Vidokezo 5 Muhimu Kwa Wanawake Wanao Jaribu Kupata Mimba

Vidokezo 5 Muhimu Kwa Wanawake Wanao Jaribu Kupata Mimba

Afya ni muhimu sana kwa wanandoa wanao kusudia kupata mimba. Hakikisha kuwa unakula lishe yenye afya na kufanya mazoezi.

Ni maarifa ya kimsingi kwa kila mwanamke anaye jaribu kupata mimba kuwa anapaswa kuzingatia afya njema kama hatua ya kwanza. Ikiwa unajaribu kupata mimba, ni vyema kuepuka kujikwaza sana na fikira hizi. Baada ya kujaribu kwa muda, usi kawie kupima kuwepo kwa mimba kwa kutumia mbinu kama vile kupima mimba kwa kutumia chumvi. Mbinu hii inakupatia usiri unao hitaji kwa kutumia vifaa ulivyo navyo nyumbani mwako.

Wanawake wanapaswa kufanya nini kuongeza nafasi zao za kupata mimba?

kupoteza mimba ya wiki mbili

Ushauri mkuu wanawake wanaopatiwa wanapo kuwa kwenye safari ya kupata mimba ni, kufahamu miili yao zaidi. Hasa vipindi vyao vya hedhi. Kulingana na daktari wa afya ya uke na uspesheli wa ugumba Ellen Pavone, ana shauri wanawake kufahamu umbali wa vipindi vyao vya hedhi. Ili afanye ngono maksudi kujaribu kupata mimba.

Tuna angazia vidokezo 5 muhimu vilivyo dhibitika kuwasaidia wanawake wanao jaribu kupata mimba

  1. Rekodi unapo pata vipindi vyako vya hedhi

Mwanamke aliye na nia ya kupata mtoto anapaswa kufuatilia kwa makini hedhi yake. Kuona kama hedhi zake huanza siku sawa kila mwezi, kipindi cha aina hii kina tambulika kama cha kawaida. Ikiwa vipindi vyake huanza siku tofauti kila mwezi na umbali wa vipindi hivi sio sawa kila mwezi, kipindi cha aina hii kina fahamika kama kisicho cha kawaida. Kuna programu za rununu zinazo saidia mwanamke kufuatilia kipindi chake cha hedhi. Pia, una hiari ya kutumia kalenda. Kwa kufanya hivi, mwanamke anajua wakati ana ovulate, huu ndiyo wakati alio na uzazi zaidi na ana nafasi kubwa ya kutunga mimba.

2. Fanya ngono kila siku unapokuwa na nafasi kubwa ya uzazi

Kipindi hiki mara nyingi huwa siku sita, siku tano kabla ya kupevuka kwa yai na siku yenyewe, kulingana na utafiti ulio fanywa na American Society for Reproductive Medicine. Hizo ndizo siku ambazo mwanamke ana nafasi zaidi za kutunga mimba kila mwezi. Ikiwa una tatizika kujua siku zako ulizo na uzazi zaidi, kuna programu tofauti za simu na mtandao ambazo zinaweza kusaidia.

Utafiti umedhihirisha kuwa kuna tofauti kubwa katika nambari ya mimba kati ya wanandoa wanaofanya ngono kila siku katika 'kipindi chao cha uzazi mkubwa' (asilimia 37) ikilinganishwa na wanandoa walio fanya ngono baada ya siku moja (asilimia 33). Kwa hivyo kufanya ngono kila siku kunawasaidia wanandoa zaidi.

couple exercises

3. Hakikisha una uzito wa mwili wenye afya

Uzito wa mwili huchangia pakuu katika nafasi za mama kupata mimba. Hata kama watu wengi hupuuza jambo hili. Kuwa mzito sana kuna weza punguza nafasi za mama kutunga mimba, pia kuwa mwembamba sana huenda kukapunguza nafasi zake.

Kulingana na utafiti, mwanamke mwenye uzito zaidi anaweza chukua muda mara mbili kupata mimba ikilinganishwa na mwanamke aliye na uzito wa kawaida. Mwanamke mwembamba anaweza chukua muda hadi mara nne zaidi kutunga mimba. Kuwa na ufuta zaidi wa mwili husababisha mwili kutoa viwango vingi vya homoni ya estrogen ambayo inaweza ingiliana na kupevuka kwa yai. Kupunguza uzito wa mwili kabla ya kuanza safari ya kutunga mimba kunaweza ongeza nafasi za mwanamke kupata mimba, kulingana na American Society for Reproductive Medicine.

Utafiti zaidi ulio fanyika ulionyesha kuwa wanandoa walio na uzito mwingi wa mwili huchukua asilimia 50 ya wakati zaidi kupata mimba. Kwa hivyo jukumu la kupunguza uzito sio la mama tu, mbali la wanandoa wote wawili ili pia wapate mtoto mwenye afya mbali na kutunga mimba kwa urahisi.

Mwanamke anaye taka kuwa mjamzito ana shauriwa kuanza kufanya mazoezi ili mwili wake uwe tayari. Wataalum huwashauri wanadada kuwa ikiwa hawawezi kimbia mbio za masafa marefu, hawako tayari kupata mimba. Kwa hivyo hakikisha unafanya mazoezi.

4. Kuchukua vitamini vya utunzi wa kabla ya kujifungua

Mara nyingi, vitamini hizi huchukuliwa na wanawake walio na mimba. Na kuanza mapema wanapo gundua kuwa wana tarajia mtoto. Wataalum wa afya ya wanawake wanashauri mabinti wanao taka kutunga mimba kuanza kuchukua vitamini hizi kabla ya kupata mimba. Angalau mwezi mmoja kabla kuanza juhudi za kuwa mjamzito. Kwa njia hii, wata tambua vitamini zinazo wafaa na kuziendeleza wanapokuwa wajawazito. Ni muhimu sana katika kuepusha mtoto kupata kasoro za kuzaliwa kwenye ubongo na uti wa mgongo.

Vidokezo 5 Muhimu Kwa Wanawake Wanao Jaribu Kupata Mimba

5. Kula vyakula vyenye afya

Lishe ni muhimu sana katika safari ya wanandoa ya kuwa wajawazito. Lishe iliyo sawasishwa ina mpa mama virutubisho tosha kutayarisha mwili wake kubeba mtoto. Lishe yako inapaswa kuwa na chakula kutoka kwa vikundi vyote kama vile protini, wanga, vitamini na fiber. Matunda na mboga ni muhimu sana katika lishe yako ya kila siku.

Punguza vyakula vilivyo kaangwa kwenye ufuta mwingi kama vile vibanzi vya viazi ama viazi vitamu. Koma kunywa pombe na kuvuta sigara ikiwa una uraibu wa kutumia bidhaa hizi. Punguza kiwango cha kahawa unacho kunywa kila siku. Viwango vingi vya kahawa huenda vika athiri juhudi zako za kujaribu kupata mimba.

Hitimisho

Kuna imani nyingi zisizo za kweli kuhusu mitindo ya ngono na kupata mimba. Baadhi ya watu wanaamini kuwa mitindo maalum ya kufanya ngono huongeza nafasi za wanandoa kupata mimba. Kama vile mtindo wa mwanamke kulala kwa mgongo. Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa mwanamke kulala kwa mgongo baada ya ngono kuna fanya manii kuingia ndani ya uke wake na kuongeza nafasi zake kupata mimba. Ukianza kuona dalili za kuwa na mimba, hakikisha una mimba kwa kutumia kifaa cha kupima mimba ama kupima mimba kwa kutumia chumvi ukiwa kwa starehe zako nyumbani.

Chanzo: LiveScience

Soma Pia:Vidokezo Vya Kupata Mimba Na Vipindi Vya Hedhi Visivyo Vya Kawaida

Written by

Risper Nyakio