Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

Je, umekuwa ukihisi kana kwamba mwili wako una badilika na una ugonjwa usio kuwa na uhakika kuuhusu. Una zifahamu ishara hizi?

  • Kuhisi kutapika mara kwa mara.
  • Kuenda msalani baada ya kila dakika chache
  • Chuchu zilizo laini na zilizo fura
  • Kuhisi uchovu mwingi hata asubuhi unapo amka
  • Kuumwa na tumbo mara kwa mara
  • Kukosa hamu ya kula na kutamani vyakula fulani
  • Kukosa kipindi chako cha hedhi

Hongera! Hizi ni ishara za mapema za mimba. Kuna mbinu nyingi ambazo unaweza tumia kudhihirisha ukweli wa mambo ikiwa una mimba ama hizi ni ishara za tatizo lingine la kiafya. Unaweza kutumia mbinu za kiasili kama vile kupima mimba kwa kutumia dawa ya mswaki.

Umuhimu wa kufanya kipimo cha mapema cha mimba

Vipimo Rahisi Vya Mimba Vya Kinyumbani Visivyo Hitaji Fedha

Kipindi cha ujauzito ni kipindi nyeti na mama anapaswa kuwa makini sana na mambo anayo yafanya katika kipindi hiki. Hii ndiyo sababu kwa nini anashauriwa kupima mimba ingali changa ili kubainisha ikiwa kwa kweli ana tarajia kujifungua ama la. Kwa kufanya hivi, atachukua hatua zinazo faa katika kuhakikisha kuwa ako salama na pia maisha ya mtoto aliye tumboni mwake anazidi kukua kwa afya.

Ikiwa shaka yako ni jinsi ya kufanya kipimo cha nyumbani cha mimba, usiwe na shaka tena kwani kuna mbinu nyingi za kufanya hivi kwa kutumia bidhaa ulizo nazo jikoni mwako. Vipimo hivi vya kinyumbani vinakuwezesha kupima mimba kwa usiri wa nyumba yako, bila kutumia pesa zozote na bila kutumia wasaa mwingi kwenda kwenye zahanati ama kituo cha afya kufanyiwa vipimo hivi.

Baada ya kufanya kipimo hiki na kubaini hali yako, utaweza kufanya uamuzi baada ya hapo. Utunzaji kabla ya kujifungua ni lazima kwa mama mwenye mimba. Kwa hivyo kufanya kipimo cha mapema kama vile kwa kutumia njia ya kupima mimba kwa kutumia dawa ya mswaki, kutakuwezesha kuwasiliana na daktari wako ili akuanzishie vitamini ambazo ni muhimu sana katika hatua za mapema za mimba.

Kumbuka kujitenga na vileo, dawa za kulevya na sigara katika kipindi hiki. Kula chakula chenye afya kwani kuna kiumbe kinacho kua ndani yako na chakula chako ndicho kinacho mrutubisha.

Soma Pia:Mbinu 4 Za Kupima Mimba Zilizo Tumika Na Nyanya Zetu

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio