Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Kitunguu

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Kitunguu

Kutumia kitunguu kupima mimba kunamsaidia mama kupata matokeo ya kasi bila gharama yoyote. Soma zaidi ufahamu jinsi kipimo hiki kina fanyika.

Vipimo vya nyumbani vimekuwa vikitumika kudhihirisha matokeo ya mimba kwa muda mrefu. Vipimo vya kienyeji vya mimba ni kama vile kupima mimba kwa kitunguu ama kutumia chumvi kupima mimba. Vipimo hivi vina fanya kazi kwa kudhibitisha kuwepo kwa homoni ya human chorionic gonadotropin (HCG) kwenye mkojo. Homoni hii inapatikana baada ya yai kujishikilia kwenye kuta za uterasi. Mchakato huu unafanyika siku 6-12 baada ya kupevuka kwa yai na homoni ya HCG inatolewa na seli zinazo anza kutunga placenta.

Vipimo vya nyumbani vilipata umaarufu mwaka wa 1978 hata kama vilichukua zaidi ya masaa mawili kupata matokeo. Mara nyingi vipimo hivi asili vya mimba vilikuwa na asilimia 80 sahihi ya matokeo hasi. Sasa hivi, unaweza pata matokeo sahihi siku tano kabla ya kukosa kipindi chako cha hedhi.

Kupima mimba kwa kitunguu

Kabla ya kuibuliwa kwa kifaa kinacho tumika leo kupima mimba, njia iliyo aminika ya kudhihirisha kama mwanamke alikuwa mjamzito ilikuwa kungoja  na kuona. Lakini hata kama ilikuwa vyema kushtuliwa, kugundua kama una mimba kwa njia za kale, kukosa kipindi chako cha mimba, wanawake bado walitaka kufahamu mapema ilivyo wezekana kama walikuwa wana tarajia mtoto ama la.

Kuna vipimo vingi asili vya mimba walivyo tumia. Mojawapo ya vipimo hivi ni kupima mimba kwa kutumia kitunguu.

Kipimo cha mimba kwa kutumia kitunguu kinafanyika vipi

kupima mimba kwa kitunguu

Kipimo hiki kilikuwa maarufu sana miongoni mwa wana Greeks walio kiibua. Kulingana nao, wali shauri kuwa mwanamke aliye shuku kuwa na mimba. Alihitajika kuingiza kitunguu kwenye uke wake usiku mzima. Ikiwa asubuhi alinuka kitunguu, hakuwa na mimba. Kwani uterasi yake ilikuwa wazi na harufu ya kitunguu ilipungwa juu hadi ikafika kwenye mdomo wake.

Na kama baada ya kuweka kitunguu kwenye uke wake kwa usiku mzima na asubuhi hakuwa na harufu ya kitunguu, alikuwa na mimba. Kwa sababu uterasi yake ilikuwa imefungana kwa hivyo harufu haikufika kwenye mdomo wake.

Hata kama kipimo hiki kili aminika sana siku za hapo kale, ni vyema kukumbuka kuwa hakuna utafiti wa kisayansi unao uunga mkono. Hauja dhibitika kuwa na matokeo sahihi kisayansi.

Kwa hivyo baada ya kupima mimba kwa kutumia kitunguu, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako na kufanyiwa vipimo vinavyo hitajika kudhibitisha ikiwa una mimba ama la.

Chanzo: MentalFloss

Soma Pia:Jinsi Ya Kutatua Uchungu Wa Nyonga Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio