Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Chumvi Na Mkojo

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Chumvi Na Mkojo

Kuna njia nyingi za kupima mimba. Kipimo hiki kina tumia vitu ulivyo navyo jikoni mwako.

Je, ni vipimo gani unavyo tambua vya kukusaidia kujua hali yako ya ujauzito ukiwa nyumbani? Kabla ya kufanya kipimo chochote, ni vyema kuhakikisha kuwa ni salama kwako na kwa afya yako. Kuna njia nyingi za kupima mimba ukiwa nyumbani. Una fahamu jinsi ya kupima mimba kwa kutumia chumvi na mkojo? Usiwe na shaka, makala haya yata kuelimisha zaidi kuhusu jinsi ya kufanya kipimo hiki ukiwa nyumbani bila shaka yoyote na pia kwa kutumia vitu ambavyo viko kwa nyumba yako.

Ni ishara zipi ambazo umeshuhudia zilizo kusukuma kutaka kujua iwapo una mimba ama la? Tu

kupima mimba kutumia chumvi na mkojo

 

Ishara iliyo maarufu zaidi ni kukosa kipindi chako cha hedhi. Ila ni vyema kutia akilini kuwa kukosa kipindi chako cha hedhi sio ishara kuwa una mimba wakati wote. Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikakufanya ukose kushuhudia kipindi chako cha hedhi. Hakikisha una angalau ishara tatu za mimba kabla ya kufanya uamuzi wowote.

Ishara za mimba ni:

 • Kukosa kipindi cha hedhi
 • Kuhisi uchovu
 • Kichefu chefu
 • Ugonjwa wa asubuhi
 • Hamu ya kula iliyo ongezeka

Jinsi ya  kupima mimba kwa kutumia chumvi na mkojo

Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Chumvi Na Mkojo

Vitu unavyo hitaji

 • Mkojo- asubuhi
 • Chumvi
 • Kontena safi isiyo na rangi

Utaratibu wa kufuata

 1. Okota angalau nusu kikombe cha mkojo. Una shauriwa kutumia mkojo wa asubuhi punde tu unapo amka kabla ya kufanya kitu chochote.
 2. Weka mkojo huo kwenye kontena. Hakikisha kuwa kontena hiyo haina rangi ili uweze kuona kinacho endelea ndani.
 3. Ongeza chumvi kwenye kontena hiyo.
 4. Kuwa makini kuangalia mabadiliko yoyote kwenye kontena.
 5. Mchanganyiko ule ukibadilika rangi uwe mweupe, hiyo ni isha kuwa una mimba.
 6. Iwapo rangi ya mkojo haitabadilika, hiyo ni ishara kuwa hauna mimba.

Iwapo umekuwa ukitatizika na njia ya kutumia kupima mimba ukiwa nyumbani bila watu kujua ama iwapo hauna vifaa vya zahanati vya kupima mimba. Usiwe na shaka, utaratibu tulio angazia utakusaidia pakubwa. Pia hauta hitajika kununua chochote kwani unatumia vitu vilivyo jikoni mwako.

Kumbukumbu:webmd

Written by

Risper Nyakio