Jinsi Ya Kutatua Uchungu Wa Nyonga Katika Mimba

Jinsi Ya Kutatua Uchungu Wa Nyonga Katika Mimba

Safari yako ya mimba inaanza baada ya kupima mimba kwa chumvi na kugundua kuwa una tarajia mtoto. Ni vyema kuhakikisha kuwa una maarifa ya safari hii.

Huenda ikawa kuwa umekuwa ukijaribu kutunga mimba kwa muda sasa. Na una furaha isiyo na kifani baada ya kufanya kipimo cha mimba cha kienyeji ama kupima mimba kwa chumvi ama kutumia njia yoyote ile ya kupima mimba na kugundua kuwa unatarajia mtoto. Hongera! Bila shaka hiki ni kipindi chenye furaha zaidi maishani mwako. 

Ni vyema uanze kujitayarisha na kufahamu mabadiliko yanayo tendeka ukiwa na mimba. Makala haya yana kufahamisha zaidi kuhusu uchungu kwenye nyonga na jinsi ya kutatua.

Uchungu kwenye nyonga(hip) ukiwa na mimba huwa mojawapo ya matatizo yanayo andamana na kupata mtoto kwa wanawake wengi. Uchungu huu huwa kiasi kidogo kwa wanawake wengi, huenda ukawa mwingi kwa wengine, na hata kuathiri utendaji kazi wao. Walakini, baadhi ya mazoezi yanaweza saidia kupunguza uchungu huu katika mimba.

Wataalum wana amini kuwa uchungu huu husababishwa na na misuli kunyooka ili kutengeneza nafasi ya mimba na mtoto anaye kua.

Vyanzo vya uchungu wa nyonga katika mimba

kupima mimba kwa chumvi

Kuna sababu nyingi ambazo huenda zika sababisha uchungu huu ukiwa na mimba. Hapa chini kuna baadhi ya vyanzo.

  • Ongezeko la uzito

Ujauzito huja na ongezeko la uzito mwilini, uzito wako na wa mtoto aliye tumboni mwako. Na uzito huu una shinikiza viungo. Shinikizo hii inapo zidi kuongezeka, huenda nyonga yako ikaanza kuuma.

Wataalum wana shauri wamama wenye mimba wawe makini na uzito wao. Kiwango cha uzito kinacho shauriwa kinalingana na uzito wako kabla ya kutunga mimba. Mara nyingi ikiwa una uzito wenye afya kabla ya mimba, kuongeza uzito wa kilo 13 hadi 18 ukiwa na mimba ni sawa.

  • Kupumzika

Ukiwa na mimba, homoni zinazo julikana kama relaxin huongezeka. Ina jukumu la kutuliza tishu zinazo unganisha mifupa mwilini wako. Na hili linaweza sababisha uchungu wa mgongo na nyonga.

  • Kuto keti wima na kulala vibaya

Kuongeza uzito huandamana na mabadiliko ya unavyo keti. Unavyo kaa kunalingana na jinsi uzito ulivyo sambaa mwilini mwako. Ikiwa uzito wa mtoto wako huegemea upande mmoja, huenda ukashuhudia uchungu wa nyonga. Pia, mtindo wako wa kulala huenda ukachangia katika uchungu wa nyonga. Kwa hivyo jaribu kulala na mto katikati ya miguu ikiwa kulala kwa mtindo mwingine unakufanya uhisi hauna starehe.

Jinsi ya kutuliza uchungu wa nyonga ukiwa na mimba

Kuna mazoezi machache ya mwanamke mwenye mimba anaye tatizika na uchungu wa nyonga. Kama vile:

how to prevent miscarriages

Kunyooka ukiwa umesimama kwa pande

Lainisha bega lako na mlango wako kisha upitishe upande wa ndani wa mguu juu ya upande wa nje na ulalie mlango. Kisha ushikilie na mikono miwili.

Mwanamke mjamzito anapaswa kukumbuka kuwa kipindi cha mimba ni nyeti na anapaswa kuwa makini sana na mazoezi anayo fanya. Una shauriwa kuwasiliana na mtaalum wa mazoezi aliye na vyeti ama mkunga ili waku shauri mazoezi yatakayo kufaa kulingana na trimesta ya mimba uliyoko.

Furaha ya safari hii haiishi baada ya kufanya kipimo cha nyumbani cha kupima mimba kwa chumvi na kugundua kuwa una mimba. La, huo ni mwanzo wa safari yako ya mimba iliyo na mengi ya kufurahikia, mengi ya kung'amua na pia ina nyakati zisizo na starehe.

Soma Pia:Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Written by

Risper Nyakio