Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Chumvi

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Chumvi

Je, umewahi tamani kujua iwapo una mimba au la kwa kasi? Kuna uwezekano unapojua jinsi ya kupima mimba kwa kutumia chumvi. Iwapo hauna wakati wa kukimbia dukani kununua kipimo cha mimba ama iwapo daktari ako mbali sana.

Je, mbona ushughulike na kipimo cha mimba cha nyumbani?

Huenda unashangaa kwa nini usitumie mbinu iliyo jaribiwa na ikafaulu ili kugundua iwapo una mimba. Kupimia nyumbani hukupatia matokeo unayo kusudia kwa usiri wa nyumbani mwako. Process hii yote huenda ya kutisha iwapo unataka kupata mtoto au la.

Kipimo cha mimba cha nyumbani kinapaswa kutosheleza hamu yako kwa kasi na kukupa jibu unalo tarajia katika mazingira uliyo yazoea-nyumbani mwako.

Mambo ya kufanya kabla ya kupima iwapo una mimba kwa kutumia chumvi

Ili kupata matokeo yaliyo sawa, unapaswa kungojea hadi mwili wako unapo anza kutoa idadi zinazo tosha za homoni ya HCG. Jambo hili litatendeka katika wiki ya kwanza baada ya kukosa hedhi zako. Kitu chochote kile kabla ya wiki ya kwanza huenda ukapata matokeo yasiyo sawa.

Matokeo yaliyo sawa yatategemea zaidi concentration ya mkojo,  inayo maanisha kuwa hupaswi kunywa maji mengi kabla ya kuchukua kipimo kile. Maji mengi yata dilute mkojo wako na kuifanya vigumu kupata matokeo yaliyo sahihi. Hili ni jambo muhimu la kuagazia iwapo unataka kujua jinsi ya kupima uja uzito kutumia chumvi.

kipimo cha mimba kutumia chumvi

Kupima mimba kutumia chumvi: Je, kipimo hiki kinafanya kazi kivipi?

Ni jambo la kawaida kushangaa jinsi kipimo hiki hufanya kazi iwapo ni mara yako ya kwanza kujua kuhusu jinsi ya kupima mimba kutumia chumvi. Huenda ukawa huna imani na mbinu hii kwa mara ya kwanza, ila ni sawa pia. The fact kuwa chumvi-kitu ambacho kila mtu anachokuwa nacho  nyumbani mwao – kinaweza fanya kama kipimo cha mimba halikai jambo la kuaminika sana. Homoni ya HCG hureact inapo patana na chumvi, na kukufahamisha iwapo una mimba au la.

Vitu unavyo hitaji vya kipimo cha nyumbani cha mimba kutumia chumvi

Habari nzuri ni kuwa huhitaji kukimbia kununua kitu chochote cha kipimo hiki. Unapo soma jinsi ya kupima mimba kutumia chumvi, unapaswa kufahamu kuwa kila kitu unachohitaji kimo jikoni mwako.

Matahitaji:

  • Saa, ya kupima wakati unaohitaji wa kipimo hiki

(Simu yako itafanya kazi njema!)

  • Mkojo wako wa kwanza- haswa wa asubuhi
  • Kikombe kilicho transparent
  • Finyo mbili za chumvi
Jinsi Ya Kupima Mimba Kutumia Chumvi

kwa kutumia chumvi kidogo, unaweza kufanyia kipimo chako cha mimba nyumbani

kupima mimba kutumia chumvi- maagizo ya kufuata

  1. Eka mkojo wako kwenye kikombe kile( kumbuka kuwa mkojo safi, mkojo wa asubuhi huwa bora zaidi)
  2. Ongeza pinch mbili za chumvi kwa kikombe kile chenye mkojo
  3. Changanya vitu hivi viwili vizuri
  4. Weka saa yako ipime hadi dakika 5 zinapopita
  5. Tazama mabadiliko
Jinsi ya Kupima Mimba Kutumia Chumvi

(Image credit: Pixabay)

Je, una mimba au la?

Iwapo utaona rangi nyeupe sawa na ile ya maziwa ikitokea, hii ni ishara kuwa una mimba. Ila mkojo ule unapo baki vilevile bila kugeuka, hauna mimba.

Nini kinacho fuata?   

Kujua jinsi ya kupima mimba kutumia chumvi ni njia ya kasi na rahisi kugundua iwapo una mimba au la. Pia hutumii pesa zozote kwani vitu vinavyo hitajika vinapatikana nyumbani. Walakini, huenda ukahitajika kupata vipimo vya damu hospitalini ili kudhibitisha matokeo yale. Vipimo vya nyumbani huenda vikawa sawa ila hakuna ushahidi ama prove ya kisayansi. Ni vizuri kwa wakati wote kupata kipimo bora cha uja uzito cha kupima ama kumtembelea daktari wako ili kupata uhakika.

Resources: NHS

Also Read: Things to add to your pregnancy shopping list

Written by

Risper Nyakio