama vile, jinsia ya mtoto wanaye tarajia.

Kuna njia nyingi za kitamaduni ambazo zinakusaidia kujua jinsia ya mtoto unaye tarajia ikiwa ni mvulana ama msichana kama vile kipimo cha kupima mimba kutumia baking soda. Kipimo hiki rahisi na cha bei nafuu kina kusaidia kufahamu jinsia ya mtoto unaye tarajia kwa kutumia poda ya kuoka na kontena safi.

Jinsi Inavyo Fanyika

Mbinu Ya Kupima Mimba Kutumia Baking Soda Ni Ya Kuaminika Ama La?

Kipimo cha kupima mimba kutumia baking soda ni rahisi kufanya ukiwa peke yako. Yote unayo hitaji ni kontena ndogo na safi kuokota mkojo wako na kiwango kidogo cha baking soda kutoka jikoni. Ili kufanya kipimo, chukua mkojo wako, unashauriwa kutumia mkojo wa kwanza wa siku unapo amka kabla ya kunywa maji ama kiamsha kinywa.

Baada ya kuweka mkojo kwenye chupa safi, ongeza kiwango sawa cha poda ya kuoka kwenye kontena hiyo. Ngoja kwa muda mfupi huku ukiangalia kitakacho fanyika ndani ya kontena hiyo. Ikiwa utasikia sauti, ina aminika kuwa utajifungua mtoto wa kiume. Ikiwa hakutakuwa na sauti yoyote na mkojo unabaki sawa, ina aminika kuwa utajifungua mtoto wa kike.

Je, matokeo ya kipimo cha kupima mimba kutumia baking soda ni sahihi?

Kipimo hiki hakija dhibitishwa kisayansi. Matokeo sahihi huenda yakawa asilimia 50 kwa vipimo vinavyo fanyika. Poda ya kuoka hutoa sauti inapo changanyika na asidi, kwa hivyo ikiwa kwa sababu yoyote mkojo wako una asidi, utatoa sauti hiyo na huenda ukadhani kuwa una tarajia mtoto wa kiume.

Sababu ambazo huenda zikafanya mkojo wako uwe na asidi ni kama vile, lishe yako, viwango vya maji mwili, maambukizi kwenye mfumo wako wa mkojo na kadhalika. Pia aina ya vyakula unavyo kula, na kuadhiri matokeo ya kipimo chako.

Baada ya kufanya kipimo hiki cha nyumbani, unashauriwa kutembelea kituo cha afya kupata matokeo sahihi. Kwa kutumia mbinu zilizo dhibitika kisayansi.

Vyanzo: Medical News Today, Healthline

Soma Pia:Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Dawa Ya Meno

Written by

Risper Nyakio