Njia Tofauti Za Kupima Mimba Ingali Changa

Njia Tofauti Za Kupima Mimba Ingali Changa

Jinsi ya kupima mimba ukiwa nyumbani bila kutumia pesa zozote.

Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikakufanya ufanye uamuzi wa kupima mimba mara tu unapo shuku kuwa huenda ukawa na mimba. Kama ndoto yako kwa muda mrefu imekuwa kuitwa mama, utakuwa na hamu nyingi sana za kujua iwapo ndoto yako itatimia. Huenda pia ikawa kwa bahati mbaya, mbinu ya kudhibiti mimba mliyokuwa mkitumia ilienda kombo. Kwa hivyo ni vyema kudhibitisha ikiwa ume tunga mimba. Mara nyingi huenda ukataka kufanyia kipimo hiki nyumbani kabla ya kwenda kwenye zahanati. Kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia kupima mimba ukiwa nyumbani. Mojawapo ya mbinu maarufu ya kufanya kipimo cha mimba cha nyumbani ni kupitia kupima mimba kwa kutumia baking soda.

kupima mimba kutumia baking soda

Kuna faida nyingi za kupima mimba kwa kutumia baking soda. Hizi ni kama vile:

 • Unapata nafasi ama usiri wako bila mtu yeyote kujua unacho kifanya
 • Baking soda ni kiungo kilicho jikoni mwako na rahisi kupata
 • Hautumii pesa zozote kununua kifaa cha kupima mimba
 • Unatumia wakati mfupi kufanya kipimo hiki
 • Unapata matokeo ya kipimo kabla ya kuenda hospitalini

Baada ya kuangalia faida za kutumia baking soda kufanya kipimo chako cha mimba. Tuna kuelimisha jinsi ya kufanya kipimo hiki ili upate matokeo sahihi.

Mahitaji

 • Chupa safi
 • Kijiko kimoja ama viwili vya baking soda
 • Mkojo- hasa wa asubuhi punde tu baada ya kuamka kabla ya kunywa kiamsha kinywa chako

 

kupima mimba kutumia baking soda

Maagizo

 • Tia mkojo wako kwenye chupa safi na iliyo wazi ili uweze kuona kinacho tendeka
 • Ongeza baking soda kwenye chupa hiyo
 • Ikiwa una mimba, kutakua na sauti itakayo tokeo kwenye chupa hiyo 'fizzling'
 • Lakini kama hauna mimba, hakutakuwa na mabadiliko yoyote ndani ya chupa hiyo

Bado hakuna utafiti ulio fanyika kudhibitisha kipimo cha mimba cha aina hii. Unashauriwa kutembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe baada ya kupima mimba kwa kutumia baking soda ukiwa nyumbani ili kudhihirisha kipimo hicho na matokeo uliyo yapata. Ili uweze kuanzia utaratibu wa afya na utunzaji kabla ya kujifungua. 

Written by

Risper Nyakio